Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-16 19:40:34    
Ongezeko la kiasi kikubwa lapatikana katika shughuli za utalii nchini China

cri

Mwaka 2004 kiwango cha shughuli za utalii nchini China kiliinuka na ongezeko la kiuchumi la kiasi kikubwa lilipatikana katika shughuli za utalii.

Takwimu zilitolewa na idara ya utalii tarehe 27 Desemba 2005 kuhusu mapato ya shughuli za utalii ya mwaka 2004 ilionesha kuwa, katika mwaka 2004, mapato ya mwaka ya mashirika 32638 ya utalii yamefikia yuan bilioni 267.5, na ambapo mashirika hayo yalitoa ushuru yuan bilioni 9.65 kwa serikali.

Mapato yaliyopatikana katika mashirika 14927 ya utalii kote nchini China yalifikia yuan bilioni 101.7, hili ni ongezeko la asilimia 55.92 ikilinganishwa na mwaka 2003; mashirika ya utalii yalitoa ushuru wa yuan milioni 695 kwa serikali, hili ni ongezeko la 4.35% kuliko mwaka 2003.

Mapato ya hoteli za ngazi ya nyota kote nchini China yalifikia yuan bilioni 123.8, hili ni ongezeko la yuan bilioni 25.5 kuliko mwaka 2003, na ni ongezeko la 26% kuliko mapato ya mwaka 2003; ushuru uliotolewa kwa serikali ulifikia yuan bilioni 7.1, hili ni ongezeko la 43.5% kuliko mwaka 2003.

Mapato kutoka sehemu za utalii, kampuni zinazotoa vyombo vya usafiri wa kitalii na mashirika mengine ya utalii mwaka 2004 yalifikia yuan bilioni 41.9, ushuru uliotolewa kwa serikali ulifikia yuan bilioni 1.84, na kupata faida za yuan bilioni 27.75.

Takwimu zilizotolewa na idara ya utalii ya China zimeonesha kuwa, mwaka 2004, kulikuwa na mashirika ya kitalii, hoteli za ngazi ya nyota, sehemu za utalii na mashirika mengine 32638, hii ni ongezeko la 7.7% kuliko mwishoni mwa mwaka 2003.

Mpaka mwishoni mwa mwaka 2004, idadi ya wafanyakazi katika idara za utalii ilifikia milioni 2.44, hii ni ongezeko la 1% ikilinganishwa na lile la mwaka 2003; thamani ya mali zisizohamishika za mashirika ya utalii ilifikia yuan bilioni 472.6, hili ni ongezeko la 8.9% ikilinganishwa na lile la mwishoni mwa mwaka 2003, na 68.3% ya mali hizo inamilikiwa na hoteli za ngazi ya nyota.

Mikoa kumi yenye mashirika ya utalii, mahoteli ya ngazi ya nyota na sehemu za utalii ambazo thamani ya mali zao zisizohamishika inachukua nafasi 10 za mbele ni pamoja na Guangdong, Beijing, Shanghai, Jiangsu, Zhejiang, Shandong, Sichuan, Liaoning, Hubei, na Yunan.