Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-08 17:54:46    
Mageuzi ya kodi ya mapato yafuatiliwa na watu

cri

Hivi karibuni mswada wa marekebisho ya "Kodi ya Mapato" ulipitishwa kwa wingi wa kura kwenye idara ya utungaji sheria ya China. Hayo ni marekebisho muhimu zaidi tangu kutekelezwa sheria ya kodi ya mapato, hususan ni kubadilisha kiwango cha kuanza kulipa kodi hiyo kutoka pato la Yuan 1,600 kwa mwezi kikilinganishwa na kile cha zamani cha Yuan 800. Ofisa husika alisema kuwa mabadiliko hayo yanaboresha uwezo wa kodi hiyo ya kurekebisha mapato ya watu na kuleta athari kubwa kwa maisha ya kiuchumi ya watu wa sekta mbalimbali nchini.

Katika kipindi cha hivi karibuni jambo lililofuatiliwa zaidi na wafanyakazi nchini ni mswada wa marekebisho ya sheria ya mapato. Kutokana na mswada mpya wa marekebisho ya sheria ya mapato, idara ya kodi ya China itatumia kiwango kipya ya kuanza kulipa kodi ya mapato kote nchini kutoka mwanzo wa mwaka ujao, yaani kutumia kiwango cha kuanza kulipa kodi cha pato la Yuan 1,600 kwa mwezi badala la Yuan 800. marekebisho hayo uanapongezwa na watu wengi wenye mapato ya wastani na chini wa China.

Bibi Chen Yuexiu wa mkoa wa Sanxi ulioko sehemu ya kaskazini ya China, mshahara wake ni kiasi cha Yuan 1,700 kwa mwezi, anaunga mkono sana marekebisho ya kodi ya mapato ya China. Bibi Chen alisema kuwa kiwango cha kuanza kulipa kodi kimeinuka, hatua hiyo ni kama kupunguza kodi kwa watu wenye mapato ya wastani na chini kama yeye. Alipiga hesabu mbele ya mwandishi wa habari.

"Sehemu kubwa zaidi ya mshahara wangu inatumika katika kulipa mkopo wa nyumba, na mshahara wangu unabaki kidogo sana baada ya kulipa gharama ya simu na usafiri. Kuinua kiwango cha kuanza kulipa kodi ya mapato hadi Yuan 1,600, Kiasi cha zaidi ya nusu ya idadi ya watu hawatalipa kodi ya mapato; Licha ya hayo, ingawa watu wengine wataendelea kulipa kodi ya mapato, lakini kutokana na kuinuka kwa kiwango cha kuanza kulipa kodi hiyo, fedha wanazolipa zitapungua pia. Hivyo fedha wanazookoa watu wa China zinazidi Yuan bilioni 28 kwa mwaka.

Kuhusu mswada wa marekebisho ya kodi ya mapato unaofuatiliwa na watu wengi nchini, kwa wafanyakazi wanaozingatia zaidi ni pochi zao za fedha, kwa wanauchumi wanachotia maanani ni madabiliko ya uwezo wa marekebisho wa kodi kuhusu athari zake kwa uchumi wa taifa, na kwa wataalamu wa elimu ya jamii wanachojali zaidi ni kupugua kwa tofauti kati ya watu maskini na matajiri.

Bw. Yu Guangyuan aliyeshiriki marekebisho ya kodi ya mapato, alisema kuwa marekebisho mengine muhimu yanayofanyika ni kuimarisha ukusanyaji kodi juu ya kundi la watu wenye mapato makubwa. Sheria mpya iliyorekebishwa inataka watu wenye mapato makubwa kulipa kodi kwa mujibu wa taarifa wanazotoa, idara za kodi zitaqapiga faini wale wasiotoa taarifa au kutoa taarifa za uwongo; Na wale waliofanya makosa makubwa watafunguliwa mashitaka. Kwa upande mwingine sheria hiyo mpya inafuata utaratibu wa usimamizi juu ya taarifa wanazotoa watu wenye mapato makubwa ili kutenzua dosari zilizoko katika ukusanyaji kodi.

Bw. Yu Guangyuan alisema kuwa mageuzi ya kodi hayo ni hatua moja muhimu ya kupunguza tofauti kati ya matajiri na watu maskini kwa kutumia kodi ya mapato.

"Kwani baada ya kuinua kiwango cha kuanza kulipa kodi, fedha za kulipa kodi ya mapato ya walipaji kodi pia zitapungua. Hivyo hatua hiyo ni muhimu sana kwa kuinua kiwango cha maisha ya watu wenye mapato ya chini, kupunguza hali isiyo ya haki katika ugawaji wa pato, kupunguza mgongano kati ya watu wenye pato kubwa na watu wenye pato dogo na kuhifadhi utulivu wa jamii."

