Tokea muda mrefu uliopita, China inachukuliwa kuwa ni nchi kubwa ya uzalishaji bidhaa. Lakini bidhaa nyingi ziwe zile zinazouzwa nchini au zile zinazosafirishwa nchi za nje, zinabandikwa nembo za makampuni makubwa ya kimataifa, bidhaa maarufu zenye hakimiliki za China bado ni chache, na tena hazina nguvu kubwa ya ushindani. Hata hivyo, hali hiyo inaanza kubadilika hivi sasa, wanaviwanda wa China wanajitahidi kuongeza nguvu ya ushindani ya bidhaa za China kwa kuwa na teknolojia muhimu na zenye haki-miliki za kielimu za China yenyewe.
Tokea miaka mingi iliyopita, bidhaa maarufu za nchi za nje zinachukuliwa kuwa ni bidhaa bora kutokana na kwamba kampuni na viwanda vya nchini havina nguvu kubwa ya uvumbuzi na uhafifu wa bidhaa za China, ambapo wanunuzi nchini walikuwa wanapenda kuchagua bidhaa kutoka nchi za nje. Lakini katika miaka ya karibuni, kutokana na kuimarika kwa nguvu ya uchumi wa China, katika baadhi ya sekta, teknolojia za viwanda vya nchini zimezidi vile vya nchi za nje. Kabla ya miaka mitano iliyopita soko la carbon paper lilihodhiwa na bidhaa zilizotoka Ujerumani, Japan na Marekani, ingawa ziliuzwa bidhaa ya aina hiyo ya China, lakini nguvu ya ushindani ya viwanda vya China ilikuwa ndogo kutokana na mali-ghafi muhimu ya rangi ilidhibitiwa na makampuni makubwa ya kimataifa. Mwaka 1997, kampuni ya kemikali ya Ruifeng, mkoa wa Henan ulioko sehemu ya kati ya China ilivumbua aina mpya ya rangi ya carbon paper na kupata hataza yake. Mhandisi mkuu wa kampuni ya Ruifeng Bw. Liu Zong alisema,
"Rangi tuliyovumbua imetokomeza dosari ya rangi ya nchi za nje ya kutoka rangi polepole, kuogopa mwangaza wa jua na rangi kuonekana kama ya kuchujuka."
Teknolojia hiyo inaleta mara moja ufanisi mkubwa kwa kampuni hiyo, ambayo kwa haraka imechukua 90% hivi ya nafasi ya soko la rangi la nchini kutokana na rangi bora na ya bei nafuu zaidi, hivi sasa mauzo ya rangi hiyo inakaribia Yuan milioni 100 kwa mwaka, na rangi za kampuni kubwa za nchi za nje zinaondoka kutoka kwenye soko la China hatua kwa hatua.
Mbali na maendeleo makubwa ya kiuchumi nchini China, sera za maendeleo za kampuni za China katika nchi za nje zimetekelezwa. Baadhi ya kampuni na viwanda vinauza bidhaa zenye haki-miliki za China na za teknolojia ya kisasa katika masoko ya nchi za nje, ambazo moja ya bidhaa hizo ni zana za kukagua usalama wa makontena. Zana za ukaguzi wa usalama wa makontena zinatumiwa sana na forodha za nchi mbalimbali, katika miaka michache iliyopita ni Marekani na Ujerumani tu ambazo zinaweza kuzalisha zana hiyo. Lakini sasa, zana zinazozalishwa na kampuni ya Weishi ya Qinghua ya China zimechukua 57% ya nafasi ya soko la zana hizo duniani, hivi sasa bidhaa hizo zinauzwa katika nchi na sehemu 38 duniani. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Weishi Bw. Kang Kejun alisema, kitu muhimu kabisa cha kufanikisha kampuni ni kuwa na teknolojia muhimu.
"Maendeleo yetu makubwa ni sisi kufaulu kuvumbua teknolojia ya zana za ukaguzi wa makontena zinazoweza kuhamahama, ambayo yanatufanya kuchukua mara moja nafasi ya kuongoza duniani. Licha ya hayo teknolojia yetu ya kukagua vitu vya majimaji wanavyochukua abiria kama ni vitu vya kuwaka moto au kuweza kulipuka pia ni ya pekee duniani. Tumeongoza maendeleo ya sekta hiyo duniani."
