Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-13 20:19:20    
Mradi wa kupunguza maafa ya tetemeko la ardhi waletea maisha mazuri kwa watu wa makabila mbalimbali wa Xinjiang

cri

Mkoa unaojiendelesha wa Xinjiang Uyghur uko Kaskazini-Magharibi mwa China ambako tetemeko la ardhi hutokea mara kwa mara. Mwaka 2003 matetemeko ya ardhi yenye nguvu ya 4 kwenye kipimo cha Richter yalitokea mara 61, na matetemeko ya ardhi yenye nguvu ya 6 na zaidi yalitokea mara 2. mwezi Februali mwaka 2003 tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.8 kwenye kipimo cha Richter lilitokea Kash, Kusini mwa Xinjiang, nyumba nyingi zilibomboka, na kusababisha vifo na majerahi ya watu wengi. Ili kuboresha mazingira ya makazi yaliyoko kwenye sehemu inayokumbwa na tetemeko la ardhi na kupunguza maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi, tangu mwanzoni mwa mwaka uliopita, mkoa wa Xinjiang ulianza kuanzisha mradi wa kujenga makazi mapya ili kupunguza maafa ya tetemeko la ardhi. Sasa tunawaletea maelezo kuhusu ujenzi wa makazi hayo mapya.

Mwezi Septemba ni wakati wa kusherehekea mavuno. Kutokana na uzalishaji mzuri wa mwaka huu, mapato ya wakulima yaliongezeka kuliko mwaka uliopita. Yakbu Rexiti anayetoka wilaya ya Jiashi sehemu ya Kash, Xinjiang, alipanga kununua samani mpya kwa ajili ya nyumba yake mpya, alifurahi akimwambia mwandishi wa habari kuwa, nyumba yake ilijengwa na serikali, anasema:

" nyumba hiyo ambayo ilijengwa na serikali inaweza kukabiliana na maafa ya tetemeko la ardhi, mimi sikutoa pesa yoyotena wala sikufanya kazi. Familia yangu ina watu watatu, zamani nilikuwa na nyumba moja tu ambayo ni ndogo, lakini sasa eneo la nyumba yangu linafikia mita 50 za mraba, tunaishi vizuru sana."

Yakbu mwenye umri wa miaka 38 alimwambia mwandishi wa habari kuwa, tangu mwezi Februali mwaka uliopita, mkoa wa Xinjiang ulianza kutekeleza mradi wa kujenga upya makazi ya kukabiliana na tetemeko la ardhi. Alisema kuwa, baada ya kuishi katika nyumba mpya, maoni yake kubwa ni kuwa, usiku anaweza kulala salama, kwa sababu nyumba mpya imara, ina uwezo mkubwa wa kupunguza madhara ya tetemeko la ardhi, kwa hiyo haogopi kutokea kwa tetemeko la ardhi. Zamani nyumba ya Yakbu ilijengwa kwa udongo, kwa kuwa nyumba yake haikuwa salama, alipaswa kuifanyia ukarabati kwa pesa nyingi kila mwaka. Tatizo hili lilikuwa mzigo mkubwa kwake. Miaka miwili iliyopita, tetemeko la ardhi lilitokea tena, nyumba ya Yakbu ilibomoka. Hivi sasa, Yakbu na familia yake wanaishi kwenye nyumba mpya. Alimambia mwandishi wa habari kwa furaha kuwa, mbali na kuwa na mashamba, pia anafanya kazi nyingine na kuwasaidia watu wengine kujenga nyumba zenye uwezo wa kupunguza maafa ya tetemekeo la ardhi. Mapato ya familia yake ya mwaka huu yameongezeka kwa Yuan 2000 kuliko mwaka uliopita.

Kwenye mahojiano mwandishi wa habari aliambiwa kuwa, hivi sasa wakulima wote wa kijiji cha Adila wameacha kuishi kwenye nyumba za zamani na sasa wanaishi kwenye nyumba mpya. Mkurugenzi wa kijiji hicho Abudu Klimu Turfu alisema:

" matetemeko ya ardhi hutokea katika sehemu hiyo mara kwa mara, na nyumba za wakulima zinabomoka mara kwa mara. Kutoakana na misaada ya serikali na jamii, wakulima wamejenga nyumba za kupunguza madhara ya tetemeko la ardhi. Hivi sasa, hatuna wasiwasi, uchumi wa sehemu hiyo ulianza kuednelea kwa haraka."

Mzee Azihan Mukela mwenye umri wa miaka 75 ambaye hana familia yoyote pia amehamia kwenye nyumba mpya. Anasema:

" miaka mitatu iliyopita, nyumba yangu ilibomoka kutokana na tetemeko la ardhi, baada ya hapo, serikali ilianzisha kituo cha kuwatunza wazee, tunaishi hapa. Huduma tunazopata ni nzuri, chakula kizuri, wafanyakazi wanatutunza vizuri sana."

Mzee Azihan Mulake alisema kuwa, kuna wazee wengine 40 wanaoishi katika kituo kicho. Wafanyakazi 10 wanatoa huduma nzuri na wanafanya upimaji wa afya kwa wakati.

kwenye mahojiano aliyofanya kwenye wilaya ya Jiashi, mwandishi wetu aliambiwa kuwa, mbali na makazi yaliyofanywa ukarabati, kuna nyumbani nyingi mpya ambazo zimejengwa katika siku za karibuni zinavutia sana. Mkurugenzi wa wilaya ya Jiashi Bw. Zhang Hongwen anajulisha:

" zamani nyumba zetu zilikuwa hazipo katika eneo moja hivyo, watu walikumbwa na matatizo makubwa ya umeme, maji na mawasiliano. Kutokana na hali hiyo, tulijenga makazi mapya na kujikusanya, hivyo tuliweza kuokoa pesa nyingi. Sasa masuala ya maisha kama vile umeme, maji, barabara, simu na vipindi vya televisheni yametatuliwa kwa mafanikio."

Bw. Zhang Hongwen alisema kuwa, kutokana na mpango uliowekwa, wilaya ya Jiashi itajenga makazi mapya zaidi ya mia sita, hivi sasa makazi 130 yamekamilishwa au yanajengwa.

Mwenyekiti wa mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur Simayi Tieliwaer alimwambia mwandishi wa habari kuwa, serikali kuu ya China na serikali ya Xinjiang zilitoa Yuan bilioni moja katika ujenzi wa makazi mapya. Anasema:

" mwaka uliopita, serikali ilitoa Yuan milioni 160 katika mradi huo, mwaka huu mitaji itafikia Yuan milioni 300, tuliamua kuwa, katika miaka 5 ijayo, tutaondoa kikamilifu tatizo la makazi mkoani Xinjiang."

Habari zinasema kuwa, mradi wa kujenga makazi mapya ili kupunguza maafa ya tetemeko la ardhi utakamilika mwaka 2008, wakati huo familia milioni moja zitanufaika kutokana na mradi huo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-13