Mwezi Julai mwaka 1950, Chuo Kikuu cha Qinghua kiliandaa darasa la mafundisho ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi kutoka nchi za Ulaya Mashariki. Kilikuwa chombo cha kwanza nchini China kilichoshughulikia mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje.
Mwaka 1952, Bwana Zhu Dexi na wenzake walitumwa nchini Bulgaria na Korea ya Kaskazini kufundisha lugha ya Kichina, wakifungua ukurasa wa China mpya kutuma walimu wa lugha ya Kichina katika nchi za nje. Hadi mwaka 2004, China kwa jumla iliwatuma walimu 1314 wa lugha ya Kichina katika nchi mbalimbali duniani.
Mwaka 1958, kitabu cha kwanza cha kirusi cha mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje kilichapishwa. Hadi leo, vitabu zaidi ya aina 1000 vya kiada vya mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje vimechapishwa. Mwaka 1961, kuwachagua wanafunzi wahitimu kutoka kitivo cha lugha ya Kichina na lugha za kigeni cha vyuo vikuu 11, ambao ni kama akiba ya walimu wa kufundisha lugha ya Kichina ng'ambo.
Mwezi Aprili mwaka 1962, Radio Beijing (sasa inaitwa Radio China Kimataifa) ilianzisha kipindi cha "kujifunza Kichina" katika idhaa ya lugha Japan. Hivi sasa Radio China Kimataifa kila siku inatangaza kipindi cha "Kujifunza Kichina" katika lugha 39 za kigeni.
Mwezi Januari mwaka 1965, chuo cha maandalizi kwa wanafunzi wa nchi za nje kilibadilishwa rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Lugha cha Beijing. ambacho ni chuo kikuu pekee kinachoshughulikia hasa mafundisho ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa nchi za nje, pia ni kituo muhimu cha kutoa mafundisho na kufanya utafiti wa lugha ya Kichina kwa nje. Hivi sasa China ina vyuo vikuu 420 vinavyoshughulikia mafundisho ya lugha ya Kcihina kwa nje.
Katika likizo ya majira ya joto mwaka 1978, Chuo Kikuu cha Lugha cha Beijing kiliwaandikisha wanafunzi waliojifunza lugha ya Kichina kutoka Ufaransa, huu ni mwanzo wa kuandaa mafundisho ya muda ya lugha ya Kichina. Hivi sasa mafundisho ya muda yamekuwa mtindo muhimu wa kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa nje.
Mwezi Mei mwaka 1980, vitabu vya kwanza vya kiada vya mafundisho ya muda ya lugha ya Kichina vilichapishwa.
Mwezi Oktoba mwaka 1981, video vya televisheni vya mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje vya "Lugha ya Kichina" vilikamilika.
Mwaka 1984, wizara ya elimu ya China iliikabidhi Chuo Kikuu cha Lugha cha Beijing madaraka ya kutunga mtihani wa kiwango cha Kichina HSK, mtihani huo ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 1990. Hadi leo, vituo 137 vya mtihani huo vimewekwa katika nchi na sehemu 37 duniani, na kuwashirikisha watu zaidi ya laki nne.
Mwaka 1985, Chuo Kikuu cha Lugha Cha Beijing, Chuo Kikuu cha Lugah za Kigeni cha Beijing, Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Shanghai na Chuo Kikuu cha Ualimu cha China Mashariki vilianzisha kozi ya mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje. Hivi sasa vyuo vikuu 62 vya China vina kozi hiyo, kila mwaka kuwaandaa wanafunzi 4000.
Mwezi Agosti mwaka 1985, kongamano la kwanza la kimataifa kuhusu mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje lilifanyika mjini Beijing, wawakilishi 260 kutoka nchi na sehemu 20 walihudhuria kongamano hilo. Kongamano la nane la kimataifa kuhusu mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje lililofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi Julai mwaka 2005 limewashirikisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 30.
Mwaka 1987, kikundi cha uongozi wa mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje kilichoundwa na viongozi wa idara 11 za baraza la serikali kilianzishwa, na kuweka ofisi yake katika wizara ya elimu ya China.
Mwezi Septemba mwaka 1987, jarida la taaluma la mafunzo ya lugha ya kIchina kwa nje "Mafundisho ya lugha ya Kichina Duniani" lilianza kuchapishwa.
