Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-19 20:43:39    
China yachukua hatua kuhifadhi maliasili ya misitu

cri

Hivi sasa serikali ya China imeongeza zaidi mkakati na sera kuhusu hifadhi ya mazingira, ili kuhakikisha binadamu na mazingira vinaishi kwa kupatana wakati China inapotimiza maendeleo mazuri ya kasi ya uchumi na jamii.

Tokea miaka ya 50 ya karne ya 20, China ilipanda miti mingi na kujenga eneo la misitu kwa nguvu za binadamu. Tokea mwaka 1981 hadi mwaka 2002, miti iliyopandwa na wananchi wa China ilifikia zaidi ya bilioni 39.8. Hivi sasa eneo la miti iliyopandwa nchini China limefikia hekta milioni 46.67, eneo hili ni 26 % ya lile la jumla ya eneo la miti iliyopandwa duniani, linachukua nafasi ya kwanza duniani, na eneo la misitu la China limefikia 16.55 %. Katika hali ambayo maliasili ya misitu duniani inapungua siku hadi siku, China imedumisha upanuzi wa eneo la misitu na idadi ya miti, China imeorodheshwa na Shirika la hifadhi ya mazingira la Umoja wa Mataifa kuwa moja kati ya nchi 15 zenye misitu mingi zaidi duniani.

Tokea mwaka 1998 hadi mwaka 2001, serikali kuu ya China ilitenga yuan bilioni 42.7 katika hifadhi ya misitu na mbuga kwenye sehemu ya magharibi ya kati wanakoishi watu wengi zaidi wenye matatizo ya kiuchumi, kutoa ruzuku kwa wakulima wa huko na kuwahamasisha watu kupanda miti kwenye mashamba yaliyochimbuliwa kupita kiasi, au kupanda majani kwenye mashamba kama hayo ili yawe malisho. Mradi wa kufufua misitu kwenye ardhi za misitu zilizotumiwa kuwa mashamba ya kulima ulianzishwa katika mikoa na miji 25 nchini, ilipofika mwaka 2002, miti imepandwa tena katika ardhi zenye hekta milioni 6.44 zilizotumiwa kuwa mashamba ya kulima. Ufanisi wa hatua ya mwanzo umeonekana, ambapo hali ya mmomonyoko wa ardhi imeboreshwa kwa kiasi fulani. Na kuanzia mwaka 1998, mradi wa kuhifadhi misitu asilia ulianzishwa kote nchini na kupata mafanikio, mradi huo unataka sehemu zote nchini kuacha kukata miti ya misitu ya asili, katika sehemu nyingi, wafanyakazi wa ukataji wa miti wamekuwa walinzi wa misitu.

Kwa kufuata lengo lililowekwa kwenye taarifa ya utafiti wa mikakati ya maendeleo endelevu ya shughuli za misitu za China, ifikapo mwaka 2050, eneo la misitu la China litafika 28 %.

Baada ya kufanya juhudi za zaidi ya miaka 30 iliyopita, mafanikio yaliyotambuliwa duniani yamepatikana katika hifadhi ya mazingira ya China. Katika mchakato wa kurekebisha miundo ya kiuchumi na kuongeza mahitaji nchini, China imeongeza kidhahiri nguvu ya hifadhi ya mazingira. Kwa ujumla, imedhibiti mwelekeo wa uchafuzi unaozidi kuwa mbaya kote nchini, na hali ya mazingira ya miji na sehemu kadhaa imeboreshwa kwa kiasi fulani na kuchangia utekelezaji wa mikakati ya maendeleo endelevu nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-19