Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-01 20:33:17    
Eneo la ardhi, Bendera ya Taifa, Nembo la Taifa, Wimbo la Taifa na Mji Mkuu

cri

Eneo la ardhi

Jamhuri ya Watu wa China yaani China, iko kwenye sehemu ya mashariki ya Bara la Asia na kando ya magharibi ya Bahari ya Pasifiki. Eneo la nchi kavu la China ni karibu kilomita za mraba milioni 9.6, ambayo ni nchi yenye eneo kubwa zaidi kwenye Bara la Asia, na ni nchi kubwa ya tatu duniani ikizifuata Russia na Canada.

Toka kaskazini hadi kusini, ardhi ya China inaanzia kwenye chanzo cha Mto Heilongjiang, kaskazini ya Mto Mo (digri 53.30 ya latitudo ya kaskazini) mpaka Zengmu Ansha ya ncha ya kusini ya Visiwa vya Nasha (digrii 4 ya latitude ya kaskazini), umbali kati ya kusini na kaskazini ni kilomita 5500; toka mashariki hadi magharibi, ardhi ya China inaanzia sehemu ya makutano kati ya Mto Heilong na Mto Usuri (digrii 135.05 ya longitudo ya mashariki), mpaka Uwanda wa juu wa Pamier (digri ya 73.40 ya longitude), umbali kati ya mashariki na magharibi ni kilomita 5000.

Mpaka wa nchi kavu ya China una urefu wa kilomita 22,800, upande wa mashariki, China inapakana na Korea ya kaskazini, upande wa kaskazini inapakana na Mongolia, upande wa mashariki inapakana na Russia, upande wa kaskazini magharibi inapakana na Kazakstan, Kyrgyzstan na Tajikstan, upande wa magharibi na wa kusini magharibi inapakana na Afgahnistan, Pakistan, India, Nepal, na Buthan, upande wa kusini inapakana na Myanmar, Laos na Vietnam. Na upande wa mashariki na wa kusini mashariki China inakabiliana kwa bahari na Korea ya kusini, Japan, Philipines, Burnei, Malaysia na Indonesia.

Bendera ya Taifa, Nembo la Taifa, Wimbo la Taifa na Mji Mkuu

Bendera ya Taifa: Bendera ya Taifa la Jamhuri ya Watu wa China ni Bendera nyekundu yenye nyota tano za manjano, kiasi cha ulinganifu kati ya urefu na kimo cha bedera hiyo ni 3:2. Bendera ya Taifa ina rangi nyekundu ambayo inamaanisha mapinduzi. Nyota 5 zenye pembe 5 kwenye bendera hiyo ni za rangi ya manjano, na kila ncha ya nyota 4 ndogo zenye pembe 5 inaielekea katikakati ya nyota kubwa, ambayo inaonesha mshikamano mkubwa wa wananchi chini ya uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China.

Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Watu wa China: Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Watu wa China inaonesha Bendera ya Taifa, Uwanja wa Tian An Men, gurudumu lenye meno na mashuke ya ngano na mpunga, ambayo inamaanisha mapambano ya mapinduzi ya demokrasia mpya yaliyofanyika tokea harakati za "tarehe 4 Mei" mwaka 1919 na wananchi wa China pamoja na kuzaliwa kwa China mpya yenye utawala wa kidemokrkasi wa uumma chini ya uongozi wa tabaka la wafayakazi na kwenye msingi wa shirikisho la wafanyakazi na wakulima.

Wimbo wa Taifa: Wimbo wa Taifa wa Jamhuri ya Watu wa China ni wimbo wa "Songa mbele watu mliojitolea", ambao ulitungwa mwaka 1935, mtungaji wa maneno ya wimbo huu ni mwandishi maarufu wa tamthiria Bwana Tian Han, muziki wa wimbo huu ulitungwa na Bwana Nie Er ambaye alikuwa mwanzilishi wa harakati za muziki mpya wa China. Wimbo huo ulikuwa wimbo wa kauli mbiu ya filamu ya "Vijana waliokumbwa na mashambulizi". Filamu hiyo ilieleza kuwa baada ya tukio la "Tarehe 18 Septemba" mwaka 1931, Japan iliposhambulia na kuikalia mikoa mitatu ya kaskazini mashariki ya China, taifa la China lilikuwa katika kipindi cha kufa na kupona, ambapo baadhi ya vijana walijitoa kutoka kwenye hali ya uchungu na mahangaiko wakaenda kwenye medani ya vita kupambana na mashambulizi ya Japan. Kutokana na filamu hiyo, wimbo huu uliimbwa na wachina wa kila sehemu nchini China, ukasifiwa kuwa mbiu wa kutoa mwito wa kujipatia ukombozi wa taifa la China.

Tarehe 27 Septemba mwaka 1949, mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China ulipitisha azimio kuwa kabla ya kutungwa rasmi kwa wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Watu wa China, wimbo wa "Songa mbele watu mliojitolea" uwe wimbo wa taifa. Tarehe 14 Machi, mwaka 2004, Mkutano wa pili wa Halmashauri ya kudumu ya 10 ya Bunge la umma la China ulipitisha mswada wa marekebisho ya katiba ukaamua kuwa wimbo wa Taifa wa Jamhuri ya Watu wa China ni wimbo wa "Songa mbele watu mliojitolea ".

Mji Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China: Mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China ni Beijing.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-01