Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Zimbabwe umekuwa ukiimarishwa siku hadi siku, na Zimbabwe imekuwa ikiagiza bidhaa nyingi kutoka China.
Nchini Zimbabwe, vitu vilivyotengenezwa nchini China vinaonekana sehemu mbalimbali: Mapaa yenye vigae vya kichina vyenye rangi ya kibuluu ya Ikulu iliyokarabatiwa upya; ndege za kivita zinazotumiwa na jeshi la anga la Zimbabwe katika kufanya mazoezi; ndege za jeti zinazowabeba maofisa kutembelea nchini, pamoja na viatu na mabasi barabarani. Aidha, Rais Robert Mugabe anawahimiza wazimbabwe wajifunze kichina, na kujaribu mbinu za kupika chakula cha kichina.
Habari zinasema kuwa, uhusiano mwema kati ya China na Zimbabwe si kama tu unaonekana kwenye maisha ya kawaida. Hazina ya Platinamu nchini Zimbabwe inachukua nafasi ya pili duniani, na serikali ya Zimbabwe inataka kushirikiana na serikali ya China katika kuchimba madini.
Tangu Zimbabwe ipate uhuru mwaka 1980, uhusiano wa kibalozi kati ya China na Zimbabwe umekuwa ukiendelea vizuri. Mwaka 2002, Zimbabwe iliondolewa kutoka kwenye Jumuiya ya Madola kutokana na shinikizo la nchi za magharibi, hali ambayo ilimfanya Rais Mugabe wa Zimbabwe kuzisogelea na nchi za Asia, na kutafuta misaada kutoka kwa nchi za Asia wakati matatizo ya kiuchumi yalipotokea nchini humo.
Rais Mugabe anaechukulia sera hiyo kuwa ni sera ya "kutazama mashariki", ili kuondoa vikwazo vilivyowekwa na Uingereza na Marekani dhidi yake. Katika miaka miwili hadi mitatu iliyopita, hali ya uchumi nchini Zimbabwe imekuwa mbaya, kutokana na hali hiyo, China imekuwa nchi iliyowekeza vitega uchumi vingi nchini Zimbabwe.
Kati ya misaada mbalimbali inayotolewa na China, mingi ni kwa ajili ya kuonesha urafiki na Zimbabwe, kwa mfano Rais Robert Mugabe alijenga Ikulu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 13 kwenye kitongoji cha Harare, na mapaa ya ikulu hiyo yana vigae vya kichina wa rangi ya kibuluu yaliyotolewa kama zawadi na China.
Mbali na hayo, vitega uchumi vingine vya China vinazinufaisha nchi zote mbili. Kwa mfano, kampuni ya China ilipata mkataba wa mradi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni mia kadhaa, kujenga kituo cha utoaji wa umeme kwa nguvu ya maji nchini Zimbabwe. Kampuni ya usafiri wa anga ya juu ya China iliiuzia au kuizawadia Zimbabwe ndege 3 za jeti. Kiwanda cha kwanza cha magari ya China kimekubali kuiuzia serikali ya Zimbabwe mabasi 1000. Mwaka jana, China ilipata mkataba wa kuendesha shamba lenye kilomita za mraba 1000 nchini Zimbabwe. Aidha, jeshi la anga la Zimbabwe lilinunua ndege za mafunzo zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 200 kutoka China.
Serikali ya Zimbabwe inasema kuwa, katika miezi mitatu ya mwanzo mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara kati ya Zimbabwe na China imefikia dola za kimarekani milioni 100. Mtaalamu wa Zimbabwe kutoka Kituo cha utafiti wa usalama cha Pretoria Afrika ya Kusini Bw. Maron alidokeza kuwa, njia muhimu ya biashara kati ya China na Zimbabwe ni kubadilishana vitu kwa vitu. Kwa mfano, Zimbabwe iliwahi kupata mashine kutoka China kwa kutumia tumbaku inayolimwa nchini Zimbabwe.
Licha ya Zimbabwe, China vilevile imewekeza fedha nyingi kwenye viwanda vya mafuta nchini Angola, na viwanda vya madini ya shaba nchini Zambia. Bw. Maron anaona kuwa, watu mashuhuri na viongozi wengi wa nchi za Afrika wanaona mfumo wa kisiasa wa China una mvuto mkubwa kwao.
Mawasiliano ya biashara kati ya China na Afrika, na vitega uchumi vya China katika nchi mbalimbali barani Afrika vinatoa mchango muhimu kwa kuondoa wa umaskini katika nchi za Afrika. Gazeti la Dunia ya Vijana la Ujerumani toleo la tarehe 22, Julai lilisema kuwa, tarehe 7, Juni, Kamati ya Afrika ilitangaza ripoti kuhusu China kufanikiwa kuondoa umaskini katika maeneo makubwa zaidi. Katika ripoti hiyo, mafanikio ya China katika kuondoa wa umaskini yanachukuliwa kuwa ni mfano mzuri kwa nchi za Afrika. Balozi wa Uingereza nchini China Bw. Christopher Hum pia anasisitiza kuwa, maendeleo ya uchumi wa China si kama tu yanatoa michango muhimu katika uchumi duniani, bali pia yametoa mfano mzuri wa kuondoa umaskini duniani."
Mbali na hayo, njia ya biashara kati ya China na nchi za Afrika zinasifiwa na Kamati ya Afrika kwa kuondoa umaskini barani Afrika. Ripoti inayohusika inasema kuwa, thamani ya biashara ya vitu kwa vitu kati ya China na nchi za Afrika iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 26.3 mwaka jana kutoka dola za kimarekani bilioni 2 ya mwaka 1999. Jambo muhimu zaidi ni kuwa, China imeondoa ushuru na mipaka ya biashara kwa nchi 25 za Afrika zilizoko nyuma sana kiuchumi.
Habari zinasema kuwa, China ilianza kutekeleza sera ya kutoa misaada kwa nchi za Afrika katika muda mrefu uliopita, lakini viongozi wa nchi wanachama tajiri wa Kundi la Nchi 7 walipohudhuria mkutano wa viongozi wa Gleneges, bado walitoa ahadi kwa maneno tu. Aidha, China inaongoza nchi nyingine za magharibi katika kusamehe madeni ya nchi maskini kabisa duniani. Wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Oktoba, mwaka 2000, China ilipunguza au kusamehe madeni ya RMB yuan bilioni kumi kadhaa ya nchi 31 barani Afrika. Mbali na hayo, kwenye Mkutano wa Viongozi wa Gleneagles, wanasiasa wa China walitoa wito kwa nchi tajiri zitekeleze ahadi zao kwa vitendo.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-14
|