Bw. Yin Mingshan ni mmoja wa wanaviwanda waliopata mafanikio, yeye alikuwa mwalimu, mwandishi wa habari, mhariri, mfanyabiashara wa jumla wa vitabu na kuwa mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha serikali. Alipokuwa na umri wa miaka 54 aliamua kujiajiri na alianzisha kiwanda cha pikipiki kwa mtaji wa Yuan laki 2. kiwanda chake baada ya kuendelea kwa miaka zaidi ya 10, hivi sasa kimekuwa kiwanda cha injin za pikipiki zenye haki-miliki chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya milioni 2, zile zinazosafirishwa nchi za nje zinamletea dola za kimarakani kiasi cha milioni 200 kwa mwaka.
Bw. Yin Mingshan alizaliwa katika mkoa wa Sichuan, sehemu ya kusini maghribi ya China. Yeye ana urefu wa mita 1.8, kwao anahesabiwa kuwa ni mrefu, kazi ya ualimu aliyofanya imemfanya aonekana kama msomi, na anaonekana kukosa ujanja wa wafanya-biashara, lakini amefanikiwa sana katika shughuli zake za biashara. Bw. Yin Mingshan alipozungumzia maendeleo ya kiwanda chake, alisema,
"Mwaka juzi nilitembelea Marekani, mwanakiwanda mmoja wa Marekani aliniuliza kiwanda changu ni kikubwa kiasi gani? Nilimjibu kuwa kiwanda changu kina uwezo wa kuzalisha injin za pikipiki milioni 2 na laki 5, na zaidi ya milioni 1 zinasafirishwa nchi za nje."
Bw. Yin alisema kuwa kiwanda chake kilijengwa mwaka 1992 na kinajulikana kwa "Lifan", mwanzoni kabisa kiwanda hicho kilikuwa na wafanyakazi 9 tu, lakini baada a kuendelezwa kwa miaka 10 tu, sasa kina wafanyakazi zaidi ya 4,000 na thamani ya Yuan karibu bilioni 1.2. Hivi sasa, pikipiki na injin za pikipiki zinazozalishwa na kiwanda cha Lifan zinasafirishwa katika nchi na sehemu zaidi ya 100 za Asia ya kusini mashariki, Asia ya magharibi, Ulaya, Afrika na Amerika ya kusini. Mwaka 2004 idadi ya jinjin za pikipiki, pato la fedha za kigeni na kiwango cha haki-miliki ya kielimu vilichukua nafasi ya kwanza katika sekta hiyo nchini China.
Mwandishi wetu wa habari alipofanya matembezi nchini Vietnam na Philipins aliona kuwa pikipiki za "Lifan" zimekuwa bidhaa zinazopendwa na watu wa huko. Vietnam ni soko la kwanaa kufungua kiwanda hicho katika nchi za nje. Katika duka moja la pikipiki mwenye duka bibi Nguyen Thanh Thanh alisema kuwa pikipiki za Lifan zinauzwa vizuri huko.
"Vipuri vya pikipiki za Lifan vinaweza kubadilishwa bila malipo, na zinatunzwa bure pia, kiwanda kinatoa huduma nzuri sana, hivyo zinanunuliwa kwa wingi na watu."
Sababu ya kuweza kupata mafanikio makubwa kwa kiwanda cha pikipiki cha Lifan ni kutokana na mtazamo sahihi wa Bw. Yin. Mwaka 1998 baada ya kufanya uchunguzi katika soko la kimataifa la pikipiki, Bw. Yin aliona kuwa katika nchi jirani ya China, Vietnam, karibu kila mtu ana pikipiki, hili ni koso kubwa, hivyo aliichukulia Vietnam kuwa ni soko lake la kwanza katika nchi za nje. Lakini wakati ule pikipiki zilizozalishwa na viwanda vya Japan zilikuwa zimechukua 98% ya nafasi ya soko la pikipiki la Vietnam, kwa kukabiliwa na mshindani mkubwa wa Japan, Bw. Yin Mingshan hakuwa mwoga bali aliamua kithabiti kuingia soko hilo. Alisema,
"Vietnam iko karibu zaidi na China, gharama ya usafirishaji ni ndogo. Bei ya pikipiki za China ni rahisi sana, pikipiki za China zinauzwa dola za kimarekani 700 tu kabla kusafirishwa kutoka China, ikilinganishwa na pikipiki za Japan ambazo bei yake huko Vietnam ni dola za kimarekani 2,100."
Katika soko la Vietnam, licha ya kutumia ubora wa bei rahisi, kiwanda cha Lifan kilifanya shughuli nyingi za kujisogeza karibu na wateja zikiwa ni pamoja na kufanya maonesho ya michezo, kushirikisha kwenye mashindano ya soka kati ya China na Vietnam ili kuongeza sifa za kiwanda cha Lifan, hivi sasa pikipiki za kiwanda cha Lifan zimechukua 70% ya nafasi za soko la Vietnam.
Maendeleo makubwa kiliyopata kiwanda cha Lifan yaliimarisha imani ya Bw. Yin Mingshan ya kupanua soko la pikipiki za kiwanda chake katika nchi za nje. Mwaka 2003 Bw. Yin alitupia macho soko la nchi za Afrika. Mwaka ule alishirikisha maonesho ya pikipiki za kiwanda cha Lifan na maonesho ya Gongfu ya kikundi cha Wuhan katika Nigeria, ambayo yalivutia watu wengi wa huko. Hivi sasa siyo tu watu wa kawaida wa huko wanapenda pikipiki za Lifan, hata balozi wa Nigeria nchini China Bw. Jonathan Oluwole Coker anaipenda. Sasa Nigeria imekuwa soko la kwanza kwa ukubwa miongoni mwa masoko matano ya kiwanda cha Lifan katika nchi za nje.
Idhaa ya kiswahili 2005-08-09
|