Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-05 20:16:52    
Utamaduni na sanaa nchini China 1

cri

Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, uliwekwa mkururo wa sera za utamaduni za kuhimiza michezo ya aina mbalimbali isitawishwe na kuwatumikia umma na ujamaa, kupokea mambo mazuri ya kale na ya nchi za nje, yote hayo yameweka msingi imara kwa ukuaji wa utamaduni na sanaa.

Michezo mingi mizuri ya kijadi ilifanyiwa utafiti na kutengenezwa upya, ambapo opera ya kiulaya, muziki wa symphony, filamu na nyinginezo pia zimeendelezwa.

Kuanzia mwaka 1949 hadi mwaka 1979, wasanii walitoa mchango mkubwa katika kufanya mageuzi ya sanaa za kijadi, na kupokea sanaa zilizotoka nje, ambapo michezo mingi mizuri ya sanaa ilitolewa nao.

Kwa mfano, mchezo mkubwa uitwao "Mashariki Kwekundu"

ulieleza historia ya mapinduzi ya China ya kupambana na ubeberu na umwinyi katika miaka karibu mia moja .

Michezo ya balet iitwayo "Jeshi jekundu la wanawake", na "Msichana mwenye nywele nyeupe" ilieleza majonzi ya wakulima wa China ya zamani na mapigano yaliyofanywa na wanawake wa China wa kujipatia uhuru na ukombozi.

Michezo mingi ya opera ya kibeijing , ilifanyiwa mageuzi juu ya maonyesho na uimbaji wa kijadi , ikawapendeza watu zaidi.

Katika kipindi hiki, filamu za "Mwezi wa pili wa Spring" , "Duka la Bwana Lin" na "Madada wa kimchezo" zilionyesha maisha ya makabwela na wasomi wa China ya zamani.

Tangu yafanywe mageuzi na ufunguaji mlango wazi kwa nje mwaka 1979, mabadiliko makubwa ya kihistoria yalitokea nchini China,ambapo maisha ya watu yanaboreshwa siku hadi siku, na burudani ya kiroho pia inatiliwa maaani zaidi na watu, wasanii walitunga michezo mingi mizuri kwa kufuatilia hali halisi ya

maisha ya watu, na kupokea zaidi mafanikio yote mazuri na ya kimaendeleo ya utamaduni na sanaa za kale na za nchi za nje.

Katika miaka 20 hivi illiyopita, China ilifanya kazi nyingi katika kuhifadhi na kupokea utamaduni na sanaa za kijadi, na kuufanya utamaduni na sanaa za kijadi ziendelezwe zaidi.

Michezo ya kienyeji ya China ni sehemu kubwa mojawapo ya utamaduni wa kijadi wa China, michezo mingi mizuri ya kikale yenye mvuto wa kisanaa usiodidimika ikionyeshwa tena jukwaani baada ya kuachwa katika mapinduzi ya utamaduni ya miaka kumi, ( Kama vile Mchezo wa opera ya kibeijing wa "Makutano ya njia tatu", mchezo wa opera ya kiping uitwao "Mshenga maua ", mchezo wa opera ya kihuangmei uitwayo "Mkulima aoana na malaika" na mingineyo ) ikakaribishwa na watazamaji .

Wakati huo huo, maelfu ya vikundi vya michezo ya kienyeji nchini kote China kila mwaka hutoa michezo mizuri kulingana na mahitaji ya jamii na kuwaburudisha watazamaji .

Kwa mfano michezo ya opera ya kibeijing iitwayo: "Caochao na Yangxiuo" na "Phonix arudi kiotani" iliongezwa tafsiri mpya ya zama za kisasa ikakaribishwa na watazamaji na kuwa vielelezo vya michezo ya aina hiyo.

Tamasha kubwa hizo (ya "kuadhimisha mwaka wa 200 tangu kikundi cha opera ya kihui kingie Beijing kwa maonyesho" na ya "kuadhimisha miaka 100 tangu Mei Lanfang na Zhou Xinfang wazaliwe,) zilionyesha vilivyo ukuaji wa opera ya kibeijing katika zama tulizo sasa nchini China.

Zaidi ya hayo, michezo mingi mizuri ya opera za kienyeji ilitolewa pia, kama vile "Jenerali chui" , "Matunda mekundu yameshaiva", "Baoyu mwenye ukorofi", "Ndoto ya Jumba jekundu" "Mabadiliko ya uso" na kadhalika ilionyesha kisanaa fasihi maarufu ya kale ya China na sanaa ya ajabu ya utamaduni wa kijadi wa China.

Hivi sasa kuna aina zaidi ya 300 za michezo ya sanaa ya asili inayooenea miongoni mwa makabila mbalimbali na mikoa yote nchini humo. Michezo mingi ya kuwasifu mashujaa wa taifa, maofisa wenye maadili na mapenzi ya utiifu inakaribishwa siku zote na watazamaji.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-05