Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-24 16:03:20    
Barua 0122

cri

Leo tunapenda kuwaarifu wasikilizaji wetu kuwa, Kituo cha FM cha Radio China kimataifa hapa Nairobi Kenya kitazinduliwa rasmi kuanzia Tarehe 28 mwezi Januari. Kuanzia siku hiyo, matangazo ya Radio China kimataifa kwa lugha ya kiingereza, lugha ya Kiswahili na lugha ya kichina kwa ujumla yatasikika kwa saa 19 kwa siku nchini Kenya, kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 6 usiku kwa saa za Afrika mashariki. Na matangazo yetu kwa lugha ya Kiswahili yatasikika kwa saa tatu kwa siku kwenye wimbi la FM.

Matangazo ya Radio China kimataifa kwa lugha ya Kiswahili yatasikika kwa saa tatu kwa siku kwenye mitabandi 91.9 kwenye wimbi la FM, saa ya kwanza ni kuanzia saa 2 hadi saa 3, saa ya pili ni kuanzia saa 10 hadi saa 11, na saa ya mwisho ni kuanzia saa 2 hadi saa 3 usiku.

Msikilizaji wetu Xavier L.Telly Wambwa wa Bungoma Kenya ametuletea barua pepe akisema kuwa, jumapili iliyopita yeye na familia yake walisikiliza kipindi cha sanduku la barua anatamani sana kutupongeza kupitia njia ya simu kuhusu Kituo cha FM cha Radio China kimataifa kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Januari huko Nairobi Kenya, lakini kwa bahati mbaya hajapata kununua simu.

Bwana Wambwa anasema, kwa hakika sisi wafanyakazi wote wa Radio China kimataifa tumefanya juhudi kubwa katika kuendelea kuchapa kazi ya kuboresha vipindi vyetu mbalimbali. Anasema mwaka jana baada ya kuchaguliwa kuwa msikilizaji aliyepata tuzo maalum ya kuja China kuwa mgeni wa Radio China kimataifa, alipokuwa ofisi ya idhaa ya Kiswahili alipata fursa ya kuwachunguza wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa, aliona wengi wao wakichapa kazi motomoto kabisa bila kujali kutoa jasho, ambapo wanajitolea kwa upendo wao wa kazi ili kufanikisha zaidi madhumuni ya idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa ya kuwahudumia wasikilizaji wake.

Bwana Wambwa anasema kumbukumbu hiyo imetokana na habari nzuri kuhusu Kituo kipya cha FM cha Radio China kimataifa kinachojengwa huko Nairobi Kenya kukaribia kukamilika. Tarehe 15 Januari mwaka 2006 yaani jumapili iliyopita, yeye na familia yake walipata habari kutoka kwa idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa kuhusu Kituo cha FM cha Radio China kimataifa kitazinduliwa rasmi tarehe 28 Januari na kurusha matangazo yake kwa kiingereza, Kiswahili na kichina kwa saa 19 kila siku. Anasema hii ni furaha iliyoje kwa wasikilizaji. Hayo yote ni mafanikio ya hivi sasa katika China na Kenya.

Anasema kutokana na maelewano ya kidiplomasia, mchakato wa amani, maendeleo baina ya serikali ya China na Kenya, kweli tumepiga hatua kubwa katika mwaka huu wa 2006. Na wamesikiliza risala ya mwaka mpya iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa Radio China kimataifa Bwana Wang Gennian?wanaona kuwa hotuba yake ni nzuri sana ambayo inawafurahisha wasikilizaji.

Bwana Wambwa anasema kwake yeye ni furaha kubwa sana kwani anakumbuka kuwa alipoizuru China mwaka jana 2005, alimkabidhi mama Chen kitabu chake rasmi cha hotuba, akiwa na maombi kadhaa, moja ni kutarajia kujengwa kwa kituo cha radio na televisheni cha China barani Afrika hasa Kenya kama ikiwezekana. Sasa kila siku barani Afrika mambo mapya mbalimbali yanatokea moja baada ya jingine. Anashukuru Mungu kwa tukio la kuzinduliwa kwa Kituo cha FM cha Radio China kimataifa kwa sababu huu ni kama utabiri aliotabiri na sasa umewadia.