Mwaka 1990, kamati ya elimu ya taifa la China ilitangaza "Utaratibu wa kuthibitisha sifa ya walimu wa mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje", ambao ulitekelezwa kuanzia mwaka uliofuata. Hadi mwaka 2004, watu 5361 walipata vyeti hivyo. Mwaka 2004, wizara ya elimu ya China ilitoa "Utaratibu wa kuthibitisha uwezo wa kufundisha lugha ya Kichina kama lugha ya kigeni".
Mwaka 1998, kozi ya mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje iliorodheshwa kama moja ya kozi za shahada ya udaktari.
Mwaka 1999, wizara ya elimu iliweka rasmi "Tuzo ya urafiki ya utamaduni wa lugha ya China". Hadi leo, wageni 10 wa nchi za nje wamepata yuzo hiyo.
Kuanzia mwaka 2001, wizara ya elimu ya China kwa nyakati tofauti iliidhinisha vyuo vikuu 11 vikiwemo Chuo Kikuu cha Heilongjiang na Chuo Kikuu cha Yunnan kama Vyuo Vikuu vya kuunga mkono mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nchi za majirani. Chuo Kikuu cha Lugha cha Beijing, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing, Chuo Kikuu cha Fudan cha Shanghai, Chuo Kikuu cha Beijing, Chuo Kikuu cha Nanjing, Chuo Kikuu cha Ualimu cha China Mashariki, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Nanjing na Chuo Kikuu cha Watu wa China kama vituo vya kitaifa vya kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa nje.
Mwezi Agosti mwaka 2002, kikundi cha uongozi wa mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje kiliendesha mashindano ya kwanza ya lugha ya Kichina "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu duniani. Mashindano hayo yanaendeshwa kwa mwaka, kwa jumla wagombea 186 kutoka nchi 41 duniani wamekuja China kushiriki katika mashindano hayo ya fainali. Mashindano ya nne ya fainali yalifanyika mjini Beijing mwezi Julai mwaka 2005, ambayo yaliwashirikisha wanafunzi 100 kutoka nchi 50 duniani.
Mwezi Septemba mwaka 2002, wizara za elimu za China na Marekani zilianzisha mradi wa mafundisho ya lugha kwenye mtandao wa China na Marekani. Mradi huo unalenga kutoa mfumo wa mtandao wa kuwaelimisha watoto tokea umri wa miaka 12 hadi 15 kujifunza lugha ya nchi nyingine. Mwaka 2003, ofisi ya uongozi wa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa nje ya China ilianza kutekeleza mradi wa kuwaalika wasomi wa lugha ya Kichina wa nchi za nje kutembelea China kwa muda. Mpaka sasa wasomi 83 wa nchi za nje wamenufaika kutokana na mradi huo.
Tarehe 15 Aprili mwaka 2004, wizara ya elimu ya China ilianzisha rasmi mradi wa walimu wachina waliojitolea kufundisha lugha ya Kichina nje, hivi sasa walimu 447 waliojitolea wanafundisha lugha ya Kichina katika nchi 14 duniani.
Mwezi Mei mwaka 2004, baraza la serikali liliidhinisha mradi wa "daraja la lugha ya Kichina", ambao umefanya mpango wa mafundisho ya lugha ya Kichina kwa nje katika miaka 5 ijayo.
Tarehe 21 Novemba mwaka 2004, Chuo Kikuu cha kwanza cha Confucius kilianzisha mjini Seoul. Ilipofika tarehe 20 mwezi Juni mwaka 2005, vyuo vikuu 8 vya Confucius vilianzishwa rasmi duniani, na mashirika mengine 50 duniani yako mbioni kufanay ushirikiano na China.
Kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2004, China iliwaandaa walimu elfu 23 wa lugha ya Kichina wa nchi za nje, wengi wao walipewa mafunzo katika nchi zao. Tarehe 20 hadi 22 Julai mwaka 2005, mkutano wa lugha ya Kichina duniani ulifanyika mjini Beijing. Hii ni mara ya kwanza kwa China kufanya kongamano la kimataifa la ngazi ya juu kuhudu lugha ya Kichina. Kauli mbiu ya mkutano huo ni maendeleo ya lugha ya Kichina katika mfumo wa kuwa na aina nyingi za utamaduni duniani.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-04
|