Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-21 16:47:13    
Kutazama michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi

cri
Hivi sasa mchezo mfululizo wa televisheni AHADI unaoneshwa kwenye baadhi ya simu za mkononi nchini China. Simu ya mkononi imekuwa chombo muhimu katika maisha ya kila siku, inaweza kufanya kazi nyingi, kama vile, kupiga simu, kutuma ujumbe, kupiga picha na kuhifadhi namba za simu. Kutokana na maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia, hivi sasa simu za mkononi hapa China zinaweza kufanya kazi nyingine, yaani kuonesha mchezo wa televisheni. Mchezo huo mfululizo AHIDI, ndio unaooneshwa kwenye simu za mkononi, muda wake wa ujumla ni dakika 25, na una sehemu 5, na muda wa kila sehemu ni dakika 5.

Utengenezaji wa mchezo huo AHADI unafadhiliwa na kampuni ya Leshi ya Beijing ambayo inashughulikia utengenezaji wa vipindi vya televisheni vinavyooneshwa kwenye simu za mkononi. Meneja wa kampuni hiyo Bw. Liuhong alifahamisha akisema:

"Baada ya kufikiria kwa makini hali halisi ya watumiaji wa simu za mkononi, tulithibitisha muda wa kila sehemu ya vipindi hivyo kuwa dakika 5. Kutokana na simu za mkononi kuwa na kioo kidogo, kama watu wakiangalia kwenye kioo hicho kwa muda mrefu, macho yao yatachoka, hivyo dakika 5 ni muda mwafaka.

Bi. Yangshan ni mfanyakazi wa shirika moja lililowekezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje hapa Beijing, ametazama mchezo wa AHADI kwenye simu yake ya mkononi, alisema kuwa vikilinganishwa na michezo ya kawaida ya televisheni, muda wa mchezo huo ni mfupi, lakini hadithi yake ni rahisi kuelewa, picha zake ni nzuri na wahusika wa mchezo huo wanavutia, anapenda mchezo huo. Pia alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

"Naona kuwa jambo muhimu la huduma hiyo ya michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi ni kuwawezesha watu kutazama mchezo kama huo wakati wanaposubiri basi au ndege, ili waweze kutumia wakati vizuri zaidi."

Katika nchi kama Marekani, Japan, Korea ya Kusini na baaadhi ya nchi za Ulaya, kutazama michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi lilikuwa jambo la kawaida tangu zamani, na limekuwa sehemu yao ya maisha. Katika nchi hizo, kwenye ukumbi wa kusubiria ndege au mikahawa, ni kwaida kuwaona baadhi ya watu wakitazama michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi, njia hiyo ya kupumzika inaweza kutumia vizuri wakati wa mapumziko, hivyo inapendwa na watu siku hadi siku.

Nchini China, watu walianza kutazama michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi tangu mwishoni mwa mwaka jana, sababu ya kuchelewa kwa China katika kutumia teknolojia hiyo ni kuwa, kasi ya usafirishaji wa mfumo wa mawasiliano ya China ni ndogo, ilipofika mwishoni mwa mwaka jana, kasi yake iliweza kukidhi mahitaji yanayotakiwa na michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi. Mbali na hayo, bei ya simu za mkononi zinazoweza kuonesha michezo ya televisheni ni za bei kubwa, kwa kawaida bei yake ni zaidi ya yuan za renminbi elfu 5, hali hiyo pia inaathiri maendeleo ya huduma ya michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi.

Hivi sasa, kutazama michezo ya televisheni kwenye simu za mkononi bado siyo jambo la kawaida, watu wanaoagiza huduma hiyo nchini China hasa ni vijana wa miji mikubwa, ikiwemo Beijing, Shanghai na Guangzhou. Zaidi ya michezo mfululizo, wanaweza kutazama taarifa ya habari, utabiri wa hali ya hewa na vipindi vya muziki wa televisheni kwenye simu za mkononi, vipindi hivyo mbalimbali vinatolewa na mashirika yanayoshughulikia huduma hiyo na utengenezaji wa vipindi vya televisheni, baadhi ya vipindi ni kwa ajili ya simu za mokononi tu, na vingine vinachaguliwa na kuhaririwa kutoka kwenye vipindi vya televisheni vya kawaida.

Bi. Xiaoli anapenda sana kutazama vipindi vya muziki wa televisheni kwenye simu za mkononi, alisema:

"Kama nikitaka kutazama muziki fulani wa televisheni kwenye simu ya mkononi, naweza kutembelea tovuti ya MTV na kuchagua muziki ninaoutaka, na kuuhifadhi kwenye simu yangu ya mkononi."

Bi. Xiao pia alisema kuwa ingawa hali ya muziki wa televisheni unaooneshwa kwenye simu ya mkononi hauonekani vizuri kama unavyoonekana kwenye televisheni na kompyuta, lakini kwa sababu watu huenda mahala popote pamoja na simu zao za mkononi, hivyo wanaweza kutazama MTV wakati wowote kwenye simu zao za mkononi, kwa watu kama yeye, yaani watu wanaopenda muziki, huduma hiyo ni muhimu kwao.

Imefahamika kuwa kadiri teknolojia mpya kabisa ya mawasiliano itakavyotumika hapa China, ndivyo kasi ya usafirishaji wa mfumo wa mawasiliano itakavyoongezeka kwa kiasi kikubwa, na hali ya vipindi vya televisheni kwenye simu za mkononi itaboreshwa kidhahiri, na hali hiyo itasukuma mbele maendeleo ya huduma hiyo nchini China.

Aidha, wataalamu wanasema kuwa, katika siku zijazo bei ya simu za mkononi haitakuwa kikwazo kwa maendeleo ya huduma ya vipindi vya televisheni kwenye simu za mkononi, meneja Liuhong alichambua akisema:

"Wachina wanabadilisha simu za mkononi mara kwa mara na kuacha simu zao za zamani. Miaka miwili iliyopita, simu za mkononi zenye vioo vya rangi siyo rahisi kupatikana nchini China na bei yake ilikuwa ni kubwa, lakini hivi sasa, simu za mkononi za namna hiyo, hata zenye kamera, bei zao zimeshuka hadi yuan za renminbi elfu 2. Hivyo naamini kuwa simu za mkononi katika siku zijazo zote zinaweza kuonesha vipindi vya televisheni, na bei zake zitashuka kwa kiasi kikubwa. Katika siku chache zijazo, kutazama vipindi mbalimbali kwenye simu za mokononi litakuwa jambo la kawaida."

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-21