Mafanikio makubwa sana yamepatikana katika uenezaji wa muziki wa symphony nchini China. Katika Jumba la muziki la Beijing , kila mwaka hufanywa maonyesho mara zaidi ya 300, na tamasha kubwa za muziki wa siku za spring na nyinginezo huwaburudisha watu sana . Hivi leo, wanamuziki wenye vipawa wa China wanajitokeza kizazi hadi kizazi.
China ni nchi yenye makabila mengi mbalimbali, kila kabila lina mila yake ya kuimba na kucheza ngoma. Takwimu iliyofanywa ilisema kuwa, nchini China kuna aina elfu moja hivi za ngoma za kienyeji. Kwa mfano: "Ngoma ya Dragon" na "Ngoma ya Simba", za wahan, "Ngoma ya Andei" ya wamongolia, "Ngoma ya Xienzi" ya watibet, "Ngoma ya Senemu" ya wawiur, "Ngoma ya Kuruka mwezi" ya wayi, "Ngoma ya tausi" ya watai, "Ngoma ya vipepeo" ya wakorea na kadhalika. Ngoma nyingi kama hizo za kijadi za makabila mbalimbali zenye thamani kubwa zimehifadhiwa na kupata kuendelezwa.
Katika historia ya ukuaji wa ngoma za kienyeji karibu nusu karne iliyopita, wasanii wengi mahodari walijitokeza na kutoa mchango kwa ajili ya kuendeleza ngoma za kitaifa za China. Wachezaji ngoma Jia Zuoguang, Dai Eilian, Zhao Qin, Bai Shuxiang na wachezaji vijana Yang Liping, Liu ming na wengineo ndio wakilishi miongoni mwao.
Juu ya msingi mkubwa wa ngoma za kichina, wasanii wa ngoma walivumbua aina mpya ya sanaa na kutoa michezo ya ngoma ya China , michezo ya ngoma iliyotolewa mwanzoni mwa miaka ya 50 hadi katikati ya miaka ya 60 iliweka msingi kwa maendeleo ya michezo ya ngoma ya China.
Hivi sasa kwa jumla imetolewa michezo mipya ya ngoma zaidi ya 100 ambayo imeonyesha maendeleo zaidi kuliko ile ya siku zilizopita.
Kwa mfano mchezo wa ngoma uitwao " Njia ya uchukuzi wa hariri" , ulionyesha historia ya njia hiyo kwa maonyesho safi na ya ajabu .
Elimu ya Sanaa ni msingi wa ujenzi wa utamaduni, hasa katika miaka kumi hivi iliyopita, China ilijitaihidi kuinua juu kiwango cha elimu ya taifa zima..
Nchini China kuna vyuo vikuu zaidi ya 30 vya kuwaandaa wasanii wa daraja la juu na walimu wa usanii na shule za katikati zaidi ya 130 za usanii maalum kwa kufundisha michezo ya opera za kienyeji, ngoma, sanaa ya uchoraji, filamu, televishin, na mengineyo, umeweka mfumo kamili wa elimu ya sanaa ambao umeweka msingi imara kwa maendeleo ya utamaduni na sanaa ya China.
Ujenzi wa majengo ya kimsingi ya utamaduni umezingatiwa kwa makini na kuendelezwa kwa haraka.
Majengo mengi kama vile Maktaba ya taifa, Maktaba ya Tibet, Maktaba ya Shanghai, Maktaba ya Jiangxi, Jumba la Makumbusho la Shanxi , Thieta ya Changan ya Beijing , yote hayo yamejengwa kwenye mazingira mazuri , na usimamizi wao unaendeshwa kwa njia ya kompyuta, majengo ambayo yametoa huduma nzuri kwa watu wote.
Hii ni Thieta kubwa ya Shanghai ambayo imejengwa tayari na kutumiwa rasmi. Jengo hili lenye eneo la mita elfu 62.8 lilipokea mtindo wa ujenzi wa thieta za kiulaya, umbo lake linapendeza watu, vifaa vya ndani na usimamizi wake pia umefikia kiwango cha kimaendeleo cha dunia. Jengo hilo limeongezea Shanghai mandhari nzuri .
Nchini China kuna mashirika mengi ya shughuli za utamduni yaliyoanzishwa na raia kwa hiari yao, mashirika hayo ni pamoja na mashirika ya opera za kienyeji, ya uchoraji wa picha, ya usomaji wa vitabu . Na pia kuna shughuli nyingi za kusherehekea sikukuu za kijadi za makabila mbalimbali, karibu kila siku kwa wastani wapo watu wanaosherehekea sikukuu yao katika sehemu moja.
Mwanzoni mwa miaka ya 80, China iliweka lengo la kuifanya kila wilaya iwe na Jumba la utamaduni na maktaba , na kila tarafa iwe na kituo cha utamaduni, ikawawezesha watu wajishirikishe shughuli za michezo.
Ili kuonyesha matokeo ya usanii wa jukwaani na kutoa michezo mizuri ya sanaa, kuaniza mwaka 1987, serikali kuu kila baada ya muda fulani huandaa tamasha ya sanaa ya China, tena kuwaalika wasanii wa nchi mbalimbali waje kushiriki tamasha hiyo, mpaka sasa tamasha hiyo imeshafanywa kwa mara 5. Na Serikali kuu pia imeweka utoaji tuzo la Wenhua la usanii wa jukwaani, tuzo la uchaishaji vitabu, tuzo la fasihi ya Maodun , tuzo la kiserikali la filamu na tuzo la kuwasifu watungaji au wasanii wasio rasmi kwa kazi yao, matuzo hayo yamehimiza maendeleo na usitawi wa utamaduni na sanaa za China.
Hivi sasa maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje yamefanywa kwa njia na aina nyingi mbalimbali, ambapo vikundi vya utamaduni na sanaa vya China na vya nje hutembeleana mara kwa mara , na watazamaji wa Chiina wameonyesha pia shauku kubwa juu ya utamaduni na sanaa za nchi za nje.
Katika miaka kadha iliyopita, mkururo wa tamasha kubwa za maingiliano ya utamaduni ya kimataifa zilifanyika nchini China, kama vile Muziki wa symphony wa kimataifa wa mwaka 1996,Opera na michezo ya ngoma ya kimatiafa ya mwaka 1997, Sanaa ya uchoraji ya kimataifa ya mwaka 1998, na Sanaa ya Asia ya mwaka 1998 zote zilishirikisha vikundi na wasanii wenye kiwango cha juu wa nchi za nje na kuwafanya watazamaji wa China wapanue upeo wao sana.
Utamaduni na sanaa za Chiina umekusanya na kuendeleza umaalmu mbalimbali wa utamaduni na sanaa za makabila 56 ya China, umeonyesha uvumbuzi wa watu wenye mawazo tofauti na mabuni mballimbali, utamaduni na sanaa hizo pia zimepokea ubora wa utamduni wa nchi mbalimbali na matunda ya ustaarabu wa binadamu .
Wakati karne mpya , utamaduni na sanaa za China zitapatana na utamaduni na sanaa za dunia nzima zenye kung'ara .
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-19
|