Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-26 20:28:08    
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Hong Kong wanaojitolea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa China bara

cri

Kikundi cha kwanza cha wanafunzi 10 wa vyuo vikuu wa Hong Kong wanaotekeleza "mpango wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa Hong Kong wanaojitolea kutoa mafunzo katika China bara" wataishi maisha yenye taabu kwenye sehemu maskini ya China bara, kama vile kwenda mbali kuteka maji ya kunywa, kutoweza kuoga kwa maji ya moto, na kulala kwenye vitanda vyenye kunguni na vyura.

Tarehe 24 wanafunzi hao walikwenda chuo kikuu cha umma wa China na kufanya maandalizi yao ya mwisho kabla ya kwenda kwenye sehemu maskini ya China bara, kupata uzoefu kutoka kwa kikundi cha wanafunzi wa chuo kikuu hicho waliojitolea kutoa mafunzo kwa miaka 7 iliyopita na kusikiliza jinsi walivyofanya kazi huko.

Wanafunzi hao wa Hong Kong wanashiriki kwa mara ya kwanza kwenye harakati za wanafunzi wa vyuo vikuu wa China wanaojitolea kuwafundisha watoto wa sehemu maskini zinazoandaliwa na China bara, ambao wanatoka katika chuo kikuu cha Hong Kong, chuo kikuu cha lugha ya Kichina cha Hong Kong na chuo kikuu cha Jinhui cha Hong kong. Mbali na watu watatu ambao ni wafanyakazi, wengine wote ni wanafunzi waliohitimu kutoka katika vyuo vikuu hivyo.

Alasiri ya tarehe 25, wanafunzi hao watafunga safari kwenda sehemu maskini milimani ya wilaya inayojiendesha ya makabila ya Watujia na Wamiao, magharibi ya mkoa wa Hunan na kuanza maisha ya kuwafundisha watoto kwa mwaka mmoja kwa masomo ya muziki, hisabati, fizikia, lugha ya Kichina na lugha ya Kiingereza kwenye shule tatu za sekondari.

Namna ya kuwafundisha wanafunzi watukutu na mambo gani yafuatiliwe wakati wa kutembelea familia za wanafunzi, namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoacha masomo kutokana na matatizo ya nyumbani na kuwapangia shughuli baada ya masomo, ili kuwawezesha watoto wawe na imani na kuungana zaidi, masuala hayo yote yamefuatiliwa na wanafunzi hao wanaojitolea.

Mwanafunzi Bi. Tan Huixin aliyehitimu kutoka katika idara ya lugha ya Kichina ya chuo kikuu cha Jinhui cha Hongkong alisema kuwa, ingawa amekuwa na shahada ya elimu, lakini hii haitoshi, kwani mfumo wa elimu ya China bara ni tofauti na ule wa Hongkong, kufundisha masomo katika sehemu mbali ya China bara ni changamoto kubwa kwake. Kuhusu kufundisha kwa matamshi ya kawaida ya Kichina, wanafunzi hao wanaojitolea wamepitishwa mtihani, kwa hiyo hamna tatizo.

Mwanafunzi mmoja wa kikundi cha kutoa mafunzo cha chuo kikuu cha umma wa China Bw. Li Peng alitoa hotuba kuhusu namna ya kuwasaidia wanafunzi wa sehemu hiyo waache ushabiki wa michezo ya mtandao na kuwaoneshea filamu. Mwanafunzi wa chuo kikuu cha lugha ya Kichina cha Hongkong Bi. Pan Jiaqi alieleza kuwa ana mpango wa kupiga muziki pamoja na watoto na kuwapatia furaha, ili awasiliane vyema na watoto hao.

Ingawa maisha yanayosimuliwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha umma wa China ni magumu, lakini wanafunzi wanaojitolea wanasema kuwa wanataka kubadilisha maisha ya watoto wa milimani kwa jitihada zao.

Idhaa ya Kiswahili 2005-08-26