Mahitaji
Korosho gramu 100, nyama ya kuku gramu 200,pilipili mboga gramu 80, karoti gramu 80, tangawizi gramu 5, ute wa yai moja, chumvi gramu 10, wanga gramu 10, mvinyo wa kupikia gramu 5, na mafuta gramu 30.
Njia
1. Kata nyama ya kuku iwe vipande vidogo tia ute wa yai, chumvi na wanga, kuviweka kwa dakika 10. Kata pilipili mboga na karoti ziwe vipande. Mimina maji kwenye sufuria kisha pasha moto, na baada ya kuchemsha tia vipande vya karoti kwenye maji ya moto, halafu uvipakue na kuvikausha.
2. pasha moto tena, tia mafuta kidogo kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya 60, tia korosho ndani ya sufuria korogakoroga uipakue. Tia mafuta kwenye sufuria tena, na tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga na uvipakue.
3. pasha moto tena, tia vipande vya tangawizi, pilipili mboga na karoti, koroga koroga, halafu tia korosho na vipande vya nyama ya kuku, tia chumvi, mvinyo wa kupikia na maji ya wanga, koroga koroga, na uvipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|