Mtangazaji
Fafanua kidogo, una maana gani unaposema michezo kwa ajili ya afya na kwa ajili ya uchumi.
Bwana Urio
Uwanja huo utatumika kuwapokea wanamichezo na wageni wengine watakaokuja kwa ajili ya michezo. Tunataka kuutumia uwanja huo kwa kila namna na kuweza kutega uchumi kuleta fedha za kigeni ili ziingie nchini kwetu kupitia michezo. Wakiwa Tanzania wageni hao wataumia pesa hizo na tutaweza hata kuwapeleka kwenye mbuga za wanyama ambako nako wataumia pesa zao.
Lakini vilevile sio uchumi tu, vilevile tutautumia uwanja huo kwa ajili ya michezo kwa ajili ya amani. Ninaposema michezo kwa ajili ya amani ni kwamba kama tukiweza kuandaa mchezo kati ya timu mbili kutoka sehemu zinazopambana, timu zao zikiwa uwanjani watu hao wanaweza kuweka chini silaha kwa muda ili waburudike, na kama wakiweka chini silaha basi kunakuwa na nafasi hata ya kuweza kuanza mazungumzo ya amani
Mtangazaji
Hali ya ubora wa ujenzi na wa Uwanja huo pamoja na zana zilizopo ikilinganishwa na zile za viwanja vilivyojengwa na wachina kule Nairobi na Kampala inaweza kulinganishwa?
Bwana Urio.
Ubora wa ujenzi wa uwanja huo pamoja na zana zake ni wa hali ya juu. Rais mstaafu wa Tanzania mheshimiwa Mkapa alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo tarehe 18 Julai 2005, alisifu kasi kubwa ilivyooneshwa na wajenzi wa China, na alitoa shukrani zake kwa ubalozi wa China Tanzania, wafanyakazi wa Tanzania wanaosimamia ujenzi wa uwanja huo na ubalozi wa Tanzania nchini China. Na zana zinazotumika kwenye uwanja huo ni za kiwango cha juu, tunadhani zitatusaidia sana hata tukitaka kutoa ombi la kuandaa michezo ya Afrika (All Africa games) na hata michezo mingine mikubwa ya kimataifa.
|