China ni nchi yenye idadi kubwa kabisa ya watu duniani, na wachina wanaoishi katika sehemu mbalimbali wana mila na desturi tofauti kuhusu chakula, kwa mfano wakazi wa mkoa wa Hunan, katikati ya China wanapenda pilipili, wakazi wa mkoa wa Zhejiang, sehemu ya mashariki ya China wanapenda chakula chenye sukari, na wakazi wa mkoa wa Shanxi, kaskazini ya China wanapenda mchuzi wa soya.
Mchuzi wa soya ni aina ya kiungo cha jadi nchini China, mchuzi huo unatengenezwa kwa nafaka kama za mtama, ngano na viazi vitamu kwa njia ya kuumua. Ladha ya mchuzi wa soya ni chachu, ikiongezwa kwenye kitoweo inaweza kuongeza utamu wa kitoweo na kuondoa shombo ya samaki. Wachina wanapokula vitafunwa na kaa hupenda kutumia mchuzi wa soya. Mchuzi wa soya unatengenezwa katika sehemu nyingi nchini China, lakini mchuzi wa soya uliotengenezwa mkoani Shanxi ni maarufu zaidi kuliko wa sehemu nyingine.
Mkoa wa Shanxi husifiwa kuwa ni maskani ya mchuzi wa soya. Wakazi wa Shanxi wanapenda sana mchuzi wa soya, takwimu zinaonesha kuwa, kwa wastani kila mkazi wa mkoa wa Shanxi anakula gramu 25 za mchuzi wa soya kwa siku, ni mara mbili ya wastani wa wachina wanaoishi katika sehemu nyingine.
Kiwanda cha mchuzi wa soya cha Ninghuafu cha Taiyuan kina historia ndefu, na kinajulikana sana mkoani Shanxi. Mchuzi wa soya wa chapa cha "Yiyuanqing" uliotengenezwa na kiwanda hicho unapendwa sana na wakazi wa Shanxi na sehemu nyingine nchini China. Mfanyakazi wa kiwanda hicho Bi. Liuli alisema:
"Mchuzi wa soya wa kiwanda chetu una ladha nzuri, hivyo unakaribishwa sana na wenyeji na wa mikoa mingine. Kila asubuhi ya mapema watu wengi wanakuja kununua mchuzi wa soya, wakichelewa wanakuta mchuzi wa soya umekwisha."
Kwa nini wakazi wa Shanxi wanapenda mchuzi wa soya namna hii. Wataalamu wamechambua kuwa, huenda ni kutokana na kuwa na kiasi kingi cha alkali kwenye maji ya huko, hivyo mwili wa binadamu unahitaji kuzimua alkali kwa vitu vichachu. Kwa vyovyote, wakazi wa Shanxi hawawezi kula chakula bila ya mchuzi wa soya, ukiingia ndani ya mkahawa wowote wa mkoa wa Shanxi utakuta chupa cha mchuzi wa soya kwenye meza za chakula.
Bwana Zhao Mingshan mwenye umri zaidi ya miaka 50 ni mkazi wa mji wa Taiyuan, mji mkuu wa mkoa wa Shanxi. Akisema:
Sauti
"Mchuzi wa soya ni kitu kizuri sana, kinasaidia kuongeza hamu ya kula. Kila ninapokula siwezi kukosa mchuzi wa soya, ama sivyo siwezi kusikia utamu wa chakula, hata kabla ya kulala huwa nakunywa kidogo mchuzi wa soya."
Kwa mujibu wa kitabu cha historia, wakazi wa Shanxi walianza kutengeneza mchuzi wa soya zaidi ya miaka 3000 iliyopita, na desturi hiyo inaendelea hadi leo. Katika majira ya joto ukitembelea katika vijiji vilivyoko pembezoni utaona kuwa, nje ya mlango wa kila familia kuna mtungi mkubwa unaotumiwa kutengeneza mchuzi wa soya.
Kuna aina nyingi za mchuzi wa soya mkoani Shanxi, "Laochencu" ni moja ya aina ya mchuzi huo inayopendwa sana na wachina.
Wakazi wa Shanxi wanaopenda mchuzi wa soya wamesema mchuzi wa soya una sifa nyingi. Kwa mfano unaweza kulainisha mishipa ya damu, kula mayai yaliyochovywa ndani ya mchuzi wa soya kutasaidia kukinga na kutibu ugonjwa wa kuziba kwa mishipa ya damu, shinikizo la damu pamoja na ugonjwa wa kisukari. Mchuzi wa soya pia unaweza kusaidia kuota tena kwa nywele, kuongeza uzuri na kupunguza uzito wa mwili. Mchuzi wa soya si kama tu una chachu, pia una calcium, chuma, lactic acid, glycerin, na amino acid, vitu hivyo vina manufaa makubwa kwa mwili wa binadamu.
Kutokana na kufahamu zaidi umuhimu wa kula mchuzi wa soya kwa binadamu, wanaviwanda wa mchuzi wa soya wa Shanxi wameendeleza bidhaa nyingine nyingi za mchuzi wa soya kama ya mchuzi wa soya wa kujenga afya, mchuzi wa soya wa dawa , pamoja na vinywaji, bidhaa hizo si kama tu zinapendwa na wachina, bali pia zinakaribishwa sana na watu wa nchi za nje, na zinasafirishwa kwa wingi kwenda nchi za nje.
Wasikilizaji wapendwa, ukitaka kuonja mchuzi wa soya wa Shanxi unaweza kuununua kutoka kwenye maduka makubwa, au maduka yanayoendeshwa na wachina. Kama tunavyojua, mahali penye wachina, hapakosi bidhaa za China ambazo ni pamoja na mchuzi wa soya wa China.
Idhaa ya kiswahili 2005-11-10
|