Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-10 21:14:06    
Mapishi ya vipande vya nyama ya ng'ombe kwa pilipili hoho na pilipili manga

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 1500, unga wa pilipili hoho gramu 75, pilipili kima gramu 20, vipande vya tangawazi na vitunguu maji kila gramu 25, mchuzi wa soya gramu 50, chumvi gramu 50, mvinyo wa kupikia gramu 30, sukari gramu 50, ufuta gramu 100, M.S.G gramu 30, mafuta gramu 50.

Njia

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vikubwa, na uviweke ndani ya maji yaliyochemshwa, tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji, pilipili kima, endelea kuchemsha kwa moto mdogo, mpaka viive, vipakue na uvikaushe, uvikate viwe kama vipande vya slesi.

2. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe nyuzi 60, tia slesi ya nyama ya ng'ombe, ikaange na ipakue.

3. pasha tena moto na tia unga wa pilipili hoho, tangawizi, korogakoroga, halafu tia slesi ya nyama ya ng'ombe na mimina maji mpaka yafunike slesi ya nyama ya ng'ombe. Tia chumvi, mchuzi wa soya, sukari, mvinyo wa kupikia, baada ya kuchemka punguza moto kidogo na endelea kuchemsha na kukorogakoroga, halafu mimina mafuta ya ufute, uipakue. Tia wanga ya pilipili hoho na ufute, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.