Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-19 16:55:31    
Idara za dini za China zaimarisha maingiliano na mawasiliano ya kimataifa

cri

Shirikisho la maingilaino ya utamaduni wa kidini la taifa la China ambalo ni jumuiya ya kiraia inayoundwa na makundi ya dini mbalimbali ya China, lilianzishwa tarehe 30 Desemba mwaka 2005 hapa Beijing. Ofisa wa shirikisho hilo amesema kwa kupitia shirikisho hilo, katika siku zijazo makundi ya dini ya China yataweza kuanzisha shughuli za maingiliano ya kidini ya kimataifa, na kuhimiza maelewano na ushirikiano na idara za dini za sehemu mbalimbali duniani.

China ni nchi yenye dini nyingi, ina waumini wa dini zaidi ya milioni 100, ambao wanaamini dini ya kibudha, dini ya kidao, dini ya kiislamu na dini ya kikristo. Takwimu zisizokamilika zinaonesha kuwa, nchini China kuna sehemu zaidi ya elfu 80 za kufanyia shughuli za kidini, na kuna makundi ya dini zaidi ya 3000.

Mbali na dini ya kidao ambayo ni dini yenye asili ya China, dini nyingine za kibudha, kiislamu na kikristo zote zilienea nchini China kutoka nchi za nje, hivyo tunaweza kusema maingiliano ya kidini kati ya China na nchi za nje yalianzia tangu zama za kale na hayakusimama mpaka leo. Kwenye mkutano wa kuanzishwa kwa shirikisho la maingiliano ya utamaduni wa kidini la taifa la China, mkurugenzi wa shirikisho la dini ya kiislamu la China Imam mkuu Chen Guangyuan alisema, kwa kupitia shirikisho hilo, shirikisho la dini ya kiislamu la China litaweza kuongeza maingiliano na mashirika ya dini ya kiislamu ya nchi mbalimbali duniani, na kueleza matumaini mema juu ya amani ya dunia. Akisema:

"Watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaoamini dini tofauti wanatakiwa kuelewana. Wanapaswa kufahamiana kwa kuimarisha maingiliano na mawasiliano ya kirafiki na yenye usawa, kubadilishana uzoefu, kusaidiana na kutimiza lengo la kuishi na kujiendeleza kwa masikilizano, na kuleta amani ya dunia nzima."

Utamaduni wa kidini ulianzia tangu enzi na dahari nchini China na katika nchi na sehemu nyingine nyingi duniani, na umekuwa sehemu moja muhimu ya historia na utamaduni wa binadamu. Watu wa idara za dini za China wanaona kuwa, kwa kupitia maingiliano katika sekta ya utamaduni wa kidini watu wa nchi na sehemu mbalimbali duniani wanaweza kutimiza lengo la kuelewana na kubaliana. Ndiyo maana, katika miaka ya hivi karibuni, makundi makubwa ya kidini ya China yalianzisha shughuli nyingi za maingiliano ya kidini na nchi mbalimbali.

Kwa kupitia shughuli hizo, idara za kidini za China zilienzi wazo la kila dini, pia ziliiwezesha dunia ielewe hali halisi ya uhuru wa uamini wa dini nchini China. Naibu mkurugenzi wa shirikisho la maingiliano ya utamaduni wa kidini la taifa la China Bwana Qi Xiaofei alisema, katika siku zijazo shirikisho hilo litatoa misaada na uungaji mkono kwa makundi mbalimbali ya dini ya China kuanzisha shughuli zao za maingiliano ya kidini na nchi mbalimbali duniani. Alisema:

"Shirikisho hilo litafanya juhudi kuanzisha maingiliano na ushirikiano wa mambo ya dini kati ya China bara na sehemu za Taiwan, Hong Kong na Makao pamoja na wachina wanaoishi ng'ambo na watu wa sekta mbalimbali za jamii za nchi na sehemu nyingine duniani, ili kuchimba na kuenzi kwa pamoja ubora wa utamaduni wa kidini, kusaidia kwa dhati kuanzisha shughuli za maingiliano na ushirikiano."

Habari zinasema mwaka huu makundi ya dini ya China yataanzisha shughuli nyingi kubwa za maingiliano ya utamaduni wa kidini pamoja na kuitisha mkutano wa baraza la dini ya kibuddha duniani, kufanya maonesho ya Biblia ya kikristo ya China nchini Marekani, kushiriki kwenye mazungumzo ya pande mbili kati ya idara za dini ya kikristo na idara za dini ya kiislamu duniani. Idara za dini za China zinatumai kuwa kwa kupitia shughuli hizo, zitahimiza maingiliano ya kidini kati ya nchi na sehemu mbalimbali duniani, ili kuondoa hali ya kutoelewana vizuri, na kujenga amani kwa pamoja.

Idhaa ya kiswahili 2006-01-19