Mahitaji
Nyama ya samaki gramu 400, yai moja, wanga vijiko 3, punje za msonobari vijiko viwili, vitunguu saumu gramu 5, maji 2/3 ya kikombe, mvinyo wa kupikia vijiko 2, siki vijiko 2, sosi ya nyanya vijiko vitatu, chumvi nusu ya kijiko, sukari nusu ya kijiko, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga wa pilipili manga kijiko kimoja, na ute wa yai vijiko viwili.
Namna ya kupika
1. osha nyama ya samaki, ikaushe na ikate iwe vipande na viweke kwenye bakuli moja, tia chumvi, sukari, mvinyo wa kupikia, mafuta ya ufuta, unga wa pilipili manga, wanga na ute wa yai, kisha korogakoroga?..
2. tia mafuta kwenye sufuria, pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60, chovya vipande vya nyama ya samaki kwenye yai lililokorogwa halafu chovya vipande vya nyama ya samaki kwenye wanga, uviweke kwenye sufuria na vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi, kisha vipakue.
3. Pasha moto tena, tia mafuta kidogo, tia vipande vya vitunguu saumu, korogakoroga, mimina maji na maji ya wanga korogakoroga halafu mimina kwenye vipande vya nyama ya samaki. Mwisho weka punje za msonobari kwenye vipande vya samaki, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|