Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-15 20:05:11    
Mapishi ya mayai kwa kutumia mvuke

cri

Mahitaji:

Mayai manne, kamba-mwakaje gramu 50, tango moja, pilipili mboga moja, maji gramu 300, mafuta kijiko kimoja, mafuta ya ufuta nusu ya kijiko, mvinyo wa kupikia nusu ya kijiko, chumvi nusu ya kijiko kiasi kidogo cha vitunguu maji.

Njia:

1. koroga mayai kwenye bakuli moja halafu tia chumvi na mimina maji kisha korogakoroga. Kata tango, pilipili mboga na vitunguu maji viwe vipande vipande.

2. mimina mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia kamba mwakaje kwenye sufuria korogakoroga halafu tia vipande vya tango, pilipili mboga halafu korogakoroga na uvipakue.

3. tia maji kwenye sufuria halafu weka bakuli hilo kwenye sufuria na kuchemsha maji ili upike mayai kwa mvuke. Baada ya dakika 10 tia kamba mwakaje, vipande vya tango, pilipili mboga kwenye bakuli hilo endelea kuchemsha kwa dakika 3. Pakua halafu mimina vipande vya vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-15