Baada ya kuwa na teknolojia muhimu yetu wenyewe, kampuni na viwanda vya China vinaanza kuimarisha bidhaa zake maarufu. Hapo awali, viwanda vingi vya China vilikuwa vituo vya uzalishaji vya makampuni makubwa ya kimataifa, bidhaa zilizozalishwa hapa nchini zilipaswa kutumia nembo za makampuni ya kimataifa, ingawa mauzo yake hayakuwa mazuri, lakini kila mwaka tulipaswa kulipa gharama kubwa ya kutumia nembo zao, tena sehemu kubwa ya faida kutokana na mauzo zilichukuliwa na makampuni hayo. Ili kubadilisha hali hiyo, kampuni na viwanda vya China ambavyo vimefikia kiwango fulani cha teknolojia ya kisasa, vinaanza kuvumbua na kuzalisha bidhaa zake maarufu.
Kampuni ya magari ya Chery ilianzishwa mwaka 1997 na ni kampuni ya magari yenye hataza ya China. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2005, idadi ya magari ya Chery yaliyosafirishwa nchi za nje zilichukua theluthi ya jumla ya magari ya China yaliyosafirishwa nje, idadi ya magari yaliyosafirishwa nje na pato kutokana na mauzo viliongezeka mara dufu kwa mbalimbali kuliko vya mwaka uliotangulia katika kipindi kama hiki. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya magari ya Chery Bw. Yin Tongyao alisema, kampuni zetu hazitakuwa na faida kubwa katika masoko ya dunia, bila kuwa na bidhaa zenye hataza zetu wenyewe.
"Ni kuwa na bidhaa zenye hataza zetu wenyewe, ndipo bidhaa zetu zitakapoweza kuingia kwenye masoko ya kimataifa. Kwani makampuni maarufu ya kimataifa hayapendi kutuacha sisi ambao ni wenzao katika biashara kugawa keki yao. Hii ndiyo chanzo kikuu kwa sisi kuwa na uwezo kuingia kwenye masoko ya dunia wala siyo wengine."
Kama tunasema katika sekta ya uzalishaji ya jadi, kampuni na viwanda vya China vyote vinayafuata makampuni makubwa ya kimataifa hatua kwa hatua kutoka hali ya kuwa nyuma, na kuvumbua teknolojia muhimu za kisasa, basi kampuni na viwanda vingi vya China vilivyovumbua kwa ushirikiano teknolojia ya awamu ya tatu ya mawasiliano ya habari yaani kigezo cha 3G (TD-SCDMA), inaonesha uwezo wa uvumbuzi wa kampuni na viwanda vya China katika sekta ya mawasiliano ya habari. Hivi sasa duniani kuna vigezo vya aina 3 vya teknolojia zenye misingi tofauti vya 3G, ambavyo moja ya vigezo hivyo ni cha TD-SCDMA kilichotolewa na China. Habari kutoka wizara ya mawasiliano ya habari zinasema, kigezo cha TD-SCDMA cha China kimekamilisha mfumo kamili wa uzalishaji kutoka Com Chips hadi zana kamili na kutoka kwa mtumiaji hadi zana za mfumo. Mtaalamu husika amekadiria, thamani ya masoko mawili tu ya ujenzi wa zana za kimsingi za mfumo wa 3G na zana za watumiaji itafikia Yuan za Renminbi trilioni kadhaa katika miaka michache ijayo, endapo kigezo cha China kitakubaliwa na nchi nyingine, basi thamani ya masoko ya siku za baadaye itakuwa kubwa mno.
Licha ya kujitahidi kampuni zenyewe, maendeleo yao makubwa yalitokana na uungaji mkono mpya wa serikali. Wizara ya sayansi na teknolojia ya China kila mwaka inatenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya sayansi na teknolojia zenye kiwango cha kisasa duniani na masoko yenye mustakabali mzuri; idara za kodi nazo zimebuni sera za kupunguza ukusanyaji kodi ili kuhamasisha kampuni na viwanda viimarishe uwekezaji wake katika uvumbuzi wa teknolojia. Aidha serikali za mitaa pia zimebuni sera nafuu zinazoendana na hali za sehemu zake ili kuhimiza kampuni na viwanda kuimarisha bidhaa maarufu zenye hataza za China.
Liwe soko la nchini au masoko ya nchi za nje, ziwe sekta za jadi au sekta mpya, kufuatilia haki-miliki na hataza za China kumekuwa maoni ya kampuni na viwanda vya China kwa pamoja. Hivi sasa bei ya juu kabisa ya bidhaa moja inayosafirishwa nje na China imefikia dola za kimarekani milioni 3 kutoka dola za kimarekani elfu 20 ya kabla ya miaka 5 iliyopita. Katika utandawazi wa uchumi wa dunia, bidhaa za China zina uwezekano mkubwa wa kuathiri sana maisha ya watu duniani.
Idhaa ya kiswahili 2006-02-14
|