Hivi sasa, walimu na wanafunzi mijini nchini China wanaweza kujipatia ujuzi na habari kupitia njia mbalimbali, zikiwemo mtandao wa Internet, matangazo ya televisheni na redio, VCD and DVD. Lakini kwenye sehemu za vijijini, njia nyingi kati ya hizo hazipatikani. Ili kubadilisha hali hiyo, China ilianzisha mradi wa elimu kwa njia ya teknolojia za mtandao katika miaka miwili iliyopita.
Hivi karibuni, mwandishi wetu wa habari alikwenda wilaya ya Mengyin ambayo ni wilaya moja maskini mkoani Shandong. Katika kipindi hiki, tutawaelezea kidogo kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi huo kwenye shule za msingi za huko.
Shule ya msingi ya tarafu ya Changlu ni shule moja ya kawaida ya wilaya hiyo na ina wanafunzi zaidi ya 600. mwandishi wetu aliona kuwa, mbali na madarasa na mkataba za kawaida, shule hiyo pia ina darasa la kisasa la multimedia na darasa la kompyuta. Mkuu wa shule hiyo Bw. Zhang Fengxiang alieleza kuwa, vipindi vya elimu kwa njia ya teknolojia za mtandao vilianzishwa mwaka jana. Alisema:
"Vipindi vya elimu kwa njia ya teknolojia za mtandao, kama tulivyofahama hivi sasa ni kutumia teknolojia za kisasa za mfumo wa televisheni na mtandao wa kompyuta, kujifunza kutokana na uzoesdfu na mtizamo mema wa elimu ya kisasa kwenye sehemu nyingine na hasa nchi za nje, ili kuinua kiwango chetu cha elimu."
Alisema kuwa, ili kutekeleza mradi huo, idara ya elimu ya wilaya hiyo ililimbikiza kompyuta, televisheni, zana za DVD na vifaa vya kupokea matangazo ya saitelaiti kwa njia mbalimbali. Hivi sasa, nyingi kati ya shule zaidi ya 240 za msingi na sekondari kwenye wilaya hiyo zilianzisha vipindi vya elimu kwa njia ya teknolojia za kisasa.
Mkuu wa shule ya msingi ya tafaru ya Changlu Bw. Zhang Fengxiang alieleza kuwa, hivi sasa, walimu wanapoandaa masomo, hawana haja tena kuandika mpango wa masomo kama zamani, hivi sasa wanaweza kutazama vipindi vya kituo cha televisheni cha elimu, au kusoma mpango wa masomo ya walimu wa shule maarufu za miji mikubwa kama Beijing na Shanghai kupitia mtandao wa Internet. Hali hiyo imepanua mtizamo wa walimu na kusaidia kuinua kiwango cha madarasa yao.
Darasa la multimedia kwenye shule hiyo ni mara mbili kwa ukubwa kuliko darasa la kawaida. Ndani ya darasa hilo, kuna kompyuta moja na scrini moja mkubwa ya LCD, pamoja na televisheni na zana za DVD. Walimu wanaweza kuonesha picha na video zilizotengenezwa kwenye kompyuta au zilizopatikana kutoka kwenye mtandao kwenye scrini, na kufanya masomo yawavutie zaidi wanafunzi. Kutokana na tekenolojia za kisasa, wanafunzi wa sehemu hizo pia wanaweza kufahamu hali halisi ya dunia ya nje. Imefahamika kuwa, ili kuwapatia fursa kila mwanafunzi kusoma kwenye darasa hilo, shule iliweka mpango wa zama. Hivi sasa darasa hilo linatumika sana, hasa muda wote wa vipindi umepangiwa kila siku.
Mwandishi wetu alipoingia kwenye darasa la kompyuta, wanafunzi wengi walikuwa wanajifunza mbele ya kompyuta. Mwanafunzi mmoja wa kike Li Xue alisema kuwa, anapenda sasa vipindi vya kompyuta, hivi sasa anaweza kutumia kompyuta bila tatizo.
"sasa naweza kutype kwenye Word, pia naweza kuchora kwenye kompyuta, na hasa kutengeneza kadi ya salama kwenye kompyuta."
Darasa hilo kwa jumla lina kompyuta zaidi ya 50. kwa kawaida, kompyuta hizo zinaweza kutosheleza kila mwanafunzi wa darasa moja. Mwalimu Zhou Junxiang alisema kuwa, shule hiyo illianzisha vipindi vya kompyuta kuanzia darasa la tatu, na vipindi hivyo visipungua 30 kwa kila muhula . kutokana na kuwa wanafunzi wengi hawana kompyuta nyumbani, hivyo wanajifunza kwa makini sana kwenye vipindi hivyo. Alisema, baada ya masomo ya mwaka mmoja, wanafunzi wamejifunza ustadi mwingi wa kompyuta.
"wanafunzi wa darasa tofauti wana uwezo tofauti wa kutumia kompyuta. Kwa mfano, wanafunzi wa darasa la tatu wanaweza kutengeneza kadi nuzri ya salama ya kitaaluma; wanafunzi wa dara la tano au sita wanaweza kutengenisha na kuchapisha fomu ya maksi za wanafunzi kwenye mutihani. Aidha, wanafunzi wengi wanaweza kutype makala yao kwenye kompyuta, na kuzitumia shirika la magazeti kwe e-mail. Makala nyingi za wanafunzi zilichapishwa kwenye magazeti."
Hivi sasa, mradi wa elimu kwa njia ya tekenolojia za kisasa unatekelezwa na kuenezwa kwa kasi kwenye wilaya ya Mengyin. Mkuu wa idara ya elimu ya wilaya hiyo Bw. Zhang Baoguang alisema kuwa, utekelezaji wa mradi huo utasaidia kukusanya na kusawazisha raslimali za elimu za huko na kuinua kiwango cha walimu wa huko. Alisema:
"lengo letu ni kutimiza maendeleo ya elimu ya kisasa kwenye wilaya ya Mengyin katika miaka 3 hadi 5 ijiayo, yaani kuunganisha shule, madarasa kwa mtandao wa radio au wa kompyuta, na kufanya wanafunzi wa wilaya hiyo waweze kutumia raslimali nzuri, mafanikio mema na tekenolojia za juu za elimu kote nchini na hasa duniani, ili kubadilisha hali ya nyuma ya elimu ya wilaya hiyo."
|