Wanawake wa nchi za Asia ya mashariki wanajulikana duniani kwa upole na mvuto. Hivi sasa, kutokana na kuongezeka kwa wanawake waliojishirikisha kwenye shughuli za kijamii, idadi ya wanawake wanaofanya kazi katika idara za sekta mbalimbali, hasa katika eneo la utoaji huduma imeongezeka siku hadi siku, ambao wakati wanapodumisha upole wao, pia wanafuatilia mwelekeo wa kisasa, na kuonesha sura zao za kupendeza.
Duka kubwa la Xinyansha la Jinyuan lililoko katika sehemu ya magharibi mwa Beijing, ni moja ya maduka makubwa kabisa duniani. Ndani yake kuna maduka zaidi ya 400 yanayouza bidhaa za chapa maarufu. Licha ya kuwa na maduka ya kuuzia bidhaa za aina mbalimbali, pia kuna mikahawa, vyumba vya burudani na kufanya mazoezi ya kujenga mwili. Wateja wengi wanafurahia kwenda kununua bidhaa huko sio tu kutokana na mazingira mazuri, bali pia kutokana na kwamba wauzaji wote wanavaa nguo za kisasa na kuwatendea wateja kwa uchangamfu. Meneja mkuu wa duka la Xinyinsha la Jinyuan Bi. Fu Yuehong alisema kuwa, zaidi ya nusu ya wauzaji au watumishi katika duka hilo ni wanawake, ambao hujulikana kwasura zao za kisasa na za kupendeza. Anasema:
"Nchini China, watu wengi wanaojishughulisha na mambo ya biashara na huduma ni wanawake, hali kadhalika, theluthi mbili ya wasimamizi wa ngazi ya juu na wastani wa duka letu ni wanawake, ambao wote ni hodari katika kazi zao, wanafuatilia sana kujifunza mambo mapya na kuonesha mwelekeo wa kisasa ."
Hivi sasa wafanyakazi wanawake wa China wanafuatilia sana mwelekeo wa kisasa. Kwa mfano, wanavaa mavazi ya kisasa kazini, kujipamba vizuri, kubadilisha mitindo ya nywele mara kwa mara, wengine huenda kwenye maduka ya kuremba kila baada ya muda fulani, na wengine hufanya mazoezi ya kujenga mwili kwenye klabu mbalimbali.
Wataalamu wameainisha kuwa, kufuatilia mwelekeo wa kisasa kunatokana na mahitaji ya wafanyakazi wanawake kufanikiwa katika zama mpya tulizo nazo. Mkurugenzi wa kituo cha maendeleo ya shughuli za wanawake na watoto cha China Bi. Zhang Qi alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema kuwa, hivi sasa wanawake walioajiriwa wanachukua asilimia 40 ya wafanyakazi wote nchini China, na wamekuwa nguvu kubwa katika kustawisha uchumi wa China. Kutokana na kuongezeka kwa ushindani wa kibiashara sokoni, kufuatilia mwelekeo wa kisasa kumekuwa mahitaji ya wafanyakazi wanawake kujiendeleza siku hadi siku. Anasema:
"Ufuatiliaji huo wa mwelekeo wa kisasa unatokana na mahitaji ya hali halisi. Kwa sababu wanawake hao hawakai nyumbani, wamejishirikisha katika shughuli za jamii, hivyo mwenendo wao, mvuto wao, na sura zao vyote vinahusiana moja kwa moja na kazi yao."
Kufuatilia mwelekeo wa kisasa huonesha katika namna ya kujipamba, namna ya kuchagua mavazi, namna ya kuongea na kutendea. Hayo yameonekana zaidi katika sura za wanawake walioajiriwa au wenye mapato makubwa.
Bi. Li Ying ambaye ni wakala wa mauzo ya magari aina ya BMW mjini Beijing, anajulikana sana kwa kuandana na fesheni, amesifiwa kuwa mwakilishi wa kufuatilia mwelekeo wa kisasa nchini China. Anasema:
Sauti
"Kwa kweli mwenendo wa mtu fulani huonesha hali ya maarifa na elimu aliyokuwa nayo. Hivyo kila siku ninapokutana na watu wa aina mbalimbali, huwa najitahadharisha kuwa lazima niwafurahishe wateja wangu kwa huduma bora."
Ingawa Bi. Li Ying ni mrembo, lakini kila siku anajipamba kabla ya kuondoka nyumbani, anavaa nguo tofauti kutokana na mazingira tofauti. Na jambo muhimu zaidi kwake ni kwamba, anafuatilia sana kujiendeleza kwa kujifunza mambo mapya yanayotokea kila siku.
Lakini baadhi ya wanawake wanaoajiriwa bado hawajui namna ya kufuatilia mwelekeo wa kisasa. Kuhusu jambo hilo, mhariri mkuu wa tovuti moja ya China Bi. Gao Lu alichambua kuwa, wanawake hao hawajui kwamba wameachwa nyuma labda kutokana na kuwa na kazi nyingi, au kuwa na kazi nyingi za nyumbani, au kamwe hawana ufahamu kuhusu jambo hilo.
Kwa ujumla, umati wa wanawake waliojiriwa nchini China bado wanahitaji kuelimika zaidi, si kama tu katika hali yao ya maarifa na elimu, bali pia sura zao katika shughuli za biashara. Ili kuwasaidia wanawake hao kuonesha uwezo wao wa kutosha, kuanzia mwaka jana, shirika moja la wanawake la China limeendesha shughuli za mashindano ya wafanyakazi wanawake wanaofuatilia mwelekeo wa kisasa, ili kuwahimiza wafanyakazi wanawake wengi zaidi kuonesha uwezo wao na kufuatilia maisha bora zaidi wakati wa kujiendeleza.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-25
|