Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-03 21:09:53    
Balozi wa China nchini Kenya apongeza kuzinduliwa kwa Kituo cha FM cha CRI huko Nairobi Kenya

cri

Wasikilizaji wapendwa, Kituo cha FM cha Radio China kimataifa kimezinduliwa Nairobi Kenya, balozi wa China nchini Kenya Bwana Guo Chongli alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alitoa pongezi kubwa kwa kuzinduliwa kwa kituo hiki. Balozi Guo alisema:

Kituo cha FM cha Radio China kimataifa ni kituo cha kwanza FM cha China kilichojengwa ng'ambo, hivyo kuzinduliwa kwa kituo hiki kumefungua ukurasa mpya wa historia ya matangazo ya China kwa nchi za nje. Kwanza kituo hiki kina umuhimu mkubwa kwa ajili ya kufanya maingiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika. Zamani tuliwahi kuandaa vipindi kadha wa kadha kutangaza kwa kupitia radio za nchi mbalimbali duniani, lakini vipindi hivyo vyote vilikuwa ni vya muda mfupi, ambavyo viliandaliwa nchini China, hivyo hatukuweza kupata wasikilizaji wengi. Katika miaka ya hivi karibuni, radio ya mijini yaani radio ya FM imeendelea kwa haraka sana, kwani usikivu wake ni safi, matangazo yake yanasikika vizuri, na inarusha matangazo kwa njia mbili, hivyo ni bora zaidi kwa kurusha matangazo ya muziki ambayo yanapendwa zaidi na wakazi wengi zaidi wa mijini. Sasa kituo cha FM cha Radio China kimataifa kimezinduliwa Nairobi, Kenya, hakika usikivu wake matangazo ya kituo hiki utakuwa mzuri sana. Tukiandaa vipindi mbalimbali vya kujulisha utamaduni wa China, shughuli za kuendeleza uchumi wa China, desturi na mila za wachina pamoja na lugha ya kichina ili kuwawezesha watu wa Afrika waijue China na kuimarisha maingiliano na maelewano kati ya wananchi wa China na Afrika kutoka kwenye msingi, kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China kimataifa kitatoa mchango mkubwa. Balozi Guo alisema:

Kwa niaba ya ubalozi wa China nchini Kenya natoa pongezi kubwa za dhati kwa kuzinduliwa kwa Kituo cha FM cha Radio China kimataifa. Kama alivyosema waziri wa habari wa zamani wa Kenya Bwana Tuju alivyosema, Kenya inakaribisha China kujenga kituo cha FM nchini Kenya, kwani Kenya inaona kuwa kuanzishwa kwa kituo hiki cha FM kitaweza kuleta utamaduni wa mashariki ya dunia nchini Kenya, kwani katika muda mrefu uliopita, utamaduni wa magharibi ya China unaonekana zaidi mjini Nairobi, kwa mfano mjini Nairobi kuna Kituo cha FM cha Radio BBC, Radio VOA ya Marekani, radio ya Ufaransa, na sasa Kituo cha FM cha Radio China kimataifa kimeanzishwa Nairobi, tunaweza kusema, utamaduni wa mashariki na wa magharibi utakutana hapa, hili ni jambo zuri sana. Mheshimiwa Tuju anatumai kuwa makutano ya utamaduni wa mashariki na magharibi yanawataletea wananchi wa Kenya fursa nyingi zaidi za kujifunza, na makutano ya utamaduni wa aina mbalimbali yatakuwa na umaalum muhimu wa mji mmoja wa kimataifa. Nadhani utamaduni wa China, na matangazo ya Radio China kimataifa yataleta vipindi mbalimbali vitakavyofurahisha wakazi wa Nairobi, ambapo vipindi mbalimbali kuhusu lugha ya kichina, hadithi mbalimbali za China, desturi na mila za wachina pamoja na habari mbalimbali kuhusu maendeleo ya uchumi wa China, hakika vitasaidia China na Kenya, na wananchi wa China na wa Afrika waongeze maelewano na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kila upande. Hatutaki kuona hali kama watu fulani walivyosema, wachina wanakuja, wamejenga radio na wataifanya Kenya au Nairobi kuwa medani ya vita vya kiitikadi. Sisi hatutaki kuanzisha medani ya kivita, tunatumai utamaduni wa mashariki, utamaduni hapa Kenya na utamaduni wa magharibi unaweza kuishi pamoja kwa masikilizano hapa, na kuwawezesha wakazi wa hapa waweze kusikiliza matangazo ya lugha mbalimbali kutokana na mahitaji yao. Tunakubaliana sana na aliyosema mheshimiwa Tuju kuhusu kutumai utamaduni wa mashariki na utamaduni wa magharibi utakutana hapa Nairobi Kenya, ambapo utamaduni wa aina tofauti utakuwepo kwa masikilizano ili kuwaletea watu ujuzi mpya kadha wa kadha hata fursa mpya ya maendeleo. Balozi Guo alisema:

Balozi Guo alisema, sisi pia tunatetea kuwepo kwa aina nyingi mbalimbali za utamaduni, kama tulivyotetea kuwepo kwa dunia ya aina mbalimbali, tunatumai utamaduni wa China tunaoleta utasaidia kuleta masikilizano kati ya utamaduni wa aina mbalimbali, hili ni lengo letu muhimu. Tunatumai kuwa wasikilizaji wetu wengi wa Afrika hasa wasikilizaji wa Kenya watanufaika kutokana na matangazo yetu.