Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-17 15:17:20    
China yafanya semina ya pili ya nchi za Afrika kuhusu uchafuzi wa maji na usimamizi wa raslimali ya maji

cri

Semina ya pili ya maofisa wa nchi za Afrika wanaodhibiti uchafuzi wa maji na usimamizi wa maliasili ya maji iliyoandaliwa na wizara ya biashara ya China na idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China ilifanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 5 hadi 24 mwezi Januari, maofisa 24 kutoka nchi 14 za Afrika ambazo ni pamoja na Botswana, Burundi, Zanzibar, Ethiopia, Misri, Ghana na Zimbabwe walishiriki kwenye semina hiyo.

Mkurugenzi wa kituo cha maendeleo ya mazingira ya idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China Bwana Chen Yanping kwenye sherehe ya kufungwa kwa semina hiyo alisema:

"Mambo yaliyomo katika semina hiyo ni pamoja na jinsi China inavyozuia na kushughulikia maji taka, sheria na utaratibu husika za China kuhusu usimamizi wa uchafuzi wa maji, hifadhi ya vyanzo vya maji safi, teknolojia na utaalam wa kushughulikia maji taka, mfumo wa upimaji na usimamizi wa mazingira ya China na kadhalika."

Licha ya kutoa mafunzo darasani, semina hiyo pia iliwapeleka wanafunzi kutembelea makampuni yanayoshughulikia maji machafu yaliyoko hapa Beijing na sehemu nyingine nchini China.

Bwana Chen Yanping alisema:

"Katika semina ya kwanza, wanafunzi walionesha hamu kubwa kuhusu teknolojia ya hifadhi ya mazingira ya China, hivyo semina hiyo ikishirikiana na shirikisho la wafanyabiashara wa China na Afrika imefanya kwa mafanikio mazungumzo kuhusu ushirikiano wa miradi ya hifadhi ya mazingira kati ya China na nchi za Afrika. Kwa kufanya mazungumzo hayo, maofisa wa nchi za Afrika wamefahamu zaidi makampuni ya China yanayoshughulikia hifadhi ya mazingira, na kuanzisha daraja la ushirikiano kati yao na makampuni ya China."

Ili kuwafahamisha wanafunzi vizuri zaidi hali ya udhibiti wa uchafuzi wa maji nchini China pamoja na uzoefu wa China katika hifadhi ya mazingira, semina hiyo pia iliwapeleka wanafunzi kutembelea na kukagua kazi ya usimamizi wa hifadhi ya mazingira katika mikoa ya Jiangxi na Fujian, kusini mwa China.

Semina hiyo imesifiwa sana na wanafunzi kutoka nchi za Afrika, Bwana Phillips kutoka Ghana alisema:

"Tumejifunza mambo mengi kutoka kwenye semina hiyo kuhusu jinsi China inavyoshughulikia maji taka, maji ya kunywa, udhibiti na usimamizi wa uchafu wa maji, na hifadhi ya mazingira kwa jumla. Kwa kweli maarifa ya China yatatusaidia sana katika kazi zetu za siku zijazo katika kudhibiti uchafuzi wa maji na kuhifadhi mazingira."

Bwana Phillips alisema baada ya kuizuru China, yeye na wenzake wamepata picha nzuri kuhusu China, wanaona China ni nchi yenye historia ndefu ya utamaduni, imepata mafanikio makubwa ya kiuchumi kwa kufuata sera ya kufanya mageuzi na kufungua mlango kwa nje.

Bwana Bakari Juma Bakari kutoka Zanzibar alisema:

Tarehe 21 Februari mwaka 2005, kwenye mkutano wa ushirikiano wa hifadhi ya mazingira kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Nairobi, naibu waziri mkuu wa China Bwana Zeng Peiyan alisema, China inapenda kuimarisha maingiliano na ushirikiano wa pande mbili mbili na pande nyingi katika hifadhi ya mazingira, na kutoa mapendekezo matatu likiwemo kuimarisha kazi ya kutoa mafunzo ya kiufundi kwa watu husika wa nchi za Afrika.

Mpango wa kuandaa mafunzo ya kiufundi kwa maofisa wa nchi za Afrika wanaoshughulikia hifadhi ya mazingira uligharamiwa na serikali ya China. Japokuwa semina hizo mbili zimepata mafanikio mazuri na zimesifiwa sana na idara husika za China na mabalozi wa nchi za Afrika nchini China, lakini Bwana Chen Yanping alisema, bado wanazingatia kukamilisha masomo yatakayotolewa kwenye semina zijazo ili kuwanufaisha zaidi maofisa wa nchi za Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2006-02-17