Hivi sasa watu wengi wanafuga wanyama kipenzi kama mbwa na paka nyumbani. Lakini wakati wakifurahishwa na wanyama hao, wanapaswa kutopuuza matatizo ya afya yatakayoweza kutokea kutokana na kufuga wanyama hao. Magonjwa gani yanaweza kuambukizwa na wanyama kipenzi, na vipi wanaweza kuambikiza magonjwa hayo? watu wanaweza kufanya nini ili kujikinga na magonjwa hayo?
Mzee Qin Liang mwenye umri wa miaka 60 hivi karibuni mara kwa mara amekuwa na matatizo ya kupumua, baada ya kufanyiwa upimaji, amegunduliwa kuwa na homa ya mapafu. Lakini katika upimaji wa pili, amegunduliwa kuwa na chembechembe za kupambana na vijidudu kwenye damu zilizoko kwenye ndege. Tatizo hilo linatokana na kasuku anayemfuga. Manyoya ya kasuku hubeba vijidudu, na wanaeneza vijidudu hivyo wakati wa kuruka. Mzee Qin alivuta hewa yenye vijidudu hivyo na kupata homa ya mapafu.
Watu wengi wamewahi kuwa na tatizo kama la Mzee Qin. Hospitali za Beijing zinapokea mara kwa mara wagonjwa wenye magonjwa yaliyosababishwa na wanyama kipenzi. Imefahamika kuwa, magonjwa zaidi ya 100 ya binadamu yanahusika na kufuga wanyama kipenzi, kati ya hayo, magonjwa 20 ni ya kawaida, yakiwemo psittacosis na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Mtafiti wa taasisi ya kukinga na udhibiti wa magonjwa ya China Bw. Wang Chengxin alieleza:
"kiudaktari, maradhi ya maambukizi yaani magonjwa ya pamoja kwa binadamu na wanyama, yanaambukiwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama."
Alisema kuwa, magonjwa ya pamoja kwa binadamu na wanyama yanatishia sana afya ya binadamu. Kwa mfano, ugonjwa wa SARS uliolipuka mwaka 2003 katika baadhi ya nchi na sehemu za Asia huenda ulitokana na wanyama; katika baadhi ya nchi za kusini mashariki ya Asia, kuna watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa mafua ya ndege. Mtafiti wa taasisi hiyo Bw. Shang Deqiu alieleza kuwa, kwa jumla kuna njia nne ambazo wanyama wanaweza kuambukiza magonjwa kwa binadamu, alisema:
"magonjwa tofauti yanaambukizwa kwa njia tofauti, kwanza ni kwa njia ya kupumua, nyingine ni kupitia njia ya koromeo, ngozi na kuumwa na wadudu fulani.
Ugonjwa wa kawaida unaoambukizwa kwa njia ya kupumua ni psittacosis, dalili zake ni homa kali, kukohoa, maumivu ya mapafu, hata unaweza kusababisha homa ya mapafu. Ugonjwa huo pia unaweza kuambukiza ndega na mifugo kama kuku na bata, ambao hauwezi kuonekana katika vipindi mbalimbali, kuanzia saa kadhaa hadi siku 21.
Ugonjwa wa kawaida unaoambukizwa kwa njia ya koromeo ni homa ya matumbo, binadamu wanapata ugonjwa huo kutokana na kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha wanyama. Ugonjwa huo unatokea kwa haraka, dalili zake ni kuuma tumbo, kuharisha na homa kali, na hautibiki kwa urahisi. Aidha, baadhi ya watu wanaruhusu wanyama kipenzi wao kuwalamba mikononi, usoni na hata kuwabusu, hali hiyo huenda inaweza kuambukiza ugonjwa kupitia njia ya koromeo.
Ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya ngozi ni ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Ugonjwa huo utaambukizwa kwa binadamu kutokana na kuumwa na wanyama kama paka na mbwa walioambukizwa ugonjwa huo. Wagonjwa wa ugonjwa huo wana dalili za homa, kuogopa baridi, mwangaza na upepo, na ugonjwa huo ukitokea, ni vigumu sana kuutibu.
Ugonjwa mkali kabisa unaoambulizwa kwa njia ya kuvutwa damu kuumwa na kwa wadudu ni ugonjwa wa tauni (Pestis). Kama paka au mbwa wakila panya wenye vijidudu vya tauni, hawataambukizwa ugonjwa, lakini vijidudu hivyo vitabaki mwilini mwao, na viroboto kwenye miili yao wanaweza kuwaambukiza wanadamu ugonjwa huo.
Mwanzo tumeeleza kidogo kuhusu magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama, sasa tumejua ni muhimu kuimarisha usimamizi wa wanyama kipenzi. Lakini watu wengi wanaofuga wanyama kipenzi hawajui vipi kujikinga na magonjwa hayo. Bi. Guo amefuga mbwa kwa miaka kadhaa, njia yake ya kuzuia maambukizi ni kumwogesha mbwa wake kwa kutumia dawa za kuogea, alisema:
"namwongesha mbwa wangu mara kwa mara, kwa kawaida namwogesha mara moja kila wiki. Natumia dawa za kuogeshea za hali ya juu, naona sina tena tatizo hilo."
Lakini kuogesha wanyama hakutatatuai matatizo yote. Wataalamu wameainisha kuwa, kwanza ni lazima kuzingatia usafi wa kufuga wanyama, mbali na kuwaogesha mara kwa mara, pia inapaswa kuwachana manyoya, kuondoa wadudu kwenye vibanda vya wanyama na kuondoa kinyesi chao mara kwa mara. Pili, inapaswa kuangalia hali ya wanyama mara kwa mara, kama wanaonekana vibaya au wanahangaika, huenda wamepata magonjwa. Wataalamu wanapendekeza kuwa, kama wanyama wakisadikiwa kuwa na magonjwa, ni lazima kuwapeleka hospitali mapema.
Mbali na kuimarisha kinga ya wanyama, ni muhimu zaidi kuimarisha kinga ya wafugaji. Mtafiti wa taasisi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa ya China Bw. Wang Chengxin alieleza:
"naona kitu cha kwanza ni kuzingatia usafi wa mwili na wa nyumbani, ama sivyo magonjwa yanaweza kuambukizwa. Pili ni kutogusana kwa karibu sana na wanyama, kwa mfano usiwaruhusu wanyama walambe mikono au uso wake na usilale pamoja nao. Tatu ni kupewa chanjo husika, kama vile chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa."
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-26
|