Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-07 14:20:31    
Chuo kikuu cha Nankai chaanzisha mfumo wa pande zote wa kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi

cri

Tarehe 3 mwezi Septemba ilikuwa siku ya kwanza ya kuandikisha wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha Nankai cha Tianjing, China. Siku hiyo, mwanafunzi mmoja na wazazi wake kutoka mkoa wa Gansu walipokea msaada wa kiuchumi na vitabu vya " Jinsi ya kusoma katika chuo kikuu", " Wanafunzi wa Nankai " na vitabu vingine pamoja na CD Rom kutoka kwa chuo hicho. Wazazi wa mwanfunzi huyo walitiwa moyo sana wakisema kuwa, hawakudhani kama chuo kikuu kinawasaidia wanafunzi ipasavyo namna hii.

Katika miaka ya hivi karibuni, hakuna mwanafunzi hata mmoja kutoka familia zenye matatizo ya kiuchumi ambaye alisimamisha masomo kutokana na matatizo ya kiuchumi. Katibu wa kamati ya chama ya chuo kikuu cha Nankai cha Tainjing, China Bw. Xue Jinwen alisema kuwa, kuwawezesha wanafunzi wote wapate elimu ya juu ni wajibu wa vyuo vikuu vya ujamaa.

Kutokana na uzoefu wa zamani na matokeo ya utafiti, Chuo kikuu cha Nankai kimetambua kuwa, ingawa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi wanaweza kujiandikisha kwenye vyuo vikuu kwa " njia isiyowekwa vikwazo", lakini baada ya muda mfupi, kutokana na kutojua hali na sera husika za chuo kikuu, baadhi ya wanafunzi watakumbwa na matatizo ya maisha, na wanafunzi wengi wenye matatizo ya kiuchumi watashindwa kuvumilia maisha ya chuoni.

Kutokana na hali hiyo, mbali na kuendelea kuanzisha " njia isiyowekwa vikwazo" , wakati wa kuwapa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi " kadi ya msaada", chuo kikuu cha Nankai pia kilitoa huduma nyingine nyingi ili kuwasaidia wanafunzi hao kuondokana na matatizo mbalimbali ya maisha kutokana na matatizo ya kiuchumi.

Wakati huo huo, chuo kikuu cha Nankai kinatoa huduma ya kisaikolojia kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi, mbali na hayo idara husika pia zinatoa msaada kwa wanafunzi hao kwa muda mrefu.

Hivi sasa chuo kikuu cha Nankai cha Tianjing, China kilichukua hatua za mfulilizo ili kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi kwa hatua zaidi. Hatua hizo ni pamoja na kutoa mikopo ya masomo, kutoa masaada wa masomo, kutoa fursa ya kufanya kazi, na kuwasamehe kulipa ada.

Takwimu zinaonesha kuwa, katika chuo kikuu cha Nankai idadi ya wanafunzi waliopewa mikopo ya masomo ya serikali ya China imefikia 2796 kutoka 25 mwaka 1999 ambao wanachukua asilimia 13.2 ya wanafunzi wote wa chuo hicho. Mikopo ya kulipa gharama za masomo imefikia yuan milioni 16 kutoka laki 4. Habari zinasema kuwa, wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi wakikidhi matakwa ya chuo kikuu na benki, wote wanaweza kupewa mikopo ya masomo.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-07