Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-21 15:48:06    
Barua 0219

cri
Msikilizaji wetu Mutanda Ayub wa P.O.Box 172 Bungoma, Kenya ametuletea barua akisema kuwa, anafuraha kubwa kuwasiliana na wasikilizaji wengi wa Radio China kimataifa huko Bungoma Kenya. Anaona wasikilizaji wa Radio China kimataifa wanaongezeka siku hadi siku. Katika barua yake hiyo Bwana Mutanda Ayub anasema ana ndoto kuwa siku moja ataonana na watangazaji wa CRI nchini China.

Msaikilizaji wetu Mogire O. Machuki wa kijiji cha Nyankware, P.O. Box 646, Kisii, Kenya anasema katika barua yake anapendekeza Redio China Kimataifa ifanye juhudi za kuchapisha ratiba ya matanganzo ya vipindi vyake. Anakumbuka mara ya mwisho alipokea ratiba ya vipindi vya Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa mwaka 2000, na hadi anaandika barua hii ana uhakika Redio China haijawahi kutoa wala kuchapisha ratiba ya matangazo yake. Anatumai kuwa huduma hii itatekelezwa kuanzia mwaka mpya. Mwisho anaomba kurefushwa kwa kipindi cha "Sanduku la Barua" kwa vile bado ni kifupi sana. Aidha, anawatakia wahariri na watangazaji wote pamoja na wasikilizaji wapenzi wa Redio China Kimataifa kila la kheri.

Tunamshukuru Bwana Machuki kwa barua yake na pendekezo Lake, tunaahidi tutafanya juhudi kukidhi mahitaji yenu kwa kadiri inavyowezekana.

Msikilizaji wetu Bi. Borca M. Ngeresa wa S.L.P 1708 Kisii, Kenya anaanza barua yake akitoa shukrani kwa kumwandikia barua, na anatoa pongezi kwa vipindi vyetu na matangazo yetu, ambayo huko Kisii Kenya wanayapokea kwa njia iliyo safi kabisa. Tena anasema asante kwa kipindi cha chemsha bongo cha mwaka 2005.

Anasema kwa maoni yake vipindi na matangazo vya Redio China Kimataifa vinavutia, na yeye amekuwa na bahati ya kusikiliza matangazo hayo kwa asilimia 80, Redio China Kimataifa ni kama utamaduni wake ama wa huko Kisii, Kenya, na pia imekuwa ni desturi yake.

Maneno aliyosema msikilizaji wetu Borca Ngeresa kweli yanatutia moyo sana, tunamshukuru kwa dhati, ni matumaini yetu kuwa atatuletea barua mara kwa mara.

Msikilizaji wetu Anari M. Albert wa S.L.P 2995 Kisii, Kenya kwanza katika barua yake anatoa salamu za heri ya mwaka 2006. Pia anatoa shukrani kwa wafanyakazi na watangazaji wa Radio China Kimataifa. Anasema anaipenda radio hii kwa sababu ni redio ya kipekee, wasikilizaji wanaipokea kwa roho safi. Anatumai kuwa Redio China kimataifa itatambulika dunia. Anasema yeye na wenzake wamefungua klabu ya waskilizaji wa CRI iitwayo Ngabigege huko Kisii, kwa hivyo Redio China kimataifa huko Kisii Kenya inapamba moto.

Katika barua yake, Bw. Anari M. Albert pia anatoa pongezi kwa wafanyakazi wa Radio China Kimataifa, na anawatakia wawe na mwaka mpya wenye mafanikiio mema na wenye fanaka njema, na kuwa na afya njema kwa maisha yetu yote. Anasisitiza kuwa Redio China kimataifa ni ya wasikilizaji wote daima dawamu, na anatumai kuwa itaendelea hivyo hivyo.

Tunamshukuru kwa dhati na pia kumtakia kila la heri mwaka 2006.

Katika barua yake nyingine anasema kuwa wasikilizaji wa Radio China kimataifa wa huko Kisii wanaipenda Radio hiyo kwa sababu redio ya kipekee inayowaletea habari na burudani mbalimbali. Anatoa shukrani kwa watangazaji wote na anawatakia kila la heri na afya bora kwa mwaka mapya wa 2006.

