Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-04 17:01:53    
Mkoa wa Guizhou, China waimarisha utoaji wa elimu ya mafunzo ya kikazi vijijini

cri

Hivi sasa theluthi moja ya wanafunzi wa shule za sekondari ya chini za mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, hawawezi kujiunga na shule za sekondari ya juu, na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari ya juu za mkoa huo hawawezi kujiunga na vyuo vikuu kuendelea na masomo yao, wanafunzi hao hawana chaguo lingine isipokuwa kurudi vijijini. Ili kuwasaidia wanafunzi hao, mkoa wa Guizhou umeimarisha utoaji wa elimu ya mafunzo ya kikazi, ili kuwaandaa watu wenye ufundi halisi kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa vijiji.

Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2005 shule za elimu ya kati ya mafunzo ya kikazi ya mkoa wa Guizhou zimewaandikisha wanafunzi laki 1.09, kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na kile cha mwaka 2004, ambapo shule za elimu ya juu za mafunzo ya kikazi zimewaandikisha wanafunzi elfu 16.4, na kufanya idadi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ifikie elfu 39.

Ili kuendeleza elimu ya mafunzo ya kikazi vijijini, mkoa wa Guizhou unazitegemea shule za elimu ya kati mafunzo ya kazi za kiufundi mijini na wilayani, kutoa mafunzo ya ufundi wa kisayansi zinazohusu mambo ya kilimo, ili kuisaidia nguvukazi ya watu wa vijijini ambao hawajapata ajira wapate ajira. Licha ya hayo, mkoa huo umeanza kutekeleza mpango wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuhusu wanawake wa vijijini kujifunza kwa njia mbalimbali, na kuzishirikisha idara husika za sehemu ya mashariki na magharibi ya China, idara husika za mijini na vijijini kutoa elimu ya mafunzo ya kazi, ili kuwaongezea wanafunzi wa shule za elimu ya mafunzo ya kazi uwezo wa kujipatia ajira, na kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi kupata ajira.

Kwa wakati mmoja, mkoa wa Guizhou umeanzisha mpango wa kutoa mafunzo ya kazi za kiufundi unaohitajiwa zaidi katika jamii, kutokana na mahitaji halisi ya maendeleo ya uchumi na soko la nguvukazi.

Sehemu zinazojiendesha za kabila la Wabuyi na Wamiao, kusini mwa mkoa wa Guizhou, zimetoa mfano mzuri wa elimu ya mafunzo ya kazi, wanafunzi wanaopata elimu ya nadharia kwenye shule zinazotoa mafunzo ya kazi, hutumia nadharia hizo kwenye vituo mbalimbali, na kujifunza namna ya kuendesha na kusimamia kampuni katika makampuni ya familia, mfano huo umeonesha mustakbali mzuri wa elimu ya mafunzo ya kazi, na kutoa fursa nyingi za ajira kwa wanafunzi hao.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-04