Kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi tarehe 28 Novemba, Semina ya kuwaandaa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea hasa kutoka nchi za Afrika yanafanyika hapa Beijing. Semina hiyo iliendeshwa kwa pamoja na wizara ya biashara ya China na taasisi ya utafiti wa chakula na umuaji wa chakula cha China. Mhusika wa semina hiyo Bwana Huang Yutong alipozungumzia kuhusu lengo la kuandaa mafunzo hayo akisema:
"Lengo la kuandaa semina hiyo ni kuwafahamisha watu husika wa nchi zinazoendelea hasa nchi za Afrika matokeo ya bioteknoljia ya chakula yaliyopatikana nchini China na kuzidisha urafiki wa jadi kati ya China na Afrika. China imepata mafanikio makubwa katika sekta hiyo, baadhi ya miradi hata imetia fora duniani."
Kati ya wanafunzi hao 63 , wako waswahili 11 wanaotoka Kenya, Tanzania, Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Mwandishi wetu wa habari aliwahoji wanafunzi hao wote, ambao wametoa maoni kuhusu manufaa ya semina hiyo kwao na walivyoiona China.
Bwana Emmanuel Komora anatoka wilaya ya Tana River, mkoa wa pwani wa Kenya, anafanya kazi katika wizara ya biashara na viwanda ya Kenya. Hii ni mara yake ya kwanza kufika China. Ameona kuwa, China kuna mambo mengi ambayo kule Kenya hayako, japokuwa China bado ni nchi inayoendelea, lakini kulinganishwa na Kenya na nchi nyingine za Afrika, China imeshajiendeleza katika tekinolojia ambazo zinafaa kuigwa na nchi za Afrika.
Bi. Hawa Msongo Kimolo ni mwenyekiti wa jumuiya ya kilimo cha viumbe cha Tanzania, anashughulikia usindikaji wa vyakula vya matunda, naye anasema kuwa, bioteknolojia ya chakula ya China itawasaidia sana watu wa Tanzania katika kuhimiza maendeleo ya usindikaji wa matunda.
Bi.Baguma Audax Agnes anafanya kazi katika wizara ya kilimo, ufugaji na samaki ya Uganda, anashughulikia hasa maendeleo ya maziwa. Anasema kuwa, ingawa amekaa China kwa siku chache tu, lakini ameshajifunza na kuona mambo mengi, biotekinolojia anayojifunza hapa China itamsaidia yeye pamoja na wenzake wa Uganda. Atawaelezea wenzake uzuri na umuhimu wa kutumia biotekinolojia katika kuongeza aina na utamu wa vyakula, kuhifadhi vyakula visiharibike haraka na kadhalika.
|