Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-02 20:28:40    
Chombo cha aina mpya cha kupasha maji moto

cri
Chuo kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai kimefanikiwa kutengeneza chombo cha aina mpya cha kupasha maji moto, kikilinganishwa na vyombo vingine vya aina hiyo, chombo hicho kinaweza kuokoa umeme kwa asilimia 75.

Vyombo vya kawaida vya kupasha maji moto kwa ajili ya matumizi ya watu vinatumia nishati nyingi kuongeza joto la maji. Lakini chombo hicho kinaweza kuingiza joto la hewa na kulibadilisha kuwa joto kali, na kulitumia joto hilo kuongeza joto la maji. Kiasi fulani cha umeme kinaweza kubadilisha joto la hewa mara tatu ya kiasi hicho, na umeme wenyewe unaweza kubadilishwa kuwa joto, chombo hicho kinajumlisha joto linalopatika na kwa njia mbili, na kupata joto mara nne ya kiasi hicho.

Kwani chombo hicho kinatumia joto la hewa kupasha maji, hivyo ndani ya chombo hicho maji na umeme vinagawanyika kwenye sehemu tofauti, hali hiyo inaweza kuhakikisha usalama kwa watu wanaotumia chombo hicho. Sifa nyingine ya chombo hicho kipya cha kupasha maji moto ni kwamba, kinaweza kutumika kwa miaka 15 hadi miaka 20.

Profesa wa Chuo kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai Pro. Wang Ruzhu alimwambia mwandishi wa habari kuwa, chombo hicho kina sehemu mbili, watu wanaweza kuweka sehemu yake kubwa zaidi nje ya nyumba, na kuweka sehemu ndogo ndani ya nyumba, ni rahisi kwa watu kutumia chombo hicho. Amesema, kutokana na uwezo wake mkubwa, chombo hicho kinaweza kupasha lita 150 za maji yanayohifadhiwa katika chombo hicho hadi nyuzi 60 ndani ya saa 2, na kuhifadhi joto la maji hayo kwa saa 24.

Hivi sasa, chombo hicho kipya kimepata hatadha ya taifa, na kimeanza kutengenezwa viwandani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-11-02