Raslimali ya ajabu ya maji kwenye jangwa la Badanjilin imewavutia wanasanyasi wengi zaidi wa nchi mbalimbali kwenda huko kufanya utafiti. Mwishoni mwa mwezi Septemba, kikundi kimoja cha utafiti wa kisayansi ambacho kinaundwa na wanasanyasi na watu wanaojitolea 25 kutoka China, Marekani, Japan, Canada, Ujerumani na Uswisi kilikwenda kwenye jangwa hilo na kutafiti tena raslimali nyingi za maji.
Jangwa la Badanjilin lililoko kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani ni jangwa la nne kwa ukubwa duniani. Kutokana na kuwepo kwa maziwa mengi kwenye eneo la jangwa hilo, asilimia 80 ya matuta ya mchango unaweza kutoa sauti ukipulizwa na upepo, na matuta mengi ya mchanga unaoweza yapo kwenye yanasambaa kwenye eneo kubwa.
Kwa kawaida kwenye eneo la jangwa lenye mvua kidogo, matuta ya mchanga yanahamishwa kutokana na nguvu ya upepo, lakini matuta hayo kwenye jangwa la Badanjilin hayahami. Wataalamu wanaona kuwa, hali hiyo inatokana na kuwepo kwa raslimali nyingi ya maji chini ya ardhi, na maji yanafanya mchanga ushikamane. Lengo moja la uchunguzi kwenye jangwa hilo ni kufichua siri ya raslimali ya maji kwenye jangwa hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni, kila mwaka vikundi viwili au vitatu vya utafiti wa kisayansi vinakwenda kwenye jangwa hilo, hivi sasa kwa ujumla wataalamu zaidi ya 300 kutoka nchi 16 walifika huko kutafuta chanzo hicho cha maji. Watafiti wamegundua maziwa 144 kwenye eneo la mbali la jangwa hilo, na eneo la jumla la maziwa hayo linazidi kilomita za mraba 23. kati ya hayo, maziwa 72 yana maji kwa mwaka nzima, na maziwa 12 yana maji baridi yenye sifa nzuri. Ziwa kubwa kabisa lina eneo la kilomita za mraba 1.5 na kina cha mita 16.
Watafiti wa safari hii ni pamoja na wataalamu wa mambo ya maji na wa mazingira, amabao wote wanatoka chuo kikuu cha Monique na taasisi ya utafiti ya taifa ya Ujerumani. Kikundi hicho cha uchunguzi kilisafiri kwa kilimita 80 kutoka ziwa la Badan hadi kufikia Danuoritu. Wataalamu walichukua sampuli nyingi za maji ya maziwa yaliyoko mbali ndani ya jangwa, na kutaka kugundua chanzo cha maji hayo kwa kuchunguza sampuli hizo. Kikundi hicho pia kiligundua mashimo ya chemchem ya maji baridi yaliyoko katikati ya baadhi ya maziwa ya maji ya chumvi. Uchunguzi wa masalio karibu na mashimo hayo unaonesha kuwa mtiririko wa chemchem hizo umekuwepo kwa karne kumi kadhaa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-12
|