Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-10 16:57:53    
Sanaa za utamaduni wa jadi wa kitibet zawavutia wateja

cri

Watu wa kabila la watibet waishio kwenye uwanda wa juu kabisa duniani, wamevumbua utamaduni mzuri wa jadi uliokuwepo katika maelfu ya miaka iliyopita, ambao ni pamoja na unajimu, kalenda ya jadi, ustadi wa kisanaa, matibabu, fasihi, mavazi, mapambo na michoro yenye umaalum wa kikabila. Leo tunazungumzia kuhusu mavazi ya "Gongbufu" na sanaa za Tangka ambazo ni sehemu moja ya utamaduni wa jadi wa kitibet.

Katika darasa moja la shule ya sekondari ya wilaya ya Linzhi, mashariki ya mkoa unaojiendesha wa Tibet, chini ya uongozi wa mwalimu, wanafunzi 37 wote walijifunza ushonaji wa nguo maalum ya kitibet iitwayo "Gongbufu".

Nguo za "Gongbufu" za huko Linzhi ni aina moja ya mavazi yenye umaalum wa kabila la watibet, zimekuwa na historia ya miaka ya 700. Nguo ya aina hiyo haina kola wala mikono, kipande cha mbele na cha nyuma vinafungwa pamoja kwa mkanda, kwenye mstari wa juu wa nguo na mkanda unashonwa mapambo maridadi, nguo hiyo inafanana kidogo na mavazi ya Robinhan yanayojulikana huko Scotland. Nguo za "Gongbufu" zinafaa kwa watu wanaoishi katika sehemu za milimani na misituni. Naibu mkuu wa shule ya wilaya ya Linzhi Bi. Lei Wanrong alipozungumzia kuhusu lengo la kuanzisha darasa hilo akisema:

"Hivi sasa ni watu wachache tu wanaoweza kushona nguo za "Gongbufu", hivyo lengo la kuanzisha darasa hilo ni kuwafundisha wanafunzi ustadi wa kushona nguo hiyo na kuenea utamaduni wa mavazi hayo duniani. Kwa sababu mwalimu wa darasa hilo ni fundi maarufu sana katika ushonaji wa nguo ya Gongbufu, hivyo darasa hilo linaungwa mkono na wazazi wa wanafunzi."

Mwalimu wa darasa hilo ni mshonaji maarufu wa kabila la watibet Bwana Ouzhu, mwaka huu ana umri wa miaka 60, alianza kujifunza ushonaji wa nguo ya Gongbufu alipokuwa na umri wa miaka 13. Hivi sasa anaendesha duka la kuuza nguo za Gongbufu, na kuwa na biashara nzuri. Mwaka mmoja uliopita, alialikwa kuwa mwalimu wa shule ya sekondari ya wilaya ya Linzhi, na mambo aliyofundisha yalirekodiwa na kutungiwa kuwa kitabu cha kiada. Bw. Ouzhu alisema:

"Nina wasiwasi kuwa utamaduni huo wa jadi wa kabila la watibet utapotezwa siku hadi siku. Nia yangu ya kuwafundisha wanafunzi ni kudumisha ustadi wa kushonea nguo za Gongbufu. Natumai kuwa, watu wengi zaidi wataweza kushona nguo hizo maalum."

Jambo hilo linatiliwa maanani na idara ya elimu ya sehemu ya Linzhi, ambayo imetenga fedha maalum kuhimiza kuandaa darasa hilo na kuandaa kitabu cha kiada. Naibu mkuu wa idara hiyo Bwana Yeling alisema:

"Nguo za Gongbufu ni mavazi maalum ya kitibet, ambazo zinaweza kuuzwa vizuri kwenye soko. Kama tukiacha juhudi za kurithisha utamaduni huo, basi utamaduni huo unaweza kutoweka kabisa hatimaye."

Kwenye mtaa wa mji wa Lahsa wenye maduka mengi yanayouza vitu vya utalii, kuna duka moja linalouza sanaa za Tangka. Tangka ni picha zinazochorwa au kutarizi sanamu za kidini, baada ya kubandikwa kwenye hariri ya rangi, hutundikwa kwenye mahekalu, ukumbi wa kuwekea sanamu za Buddha, mahali pa kukalia watawa na hata nyumbani kwa waumini wa dini ya kibuddha ya kitibet, ambayo ni sanaa maalum ya dini ya kibuddha ya kitibet. Sanaa za Tangka zinaonesha mambo mengi yanayohusu historia, unajimu na maisha ya kijamii ya kabila la watibet.

Mwendesha duka wa duka la Tangka la Bakuo ambaye pia ni mchoraji wa Tangka Bwana Cidanlangje alisema:

"Nia yangu ya kufungua duka hilo ni kuchuma pesa na kuwafahamisha watalii kutoka nje sanaa za Tangka na utamaduni wa kitibet."

Tofauti na maduka mengine yanayouza sanaa za Tangka, duka la Bw. Cidanlangje si kama tu linauza Tangka, bali pia linawafundisha mashabiki wa China na nchi za nje ustadi wa kuchora Tangka. Bw. Cidanlangje alisema kuwa, anawaandikisha wanafunzi kutoka nchi yeyote bila kujali umri, uraia na jinsia na bila kutoza malipo yoyote, lakini kutokana na eneo dogo la duka lake, anaweza kuwafunidha wanafunzi saba kila mara.

Tangka zilizochorwa na Cidanlangje zina thamani kubwa ya kisanaa, japokuwa zinauzwa kwa bei kubwa zaidi kuliko kuliko zile za maduka mengine, lakini zinakaribishwa sana na watalii kutoka nchi mbalimbali. Anaweza kuchuma Yuan laki tatu kwa mwaka, na hivyo ana uwezo wa kuwafundisha mashabiki bila malipo yoyote, na kuwafahamisha watu wengi zaidi kuhusu utamaduni wa Tangka.

Naibu mwenyekiti wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet Bwana Nimaciren aliona kuwa, utamaduni wa jadi wa kitibet haujaharibika au kuathirika kutokana na maendeleo ya utamaduni wa kisasa, unaonekana mahali popote katika mavazi, vyakula na mila na desturi. Ukitaka kujionea utamaduni wa jadi wa kitibet, kuja kutembelea.

Idhaa ya kiswahili 2005-11-10