Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-16 17:50:03    
Ushirikiano wa kiuchumi katika eneo la delta ya mto Zhujiang wapata mafanikio

cri

Mkutano wa pili wa baraza la ushirikiano na maendeleo wa eneo la mto Zhujiang ulifanyika hivi karibuni huko Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan ulioko sehemu ya kusini magharibi ya China. Eneo hilo ambalo ni la kwanza kwa ukubwa miongoni mwa maeneo ya ushirikiano ya kiuchumi nchini, limepata mafanikio makubwa katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita tangu lianzishwe.

Eneo la delta ya mto Zhujiang ni pamoja na mikoa 9 ya Fujian, Jiangxi, Hunan, Guangdong, Guangxi, Hainan, Sichuan, Guizhou na Yunnan pamoja na mikoa miwili ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macau iliyoko kwenye sehemu za kusini mashariki, kusini na kusini magharibi. Eneo la mikoa 9 ya China bara limezidi kilomita za mraba milioni 2, idadi ya watu na uwezo wa uzalishaji mali wa eneo hilo vimefikia kiasi cha theluthi moja ya jumla ya idadi ya watu na uwezo wa uzalishaji mali wa China nzima.

China bara katika eneo hilo licha ya kuweko sehemu zilizoendelea za Guangdong, Hong Kong na Macau, vile vile kuna sehemu zilizokuwa nyuma kiuchumi za Jiangxi, Hunan, Guizhou na Guangxi.

Mwaka 2004 ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la delta ya mto Zhujiang na kuhimiza maendeleo ya pamoja ya eneo hilo zima, mikoa 9 na mikoa miwili ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macau iliitisha mkutano wa kwanza wa baraza la ushirikiano na maendeleo la eneo la delta ya mto Zhujiang, ambapo ilisaini mkataba wa ushirikiano na kuchukulia sekta kumi zikiwemo miundo-mbinu, uzalishaji na uwekezaji, biashara na utalii kuwa sekta muhimu za kufanya ushirikiano. Utiaji saini wa mkataba huo unamaanisha kuwa ushirikiano wa eneo la delta la mto Zhujiang umeingia rasmi kipindi cha utekelezaji.

Hadi sasa ni mwaka mmoja umepita, hali ya maendeleo ya ushirikiano wa eneo hilo ikoje? Mkuu wa mkoa wa Guangdong aliyeshiriki mkutano wa baraza la ushirikiano na maendeleo ya eneo la delta ya mto Zhujiang Bw. Huang Huahua alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,

"Katika muda huo wa mwaka mmoja uliopita, kutokana na jitihada za pamoja za serikali na sekta mbalimbali za jamii za eneo hilo la ushirikiano wa uchumi ushirikiano wa uchumi wa viwanda vya eneo hilo umepata ufanisi dhahiri. Tumeanzisha mfumo wa ushirikiano wa viwanda vya eneo hilo, hivi sasa ushirikiano huo unaendelezwa kwa undani zaidi. Tumepata maendeleo makubwa katika baadhi ya sekta muhimu zikiwemo za mawasiliano na nishati, licha ya hayo mazingira ya soko huria yanaboreshwa hatua kwa hatua."

Ofisa husika anaona kuwa ushirikiano wa eneo la delta la mto Zhujiang kwa kiwango kikubwa umetatua upungufu wa mali asili na nguvukazi unaozikabili sehemu zilizoendelea za mikoa ya Guangdong, Hong Kong na Macau katika maendeleo yake. Kwa upande mwingine, sehemu zilizokuwa nyuma kiuchumi zinaweza kupata mitaji, teknolojia na zana inazozihitaji sana, sehemu hizo zinaweza kubadilisha ubora wake wa raslimali kuwa ubora wa uchumi na kupunguza tofauti kati yake na sehemu zilizoendelea. Kuhusu hayo, kiongozi kutoka mkoa wa Sichuan ambaye ni mshiriki wa mkutano wa baraza hilo Bw. Zhang Xuezhong alisema,

"Katika ushirikiano wa eneo la delta ya mto Zhujiang, ubora wa mkoa wa Sichuan umefungamana barabara na ubora wa sehemu ya mashariki. Sichuan ina nguvukazi nyingi na ya bei rahisi, zaidi ya hayo raslimali za maji na utalii zinajulikana sana nchini China ingawa sehemu ya mashariki imeendelea sana, lakini katika miaka ya karibuni nafasi yake imezuiliwa, na gharama ya nguvu kazi yake ya kazi pia imekuwa ikiongezeka. Wanaweza kuhamisha shughuli za uzalishaji katika sehemu yetu, hatua ambayo itanufaisha pande zote mbili."

Habari zinasema kuwa katika mazungumzo ya ushirikiano wa uchumi na biashara wa eneo la delta ya mto Zhujiang ambayo yalifanyika kwa wakati mmoja na mkutano wa baraza la eneo hilo, miradi iliyooneshwa na mkoa wa Sichuan ya uzalishaji umeme kwa gesi ya asili, nishati na kemikali ilivutia wawekezaji wengi. Hatimaye viwanda vitano katika eneo la delta ya mto Zhujiang vilisaini mkataba wa uwekezaji pamoja na mji wa Dazhou wenye thamani ya Yuan bilioni 14. Meya wa mji wa Dazhou Bw. Li Xiangzhi alisema kuwa miradi hiyo ya ushirikiano wa nishati italeta nafasi ya maendeleo kwa pande zote mbili.

"Uunganishaji wa mitaji, teknolojia na usimamizi wa kimaendeleo vya sehemu ya pwani na raslimali na viwanda vya sehemu ya ndani ya China bara utaanzisha hali ya kunufaishana. Ili kuharakisha uchimbaji wa raslimali ya gesi ya asili ya Dazhou, tutaimarisha ujenzi wa miundo-mbinu, kutoa huduma nzuri na kufanikisha ushirikiano wetu."

Hong Kong na Macau ni wawekezaji wakubwa katika eneo hilo la ushirikiano, hadi hivi sasa uwekezaji wa Hong Kong katika eneo hilo umefikia dola za kimarekani bilioni 150. Mkuu wa mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong Bw. Zeng Yinquan alisema kuwa Hong Kong itafanya kazi muhimu katika ushirikiano wa eneo la delta ya mto Zhujiang."

Katika mkutano wa baraza hilo, pande mbalimbali zilikuwa na majadiliiano kuhusu kuboresha mfumo wa ushirikiano wa kikanda, kuanzisha mfumo wa uratibu wa soko huria na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-16