Maonyesho ya nguo na mapambano ya makabila madogo dogo ya China yalionyesha seti 400 za nguo na mapambano zaidi ya 1,000 ya makabila 56 na yaliyoambatana na muziki na ngoma.
Maonyesho hayo yalidhihirisha vizuri nguo na mapambo mbalimbali ya makabila madogo dmadogo tofauti.
Nguo na mapambano ya Waoroqen, Wadaur, Wahezhe, Wakorea, Wamongolia na Wamanchu wanaoishi katika maeneo ya kaskazini-mashariki na Mongolia ya Ndani yanalenga kuzuia baridi. Waoroqen wamekuwa wakihamahama na kuwinda katika misitu ya ndani kizazi baada ya kizazi, si wanaume si wanawake wote wamebobea kupanda farasi na kupiga mishale, kwa hivyo ngozi za wanyama zimekuwa nyenzo nzuri katika kutengeneza nguo zao. Ngozi za kulungu waliokomaa ni madhubuti, nyepesi na laini, wanawake hushona kanzu, suruali na njuti kwa kano nyembamba za wanyama.
Watibeti huvaa kizibao, hii inahitilafiana na hali ya hewa ya baridi kwenye uwanda wa juu, halijoto baina ya mchana na usiku huko uwanda wa juu inatofautiana sana, mchana joto linakuwa hali na watu wanavaa nguo ya mkono mmoja wa kulia au mikono yote miwili, nguo ya mikono hiyo miwili ilifungiwa kiunoni ili kufanya kazi kwa urahisi zaidi. Baada ya miaka mingi kupita, mikono miwili ilikuwa ikizoea baridi na mtindo huo maalumu ukabadilika kuwa pambo. Aproni zinazovaliwa viunoni na wanawake wanaokuwa malishoni huko Tibet, mwanzoni zilitengenezwa kwa sababu ya kazi.
Hali ya hewa ya mikoa ya kusini mwa China ni joto na unyevunyevu, kwa hiyo nguo za makabila ya huko ni nyepesi lakini zina tofauti, k.v. wasichana Wadai wa Xishuangbanna, mkoa wa Yunnan, huvaa blauzi fupi zinazobana na sketi ndefu mpaka miguuni, nywele huchanwa na kufungwa visogoni au kuvaa ushungi wenye mabombwe. Aina za nguo na mapambo ya Wamiao ni namna kwa namna. Seti moja ya nguo mavazi ya bibi harusi hutumia kwa miaka kadha. Kila sikukuu wasichana huvaa shanga, bangili na maua ya fedha, baadhi ya nguo zinawekwa nakshi za fedha zenye uzito wa kilo zaidi ya 10, na mapambo mengine ya fedha hung'aa na kuvutia sana watu.
Inasemekana kwamba wasichana Wajingpo walitengeneza sketi ya mche-duara ya kwanza yenye mabombwe kwa manyonya ya ndege. Utarizi wa mraba wa nyuma ya mabega ya Wamiao unaonyesha maskani ya Wamiao ili vizazi vyao visisahau historia ya kabila lao na mafanikio ya mababu zao.
Nguo na mapambo hubadilika kwa kufuata mabadiliko ya maisha. Maendeleo ya ustaarabu wa kisasa yanazifanya nguo na mapambo ya kizazi cha vijana viendelee kwenye mwelekeo wa kimji, wakati huo huo uelewa na utafiti wa nguo na mapambo ya kijadi umekuwa wa aina zaidi, uzuri wa nguo na mapambo ya kikabila umevutia na kuchukuliwa zaidi. Nguo na mapambo ya kizamani yanaendelea kuwa na umaarufu mkubwa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-08-26
|