Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-30 16:14:55    
Chuo cha kwanza cha Confucius barani Afrika

cri
    Sherehe ya kuzinduliwa kwa Chuo cha kwanza cha Confucius ilifanyika tarehe 19 katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Wajumbe wa zaidi ya 300 wa serikali za China na Kenya na sekta ya elimu walikusanyika kusherehekea kwa pamoja shughuli hiyo kubwa katika mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika.

    Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Kenya kimeznsihwa kutokana na mkataba kuhusu maingiliano ya utamaduni uliosainiwa na mawaziri wa elimu wa China na Kenya Bw. Zhou Ji na profesa Saitoti. Chuo hicho ni kimoja kati ya vyuo 16 vya Confucius vya China vilivyopangwa kuanzishwa kwanza duniani, pia ni chuo cha kwanza cha Confucius kilichoanzishwa na China barani Afrika.

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Chongli alitoa hotua kwenye sherehe ya uzinduzi wa chuo hicho akisema:

    "Kikiwa ni chuo cha kwanza cha Confucius barani Afrika, kuanzishwa kwa chuo hicho kimefungua ukurasa mpya wa maingiliano ya elimu kati ya China na Kenya, na hakika kitafanya kazi kubwa zaidi katika ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili."

    Balozi Guo alieleza kuwa, Confucius alikuwa mtaalamu maarufu zaidi wa elimu, fikra na nadharia katika historia ya China, pia ni mmoja kati ya watu mashuhuri zaidi 100 katika historia ya dunia. Confucius alianzisha mfumo wa fikra yake mwenyewe. Na fikra ya Confucius, dini za kikristo na kiislamu zimeundwa kuwa mifumo mitatu ya ustaarabu duniani. Chuo cha Confucius kinadhamiria kutoa mafunzo ya lugha ya kichina huku kikieneza na kutangaza utamaduni na historia ya kale ya China.

    Lugha ya kichina ni lugha inayotumiwa na idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, kadiri China inavyopata maendeleo makubwa na kufungua mlango wazi kwa nchi za nje, ndivyo umuhimu wa lugha ya kichina unavyoinuka duniani. Hivi sasa, kuna watu zaidi ya milioni 30 wa nchi za nje wanaojifunza lugha ya kichina, na masomo ya lugha ya kichina yameanzishwa katika vyuo vikuu zaidi ya 2500 vya nchi na sehemu zaidi ya 100, na vitabu vya masomo ya lugha ya kichina vinatumiwa na shule za msingi na sekondari nchini Marekani, Uingereza, Japan na Korea ya Kusini.

    Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia wa Kenya Bw. Kilemi Mwiria aliiwakilisha serikali ya Kenya kwenye sherehe ya uzinduzi wa chuo hicho, akisema:

    "Maingiliano ya utamaduni kati ya China na Kenya yalianzishwa tangu zamani sana. Kila mwaka China inawapa wanafunzi wa Kenya nafasi 10 za kupata tuzo ya masomo. Chuo cha Confucius kitatoa fursa nyingi zaidi kwa wakenya kuijua China."

    Ili kukidhi mahitaji ya mafunzo ya lugha ya kichina duniani, mwaka 2004 China ilianzisha "Kikundi cha uongozi cha mafunzo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa nchi za nje", na hivi sasa inatekeleza mpango wa kuhimiza idadi ya watu wa nchi za nje wanaojifunza kichina waongezeke hadi kufikia milioni 100, na kuanzisha vyuo vikuu vya Confucius duniani ni hatua muhimu ya kutimiza lengo hilo. Tokea chuo cha Confucius cha kwanza kianzishwe mwezi Novemba mwaka jana nchini Korea ya Kusini, China imeanzisha vyuo vya Confucius katika mabara ya Amerika, Ulaya na Afrika. Na lengo la China ni kuanzisha vyuo 100 vya Confucius duniani.

    Naibu mkurugenzi wa kikundi cha uongozi wa mafunzo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa nchi za nje Bibi Xu Lin alitumia salamu za pongezi kwa sherehe ya uzinduzi iliyofanyika huko Nairobi. Naibu mkuu wa chuo cha ualimu cha Tianjin Bw. Gao Yubao alisoma salamu hizo:

    "Uko urafiki wa jadi kati ya China na Afrika. Katika miaka 42 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Kenya, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unazidi kupata maendeleo. Kuanzishwa kwa Chuo cha Confucius kunatokana na matumaini ya wananchi wa China na Kenya, na hakika kitakuwa daraja la kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili."

    Kutokana na kukabidhiwa jukumu na Ofisi ya kikundi cha uongozi wa mafunzo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa nchi za nje ya China, chuo kikuu cha Ualimu cha Tianjin kinashughulikia maandalizi ya ujenzi wa chuo hicho na kazi ya kutoa mafunzo katika chuo hicho. Hivi karibuni, Chuo kikuu cha ualimu cha cha Tianjin kimetuma walimu wake na kusafirisha zana za utoaji wa mafunzo huko Nairobi.

    Mwalimu wa China atakayefundisha katika Chuo cha Confucius kwenye Chuo kikuu cha Nairobi Bibi Sun Jing alieleza kuwa, watu wengi wamejiandikisha kwenye chuo hicho, na 25 kati ya wanafunzi hao wamechaguliwa kuingia chuoni. Wanafunzi hao watajifunza masomo ya awali ya lugha ya kichina kutokana na utaratibu wa masomo wa chuo kikuu cha Nairobi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-30