Kwa hivyo anatuomba sisi wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa, kuwa itakuwa vyema kama wao wasikilizaji wataalikwa rasmi kuhudhuria sherehe ya kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China kimataifa mwishoni mwa mwezi huu huko Nairobi Kenya. Anatumai kuwa hivi sasa Bw. Alley ?Chen Yonghua yeye akiwa mwandishi wa habari wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China kimataifa huko Nairobi Kenya ana furaha zaidi kushuhudia kwa macho yake kituo hicho kinapojengwa. Hata hivyo anadhani kuwa baadhi ya wasikilizaji wa Radio China kimataifa wataalikwa kupanga pamoja ratiba ya vipindi kukifanya Kituo cha FM cha Radio China kimataifa huko Nairobi Kenya kiendelee kujulikana, kusikika, na kung'ara zaidi duniani kama nyota ya usiku juu ya mbinguni.

Bwana Wambwa Anamaliza barua yake kwa kusema wachina na waafrika tuzidi kupendana, upendo wa milele daima na hongera kwetu sisi sote wafanyakazi na wachina wote kwa mafanikio hayo ya kuzinduliwa rasmi kwa Kituo kipya cha FM cha Radio China kimataifa Tarehe 28 Januari mwaka 2006. Anasema anatumai kazi watapata, elimu itaongezeka, ujuzi utaimarishwa, polepole ndio mwendo, haraka haraka haina baraka. Huu ni mwanzo tu.

Tunamshukuru sana Bwana Wambwa kwa barua yake ya pongezi kwa kituo cha FM cha Radio China kimataifa kitakachozinduliwa rasmi tarehe 28 Januari mwaka huu 2006. Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu watatufuatilia, kusikiliza kwa makini vipindi vyetu, ingawa mwanzoni huenda hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika vipindi vyetu kutokana na nguvu isiyo ya kutosha ya idhaa yetu kwa hivi sasa, lakini kama alivyosema polepole ndio mwendo, Radio China kimataifa itapiga hatua mpya ya kuendeleza kazi ya kituo hiki kipya cha FM, tuna imani kubwa mafanikio yatapatikana katika kazi yetu chini ya juhudi za sisi wafanyakazi wote pamoja na wasikilizaji wetu wote.

Na mwisho tunapenda kuwaarifu tena wasikilizaji wetu kuwa, Kituo cha FM cha Radio China kimataifa cha Nairobi Kenya kitazinduliwa rasmi kuanzia Tarehe 28 mwezi Januari. Kuanzia siku hiyo, matangazo ya Radio China kimataifa kwa lugha ya kiingereza, lugha ya Kiswahili na lugha ya kichina kwa ujumla yatasikika kwa saa 19 kwa siku nchini Kenya, kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 6 usiku kwa saa za Afrika mashariki. Na matangazo yetu kwa lugha ya Kiswahili yatasikika kwa saa tatu kwa siku kwenye wimbi la FM.

Matangazo ya Radio China kimataifa kwa lugha ya Kiswahili yatasikika kwa saa tatu kwa siku kwenye mitabandi 91.9 kwenye wimbi la FM, saa ya kwanza ni kuanzia saa 2 hadi saa 3, saa ya pili ni kuanzia saa 10 hadi saa 11, na saa ya mwisho ni kuanzia saa 2 hadi saa 3 usiku. Karibuni mtusikilize. Ni matumaini yetu kuwa, wasikilizaji wetu mtatufuatilia, kutusikiliza kwa makini, na kutoa maoni na mapendekezo yenu ili kutusaidia kuandaa vipindi vizuri zaidi vya kuwafurahisha wasikilizaji.

Fuatilia kipindi hiki cha sanduku la barua, tutaandaa mashindano madogo ya chemsha bongo kuhusu matangazo ya kituo chetu kipya cha FM, wasikilizaji watakaosikiliza kwa makini na kutoa maoni na mapendekezo mazuri watapata zawadi bila shaka.

Idhaa ya kiswahili 2006-01-24