Katika duka moja la sanaa lililoko karibu sana na kituo cha mambo ya biashara cha Beijing, meneja wa Kampuni ya maendeleo ya utamaduni ya Funo ya Beijing Bwana Zhu Zhigang aliwajulisha wateja sanaa kuhusu vinyago na michoro mizuri kutoka Bara la Afrika. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, wananchi wa China wamekuwa na hamu kubwa zaidi siku hadi siku juu ya Bara la Afrika, hivyo biashara yake imefanyika katika hali motomoto. Anaona kuwa wachina wana uwezo kabisa wa kutambua na kutathmini thamani ya utamaduni na sanaa ya Afrika. Wachina na waafrika wenye utamaduni wa kale ulio tofauti, lakini kila upande unapenda na kuwa na hamu kubwa ya kuelewa utamaduni wa upande mwingine, hali hii haiwezi kutathminiwa kibiashara.
Wananchi wa China na wa Afrika wanapendana tangu enzi na dahari. Mapema kabla ya miaka 700 na zaidi iliyopita, watalii wa China na Morocco waliwahi kutembeleana. Baada ya hapo, mwanamaji maarufu wa China ya kale Zheng He aliongoza kikosi cha merikebu kwenda nchi za Afrika kwa matembezi. Nchi ya China na bara la Afrika zikiwa machimbuko ya ustaarabu wa kale, zilikutana na ajali za namna moja katika zama za karibu, na zilihurumiana na kusaidiana siku zote katika mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni. Ndiyo maana Reli ya TAZARA iliyojengwa chini ya msaada wa China mpaka sasa unasifiwa na wananchi wa China na Afrika kuwa ni "Njia ya urafiki.
Hivi sasa wachina wengi zaidi wanapenda kwenda kwenye nchi za Afrika kufanya utalii, ambapo nchi 16 za Afrika zimekuwa nchi zinazowapokea watalii wa China. Meneja wa shirika la utalii wa kimataifa la China Bwana Zhang alisema, utalii barani Afrika umekuwa soko jipya linaloandaliwa na mashirika mbalimbali ya utalii nchini China. Mwaka jana watalii wa China wapatao elfu 50 waliwahi kwenda barani Afrika, mwaka huu idadi ya watalii wa China waliotembelea barani Afrika inaongezeka siku hadi siku. Mioyoni mwa wachina, wananchi wa Afrika ni marafiki na ndugu zao. Hivi sasa upendo kati ya wananchi wa China na wa Afrika umeongezeka zaidi. Meneja huyo alisema.
Kwa waafrika wengi, China ni "rafiki yao wa siku zote". Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia aliyemaliza ziara yake nchini China hivi karibuni, alimwambia mwandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua kuwa, katika mapambano yetu ya kujipatia ukombozi wa taifa, tuliwahi kutafuta misaada kutoka kwa nchi nyingine, lakini ni China tu ambayo siku zote ilisimama kwenye upande wetu. Kama kuna watu ambao wanajaribu kusemasema kuhusu urafiki kati ya Namibia na China, tutawajibu kithabiti, urafiki kati ya Namibia na China ulitokana na hisia halisi. Wananchi wa China walitusaidia wakati tulipokumbwa na taabu, hii imeonesha vya kutosha China ni rafiki yetu wa kikweli.
Chini ya hali mpya, ufuatiliaji wa pamoja wa China na Afrika unaongezeka siku hadi siku, China na Afrika zina maslahi na malengo ya pamoja katika kuhimiza kuanzisha utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa haki na halali duniani. Zimbabwe ambayo imewekewa vikwazo na nchi za magharibi imetunga sera yake ya "kuelekea mashariki". Rais Mugabe wa Zimbabwe alisema, Zimbabwe imetambua kutokana na hali yake yenyewe kuwa, nchi zinazoendelea zinapaswa kuimarisha mshikamano ili kukabiliana kwa pamoja msukosuko na changamoto zinazozikabili.
Nchi ya Senegal ilifufua uhusiano wa kibalozi kati yake na China mwezi Oktoba mwaka huu, baadaye ilitoa taarifa ikisema kuwa, kufufua uhusiano huo ni uamuzi wa kihistoria uliotolewa na rais wa nchi hiyo baada ya kuchambua kwa kina hali halisi kuhusu mambo ya siasa ya kijiografia duniani. Uamuzi huo umelingana kabisa na maslahi ya kimsingi ya wananchi wa Senegal.
Katika mambo ya kimataifa, China na Afrika zimefanya usawazishaji wa misimamo na ushirikiano barabara zaidi katika mambo mbalimbali, ili kulinda kwa pamoja haki na maslahi ya nchi nyingine zinazoendelea. China ikiwa mjumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama, inaunga mkono kwa msimamo dhahiri nchi za Afrika zilinde haki na maslahi yao ya mamlaka ya nchi, na kupinga uingiliaji kati kutoka nchi za nje. Kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, China inaunga mkono kuongeza kwanza uwakilishi wa nchi zinazoendelea hasa nchi za Afrika kwenye baraza la usalama.
Kwenye mkutano wa mawaziri wa shirika la biashara duniani uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2005, China ilitetea kithabiti kuhimiza nchi zilizoendelea zifute ushuru wa forodha na mgao kwa bidhaa. Ingawa China pia ni nchi inayoendelea, lakini imetangulia kufuta ushuru wa forodha kwa nchi 29 za Afrika ambazo maendeleo yao ya uchumi bado yako nyuma kabisa duniani, pia imepunguza na kufuta madeni ya nchi 31 za Afrika zinazodaiwa madeni makubwa na zenye matatizo ya kiuchumi.
Profesa wa Chuo kikuu cha kidiplomasia cha China Bwana Su Hao alisema, utamaduni wa China unaheshimu ustaarabu wa aina mbalimbali, kuishi maisha kwa masikilizano na kutafuta ustawi kwa pamoja. Ustawi wa Afrika ni msingi muhimu wa maendeleo ya masikilizano ya duniani. China siku zote inaichukulia kazi ya kuimiarisha mshikamano na ushirikiano na nchi za Afrika kuwa jukumu lake la linostahili duniani.
Na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kazi za maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini nchini China yametiliwa maanani na nchi za Afrika. Umoja wa Afrika umeahidi kufanya juhudi kubwa katika kuimarisha ushirikiano na mshikamano na China, na kuitaka China ishiriki kwenye mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya uchumi barani Afrika, pia unatumai kuwa China itaunga mkono na kushiriki kwenye mchakato wa utatuzi wa migogoro barani Afrika, vilevile kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji na kilimo, ili kuisaidia Afrika kutimiza amani, usalama na maendeleo.
Katika miaka ya hivi karibuni China na nchi za Afrika zimeimarisha ushirikiano siku hadi siku katika mambo ya kikanda, na kuongeza nguvu ya uwekezaji barani Afrika katika kuendeleza viwanda, mawasiliano na umeme na ujenzi wa miundo mbinu, ili kuboresha hali ya uzalishaji na maisha ya nchi za Afrika. Na misaada ya China ni misaada isiyo na masharti yoyote ya kisiasa.
Hivi sasa uaminifu wa kisiasa kati ya China na Afrika unaongezeka siku hadi siku. Nchi 47 kati ya 53 za Afrika zimewekeana uhusiano wa kibalozi na China. Na mwaka kesho wakati wa mkutano wa 3 wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, viongozi wa China na Afrika watafanya mkutano wa kwanza wa wakuu hapa Beijing.
Idhaa ya Kiswahili 2005-12-30
|