Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-23 21:17:39    
Mikahawa ya kichina nchini Kenya

cri

Hadi kufikia sasa, hakuna mtu anayejua idadi halisi ya mikahawa iliyoko nchini Kenya. Mwenyeji mmoja wa huko alieleza kuwa, kuna mikahawa karibu 40 ya kichina mjini Nairobi. Labda takwimu hizo zipo kwenye orodha ya mikahawa inayoshughulikia aina mbalimbali za vyakula pamoja na chakula cha kichina, na nusu kati ya mikahawa hiyo inashughulikia chakula cha kichina tu. Hata hivyo mikahawa ya kichina inachukua sehemu muhimu katika shughuli ya mikahawa ya mitindo mbalimbali ya nchi za nje nchini Kenya.

Licha ya Nairobi, mikahawa ya kichina inasambaa katika miji mingine mingi nchini humo kama vile Mombasa, Nakuru na Kisumu. Kati ya mikahawa hiyo ya kichina, baadhi yake inaendeshwa na Kampuni ya China nchini Kenya, kama vile China Garden, na mingine ilianzishwa na watu wenye asili ya kichina wanaoishi huko, na mikahawa kama hiyo inachukua sehemu kubwa kati ya mikahawa yote ya kichina nchini Kenya.

Mikahawa ya kichina nchini Kenya inaonesha mtindo wa kichina kwa njia mbalimbali. Baadhi mikahawa ina majina maalum ya kichina, kwa mfano, Mikahawa ya Shanghai, Jiangsu na China Garden, na mikahawa mingine imepambwa kwa michoro au picha zenye mtindo wa kichina. Kati ya mikahawa hiyo mbalimbali, China Garden ina mtindo pekee wa kichina kutokana na majengo yake. Wakati ujenzi wake ulipokamilika mwaka 1994, lilisifiwa kuwa ni jengo la kwanza lenye undani wa utamaduni wa China barani Afrika.

Jengo la China Garden lililowekezwa na Kampuni ya mkoa wa Sichuan lina mtindo wa Mkoa wa Sichuan, China. Wapishi wake walitoka kwenye mkoa huo. Meneja wa mkahawa huo Bw. Tian He bado ni kijana, lakini amekuwa na uzoefu mkubwa katika shughuli za mkahawa. Amewahi kushughulikia chakula cha kichina kwenye Hoteli ya Hilton nchini Kuwait na Hungary. Alisema kuwa, ili kukidhi mahitaji ya wateja, amerekebisha kwa kiasi fulani mbinu za upishi wa chakula cha kichina kwenye mkahawa wa China Garden, hata hivyo anafanya juhudi kudumisha mtindo halisi wa chakula cha mkoa wa Sichuan.

Kati ya mikahawa mbalimbali ya kichina iliyoko huko Nairobi, mikahawa ya Longzhu, Huangbaoche na Tiantian ina wateja wengi kila siku, kutokana na kuwepo katikati ya mji wa Nairobi.

Mikahawa mingine ya kichina ipo kwenye majengo ya makazi au karibu na makazi. Dada mdogo wa Bwana Liu Dehai, mchezaji maarufu wa kiwanda cha Pipa wa China Bibi Liu Huiping aliendesha mkahawa ulioko kwenye jingo moja la makazi. Ndani ya jengo hilo, kuna chumba chenye zana zilizokamilika za kufanya mazoezi ya kujenga afya, na bwawa la kuogelea liko nje ya chumba hicho. Mkahawa wa Bibi Liu Huiping upo karibu na bwawa la kuogelea. Ni jambo la kufurahisha sana kwa watu kula chakula kitamu baada ya kufanya mazoezi na viungo na kuogelea.

Meneja wa Mkahawa wa Shanghai Bw. Li Wanxin anaeleza kuwa, hali nzuri ya hivi sasa ya mikahawa ya kichina imepatikana baada ya kufanya juhudi kubwa kwa muda mrefu. Bw. Li alikwenda Nairobi kutoka mji wa Shanghai, China, mwaka 1989. Mwanzoni alifanya kazi kwenye mkahawa mwingine kama mpishi. Mwaka 1992, yeye na marafiki zake wawili walianzisha kwa pamoja Mkahawa wa Shanghai. Alisema kuwa, alipofika huko Nairobi, kulikuwa na mikahawa mitatu au minne tu mjini humo, lakini katika miaka ya hivi karibuni, mikahawa ya kichina inaongezeka kwa haraka siku hadi siku. Hali hiyo inaonesha kuwa, chakula cha kichina kinapendwa na wenyeji wa huko. Licha ya mikahawa, baadhi ya hoteli za ngazi ya juu mjini Nairobi pia zinatoa huduma ya chakula cha kichina.

Mbali na wenyeji wa huko, wakazi waliohamia nchini Kenya kutoka Ulaya, maofisa wa Umoja wa Mataifa na wanadiplomasia wa nchi za nje walioko Kwenye vilevile ni wateja wa mikahawa ya kichina. Mkurugenzi wa kituo cha upashanaji habari na mambo ya umma katika shirika la mipango la mazingira ya Umoja wa Mataifa Bw. Blavik alikwenda kwenye mkahawa huo mara kwa mara. Hivi karibuni baada ya kwenda mkahawa wa China Garden, alitoa pendekezo kwa meneja Tian wa mkahawa huo akishauri kuanzisha mafunzo ya upishi wa chakula ya kichina, na yeye na mkewe wamependa kushiriki kwenye kikundi cha kwanza cha wanafunzi wa mafunzo hayo. Pia anapendekeza kuwa China Garden isibadilishe mtindo wake halisi wa kichina.

Lakini kwa meneja Tian, jambo hilo si rahisi kufanyika kama Bw. Blavik alivyosema. Hivi sasa ongezeko kubwa la mikahawa ya kichina linaleta ushindani mkubwa. Hali hiyo inaihimiza mikahawa hiyo ijizoee mahitaji ya masoko. Hivyo, kama mikahawa ya kichina itafanya mageuzi au la itategemea hali ya mahitaji ya wateja.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-23