Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-17 17:02:42    
Kwa mara ya kwanza mapato waliyopata wakulima kutokana na shughuli zisizo za kilimo yawa makubwa kuliko mapato yanayotokana na kilimo mkoani Shandong

cri

Kuanzia mwaka 2005, mapato ya wakulima yanaendelea kuongezeka kwa haraka mkoani Shandong, China. Takwimu zilizokusanywa na kikundi cha uchunguzi wa kilimo katika familia 4200 za wakulima mkoani humo zinaonesha kuwa, toka mwezi Januari hadi mwezi Septemba mwaka 2005, kwa mara ya kwanza wastani wa mapato waliyopata wakulima kutokana na shughuli zisizo za kilimo yalikuwa makubwa kuliko mapato yaliyotokana na kilimo, na hii imekuwa njia mpya ya ongezeko la mapato ya wakulima.

Kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Septemba mwaka 2005, kwa wastani mapato ya kila mkulima mkoani humo yalikuwa ni yuan 3350.5, ambayo yaliongezeka kwa yuan 462.4, hili ni ongezeko la 16% kuliko mwaka 2004 wakati kama huu. Miongoni mwa mapato hayo, mapato yaliyotokana na shughuli zisizo za kilimo yalikuwa ni yuan 1740.5, na mapato yaliyotokana na kilimo yalikuwa ni yuan 1610. Mchango uliotolewa na shughuli zisizo za kilimo kwa kuwasaidia wakulima kuongoza mapato ulikuwa ni asilimia 61.3, hili ni ongezeko la asilimia 18 kuliko mwaka 2004 wakati kama huu.

Uchumi wa mashirika ya binafsi umepata maendeleo makubwa, na mapato ya wakulima yanayotokana na shughuli mbalimbali zisizo za kilimo iliendelea kwa haraka, mwaka 2005 ongezeko hilo ilikuwa kubwa zaidi katika miaka kumi iliyopita. Mapato ya wakulima yanayotokana na shughuli za viwanda yaliongezeka kwa asilimia 31.2, hili ni ongezeko la asilimia 22.9 kuliko lile la mwaka jana. Mapato yanayotokana na shughuli zisizo za kilimo yaliongezeka kwa asilimia 33.1, hili ni ongezeko la asilimia 23.7.7 kuliko mwaka jana.

Kazi ya kupunguza ziada ya nguvu kazi vijijini imeboreshwa, na mapato yanayotokana na kufanya kazi za vibarua mijini yanatoa mchango mkubwa zaidi kwa ongezeko la mapato ya wakulima. Katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2005, mapato yaliyotokana na kufanya kazi za vibarua mijini yalikuwa ni yuan 1046, ambayo yaliongezeka kwa yuan 132.9, yaani ongezeko la asilimia 14.6, na mchango wa mapato hayo kwa ongezeko la mapato ya wakulima ulichukua asilimia 28.7 katika mapato yote.

Sababu kubwa iliyoleta ongezeko kubwa la mapato ya wakulima ni kutokana na utekelezaji wa sera. Sera za kupunguza au kufuta kodi za kilimo, kutoa ruzuku kwa wakulima wanaozalisha nafaka na wakulima wanaonunua mbegu bora na mashine kubwa za kilimo, na sera ya kuweka kikomo cha bei ya kununua nafaka imelinda maslahi ya wakulima wanaozalisha nafaka.

Habari kutoka idara husika zinasema kuwa, kutokana na masuala ya kuhama kwa ziada ya wa nguvu kazi usio na utaratibu, na sifa ya nguvu kazi kuwa ya chini, kuanzia mwaka huu, mkoa wa Shandong uliimarisha usimamizi wa uhamiaji wa nguvu kazi, na idadi ya wakulima wanaofanya kazi katika mikoa mingine inaongezeka siku hadi siku. Inakadiriwa kuwa, toka mwezi Januari hadi mwezi Septemba mwaka 2005, kwa wastani mshahara wa kila mkulima ambaye anafanya kazi katika sekta zisizo za kilimo au kufanya kazi katika mikoa mingine uliongezeka kwa kiasi kikubwa.

Aidha, sehemu mbalimbali za mkoa wa Shandong zinatilia maani sana kazi ya kulipa mishahara iliyocheleweshwa ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini iliyocheleweshwa, na kulinda maslahi na haki ya wakulima hao. Hadi sasa mkoani humo mishahara ya yuan bilioni 3.17 imelipwa, na kazi hiyo ya kulipa mishahara iliyocheleweshwa kimsingi imemalizika.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-17