Bw. Li Zhaoxing
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Qin Gang tarehe 5 alitangaza mjini Beijing kuwa waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Li Zhaoxing atafanya ziara rasmi katika nchi sita za Jamhuri ya Cape Verde, Jamhuri ya Senegal, Jamhuri ya Mali, Jamhuri ya Liberia, Jamhuri ya shirikisho la Nigeria na Jamhuri ya Kiarabu Libya kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 19 mwezi huu.
Bw. Qin Gang alisisitiza kuwa urafiki wa jadi kati ya China na Afrika umejengwa katika msingi wa kuheshimiana katika mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na China ina msimamo mwafaka siku zote katika kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika.
Bw. Qin Gang alisema kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano hasa ushirikiano wa nishati na nchi za Afrika katika maeneo mbalimbali kwa njia ya pande mbili na baraza la ushirikiano la China na Afrika ambalo ni jukwaa la pande nyingi. Jambo hilo linaambatana na maslahi za pande mbili China na Afrika na linasaidia kuhimiza maendeleo ya pamoja ya nchi za Afrika.
Qin Gang aliainisha kuwa kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa China na kutambua kanuni ya kuwepo kwa China moja ni sharti muhimu la kwanza la kisiasa kwa China kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi zote duniani. China na nchi za Afrika zimekuza uhusiano wa kirafiki wa jadi katika msingi huo.
Bw. Qin Gang alisema kuwa kukua kwa uhusiano kati ya China na Afrika na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kirafiki kunafuatana na mkondo wa zama tulizo nazo wa "kufuatilia amani, kuhimiza ushirikiano na kutafuta maendeleo". Bw. Qin Gang alieleza kuwa China inaamini uhusiano wa kirafiki wa jadi kati ya China na Afrika utaendelezwa kwa kina zaidi katika msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja, huu ni mkondo usiozuilika.
Waziri wa mambo ya nje wa China Li Zhaoxing atazitembelea nchi hizo sita za Afrika kutokana na mialiko ya waziri wa mambo ya kidiplomasia, ushirikiano na uhamiaji wa Cape Verde Bw. Manuel Inocencio Sousa, waziri wa mambo ya taifa ya kidiplomasia wa Senegal Bw. Sheikh Tidiane Gadio, waziri wa mambo ya kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa wa Mali Bw. Modibo Sidibe, waziri wa mambo ya kidiplomasia wa serikali ya mpito ya taifa ya Liberia Bw. Thomas Yaya Nimely , waziri wa mambo ya kidiplomasia wa Nigeria Bw. Oluyemi Adeniji na katibu wa kamati kuu ya umma ya mawasiliano na nje na ushirikiano wa kimataifa ya Libya Bw. Abdel Rahman Shalgam.
Idhaa ya kiswahili 2006-01-06
|