Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-04 20:44:47    
Mji wa Chengdu

cri

Mji wa Chendu ni mji muhimu ulioko kusini magharibi mwa China tokea enzi za kale. Ulikuwa mji mkuu wa dola la Shu katika Enzi ya Madola matatu na mji mkuu wa dola la Shu ya kwanza na Shu ya pili katika kipindi cha Enzi Tano na Madola kumi. Urithi wa kiutamaduni mjini humo ni mwingi. Mwaka 1982 mji wa Chengdu uliwekwa kwenye orodha ya miji maarufu yenye historia ndefu na utamaduni mkubwa na baraza la serikali ya China. Mji wa Chengdu una historia ya zaidi ya miaka 2300. Tangu Enzi za Qin na Han, mji wa Chengdu ulikuwa ni mji maarufu kutokana na kilimo, kazi za mikono na utamaduni uliostawi sana. Na ulikuwa kituo cha siasa, uchumi na utamaduni kusini magharibi mwa China katika enzi mbalimbali.

Kuna maliasili nyingi za viumbe mjini Chengdu. Mimea adimu ni pamoja na miti ya gingko na miti ya njiwa. Wanyama adimu ni pamoja na panda wakubwa, panda wadogo na kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu. Na kuna aina zaidi ya 860 za dawa za mitishamba. Pia kuna maliasili nyingi za utalii. Vivutio vya utalii na mabaki ya kihistoria ni maarufu nchini na duniani. Kuna masalio 19 ya kihistoria ya ngazi ya kitaifa na kimkoa. Kituo cha utafiti wa panda wakubwa kiko mjini humo. Sehemu ya kijiografia ya mji huo ni mzuri.

Mji wa Chengdu unatilia maani sana kuanzisha mazingira mazuri kwa uwekezaji. Na hali ya ufunguaji mlango wa pande zote na sekta mbalimbali imeanzishwa. Mashirika ya mji huo yanafanya juhudi kuingia kwenye masoko ya nchi za nje, na mauzo ya bidhaa katika nchi za nje yanaongezeka kwa kiasi kikubwa.

Eneo la sehemu zinazofunikwa na majani na misitu mjini humo linaongezeka kwa haraka. Mwaka 1986, eneo lililopangdwa miti milimani lilifikia lengo lililowekwa. Mwaka 1997, eneo la ujumla lililopandwa na miti lilifikia lengo lililowekwa. Mwaka 1999, eneo lililopandwa miti mjini Chengdu lilifikia asilimia 32.22, ambalo liliongezeka kwa asilimia 22 kutoka asilia 10.2 mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita. Eneo la ujumla la misitu lilifikia hekta 227856.84.

Mji wa Chengdu unashikilia mkakati wa maendeleo endelevu, miradi ya kuhifadhi mazingira vikiwemo viwanda vya kusafisha maji machafu na kushughulikia takataka vinajengwa haraka, uchafuzi viwandani umedhibitiwa vizuri. Wilaya 8 za mji wa Chengdu zimewekwa kuwa sehemu za kielelezo cha hifadhi ya maumbile ya ngazi ya kitaifa. Mradi wa Mto Funan umeleta ufanisi mkubwa wa kiuchumi, kijamii na hifadhi ya mazingira, ambao umesifiwa na watu nchini China na duniani, na ulipewa tuzo ya makazi ya binadamu, tuzo ya uvumbuzi wa kwanza na tuzo ya mfano mzuri na Umoja wa Mataifa.

picha husika>>

1  2