Habari zinasema kuwa kiwango cha kuanzia cha pato la Yuan 800 kilitumika tokea mwaka 1993. Katika muda wa miaka zaidi ya kumi iliyopita baada ya hapo, uchumi na jamii ya China ilipata maendeleo makubwa, pato la watu, kiwango cha matumizi ya fedha na kiwango cha maisha pia viliinuka, tena njia za mapato na matumizi ya fedha pia yalitokea mabadiliko makubwa. Kwa mfano, hapo zamani njia za mapato za watu zilikuwa mshahara tu, lakini hivi sasa njia za mapato za watu ni nyingi zikiwa ni pamoja na faida kutokana na hisa na kufanya kazi ya pili. Hivyo imekuwa ya lazima kuinua kiwango cha ulipaji kodi.

Ni katika mazingira ya namna hiyo, China imeamua kuinua kiwango cha ulipaji kodi cha pato la Yuan 1,600. naibu waziri wa fedha wa China Bw. Lou Jiwei alisema kuwa kiwango hicho kimethibitishwa kutokana na mambo mengi yakiwa ni pamoja na kiwango cha matumizi ya watu maishani na uwezo wa mambo ya fedha wa serikali.

"Uthibitishaji wa kiwango cha ulipaji kodi ya mapato ni suala moja lenye utata mkubwa. Tunapaswa kuzingatia mambo yafuatayo: Kwanza, kiwango cha ulipaji kodi lazima ni kikubwa kuliko gharama ya maisha ya wakazi, hivi sasa kiwango cha gharama ya maisha ya watu ni kiasi cha Yuan 1,100, la pili ni kuwa kodi ya mapato ya wakazi wenye pato la wastani na la chini inapunguzwa kwa kiwango kikubwa, wakati kodi hiyo ya watu wenye pato kubwa inapunguzwa kidogo au kutopunguzwa kabisa. Tatu, tunatakiwa kufikiria ulingano kati ya sehemu na sehemu na kati ya makundi ya watu.

Kodi ya mapato siyo tu kwamba ni chombo cha kurekebisha mapato cha idara za uchumi za serikali, bali pia inaathiri mbinu ya kutunza fedha za watu na njia za uwekezaji vitega-uchumi. Hivi karibuni wakazi wa miji ya Beijing, Shanghai na Shenzhen wanapenda kujaribu baadhi ya njia mpya za utunzaji wa fedha zao za akiba ili kukwepa kodi ya mapato kwa njia za halali na kuongeza manufaa ya familia. Kwa mfano, kuwekeza kwa njia ya kununua hati zenye thamani za dhamana ya serikali ambazo hazitakiwi kulipa kodi ya mapato. Licha ya hayo, trust deposits na baadhi ya njia za kupata faida zilizotolewa na kampuni za bima pia zinapendwa na watu wengi kutokana na kutolipa kwa muda kodi ya mapato.

Mkazi wa Beijing bibi Liu Yu alinunua kati za dhamana za serikali mara nyingi katika miaka ya karibuni, alisema kuwa kununua hadi za dhamana za serikali hakuna hatari kubwa, tena uzuri wake ni kutolipa kodi ya mapato. Alisema kuwa katika siku za baadaye huenda atajaribu njia nyingine za kupata faida katika uwekezaji vitega-uchumi. Alisema kuwa katika mwezi uliopita alinunua hati za dhamana ya serikali, baada ya kupiga hesabu anaweza kupata faida ya Yuan zaidi ya 1,000 kwa mwaka, ambazo hazitakiwi kulipa kodi ya mapato, anaona njia hizo za uwekezaji ni nzuri zaidi.

Wachambuzi wanasema kuwa marekebisho ya kodi ya mapato yanayofanywa safari hiyo nchini China ni kugusa kidogo tu kuhusu kuinua kiwango cha ulipaji wa kodi ya mapato na kuimarisha usimamizi kuhusu ulipaji kodi wa watu wenye pato kubwa wala hayajagusa suala la asilimia ya ulipaji kodi na marekebisho ya ugawaji wa mapato, ambavyo ni masuala yanayofuatiliwa sana na watu, katika kipindi cha siku za baadaye watu wanaopata mshahara wangali ni watu muhimu wanaolipa kodi ya mapato. Hivyo bado kuna nafasi ya kufanya marekebisho kuhusu sheria ya kodi ya mapato ili kutumia ipasavyo umuhimu wa ukusanyaji kodi ya mapato katika kusawazisha mapato ya watu.