Mahitaji:
Nyama ya ng'ombe gramu 200, asparaga gramu 150, uyoga gramu 80 na uyoga wa majani gramu 80, kiasi kidogo cha vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, karoti, chumvi na sukari kila nusu ya kijiko, mchuzi wa soya, wanga kila kijiko kimoja, kiasi kidogo cha mafuta ya ufuta, na unga wa pilipili manga
Njia:
1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, na viweke kwenye bakuli moja pamoja na sukari, chumvi, mchuzi wa soya, koroga koroga.
2. osha asparaga na karoti uzikate ziwe vipande, tia vipande vya asparaga na karoti ndani ya maji yanayochemka, mimina mafuta ya kijiko moja, sukari na chumvi. Halafu zipakue.
3. pasha moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga, vipakue.
pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi , korogakoroga, halafu tia uyoga na uyoga wa majani, na vipande vya asparaga korogakoroga,mimina mchuzi wa soya, unga wa pilipili manga, chumvi, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, mimina maji ya wanga, korogakoroga, mwisho mimina mafuta ya ufuta. Vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-26
|