Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-03 20:27:35    
Maelezo kuhusu taratibu za forodha

cri

Kwa kawaida, msafiri anapopita kwenye forodha, mizigo yote aliyokuwa nayo inatakiwa kukaguliwa. Mizigo ambayo haijakubaliwa na forodha haichukuliwi au kusafirishwa.

Mizigo yake iliyosafirishwa, ambayo haikuwa pamoja na msafiri inatakiwa kutolewa maelezo katika "fomu ya mizigo ya msafiri", na inatakiwa kuingia au kutoka nchini katika muda wa miezi 6 baada ya msafiri kuingia au kutoka China.

"Fomu ya mizigo ya msafiri" iliyosainiwa na mfanyakazi wa forodha inatakiwa kutunzwa vizuri ili ashughulikiwe haraka wakati atakapoondoka au kuingia nchini.

Aidha, msafiri anapaswa kutoa maelezo kwa forodha wakati anapoondoka China akichukua vitu vya mabaki ya kiutamaduni. Vitu vya mabaki ya kiutamaduni alivyonunua msafiri katika maduka yenye leseni ya biashara ya mabaki ya kiutamaduni, forodha inamruhusu kuondoka baada ya kukagua risiti maalumu za biashara hiyo yenye muhuri wa idara ya usimamizi wa mabaki ya kiutamaduni ya China. Msafiri akitaka kuondoka nchini na kuchukua vitu vya mabaki ya kiutamaduni ambavyo alivipata kwa njia nyingine vikiwa ni pamoja na kurithi kutoka wazazi au kupewa zawadi na marafiki, anapaswa kuthibitishwa na idara ya usimamizi wa vitu vya mabaki ya kiutamaduni ya China. Hivi sasa, idara hiyo imefungua ofisi zake katika forodha za miji minane ikiwemo ya Beijing, Shanghai, Tianjin na Guangzhou. Vitu vinavyoruhusiwa kuchukuliwa katika nchi za nje baada ya kuthibitishwa na kupewa kibali na idara ya usimamizi wa mabaki ya vitu vya kiutamaduni vinakubaliwa kupita kwenye forodha ya China.

MAELEZO KUHUSU KARANTINI

Idara ya karantini ya China ni idara ya utekelezaji wa sheria iliyoanzishwa kutokana na agizo la serikali kuhusu shughuli za karantini zinaohusika na nchi za nje, idara hiyo na vitengo vilivyo chini yake katika forodha zilizofunguliwa mlango kwa nchi za nje kufanya ukaguzi wa karantini kwa mujibu wa sheria juu ya watu wanaoingia na kutoka nchini, na forodha zinatoa ruhusa ya kuingia au baada ya kuona vyeti vilivyosainiwa na vitengo vya karantini.

Vyombo vya mawasiliano, watu, chakula, maji ya kunywa pamoja na wadudu na maradhi ya kuambukiza vinafuatiliwa zaidi.

Vitengo vya karantini vinawazuia wageni wenye baadhi ya magonjwa kuingia nchini, ambao ni pamoja na wenye virusi vya ukimwi, magonjwa ya zinaa ya kuambukiza na kifua kikuu kilichoko katika kipindi cha kuambukiza.