Anasema kwa sasa anasubiri kwa hamu majibu ya chemsha bongo ya mwaka 2005, na huko Kisii wasikilizaji wengi pia wanayasubiri majibu hayo kwa hamu. Yeye ni mmoja wa walioshiriki kwenye chemsha bongo hiyo, hivi sasa anasubiri kwa hamu kuona kama anaweza kuwa mshindi wa mwaka 2005.

Anasema ingawa huko Kisii baadhi ya watu hawapokei vizuri matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya Radio china yanayopitia kwenye masafa mafupi, lakini kutokana na vipindi vinavyo wavutia wasikilizaji hawakosi kusikiliza matangazo yetu. Pia anatukumbusha tusisahau kuweka picha alizotutumia kwenye jarida la Daraja la Urafiki, na anasema Redio China Kimataifa ni ya wasikilizaji wote daima dawamu.

Msikilizaji wetu Anari M. Albert wa S.L.P 2995 Kisii, Kenya anasema kuwa wasikilizaji wa Radio China kimataifa wa huko Kisii wanaipenda Radio hiyo kwa sababu redio ya kipekee inayowaletea habari na burudani mbalimbali. Anatoa shukrani kwa watangazaji wote na anawatakia kila la heri na afya bora kwa mwaka mapya wa 2006.

Anasema kwa sasa anasubiri kwa hamu majibu ya chemsha bongo ya mwaka 2005, na huko Kisii wasikilizaji wengi pia wanayasubiri majibu hayo kwa hamu. Yeye ni mmoja wa walioshiriki kwenye chemsha bongo hiyo, hivi sasa anasubiri kwa hamu kuona kama anaweza kuwa mshindi wa mwaka 2005.

Anasema ingawa huko Kisii baadhi ya watu hawapokei vizuri matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya Radio china yanayopitia kwenye masafa mafupi, lakini kutokana na vipindi vinavyo wavutia wasikilizaji hawakosi kusikiliza matangazo yetu. Pia anatukumbusha tusisahau kuweka picha alizotutumia kwenye jarida la Daraja la Urafiki, na anasema Redio China Kimataifa ni ya wasikilizaji wote daima dawamu.

Msikilizaji wetu Joel Ngoko wa P.O. Box 1246, Kisii, Kenya ametuletea barua akitoa shukurani sana na kuwatakia afya njema watangazaji na wafanyakazi wa Redio China Kimataifa, na anatumai kuwa Redio China Kimataifa itaendelea kuwaletea wasikilizaji matangazo.

Anasema matangazo ya Radio China Kimataifa yanasikika vizuri sana huko Kisii Kenya. Pia anatoa shukurani kwa Idhaa ya KBC kwa kuongeza muda wa matangazo ya Radio China Kimataifa ili wanaopenda kuisikiliza matangazo ya Radio China kimataifa wapate wakati wa kutosha wa kuyategea sikio matangazo hayo.

Anasema yeye ni mmoja wa mashabiki wakuu wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa; lakini tatizo lake ni kuwa hakuwa karibu na posta ili kupokea kwa urahisi barua tunazomwandikia, hii kwa sababu ya hali ya kazi ambayo inamweka mbali. Lakini sasa ameanza kujipatia muda wa kutosha ili apate kuyasikiliza matangazo ya Radio China Kimataifa. Anasema huu ni mwaka wake wa pili tangu awe shabiki wa Radio China kimataifa. Ni furaha yake kuwa sasa atakuwa nasi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Na kwa vile muda wa matangazo umeongezwa, hiyo ni furaha kubwa kwa wasikilizaji wa Radio China Kimataifa.

Na kwa upande wa maoni anasema anafikiri kuwa tukiongeza muda wa kipindi cha salamu au kuongeza muda wa matangazo yote kwa ujumla katika siku za mbele, wasikilizaji wa Radio China kimataifa watakuwa na furaha kubwa zaidi. Na kwenye barua pia anatoa shukrani kwa Idhaa ya Kiswahili kuwaletea wasikilizaji shindano la chemsha bongo, habari za hapa na pale na Jarida dogo la "Daraja la Urafiki". Anasema hili ni jarida ambalo linastahili kupongezwa na kila mskilizaji!

Mwisho anatoa hongera kwa Idhaa ya Kiswahili na anatumai watangazaji watamtembelea ili kuonana uso kwa uso na kuwafuatia wasikilizaji wengi zaidi kuliko hivi sasa.

Katika barua yake nyingine Bwana Ngoko akitoa pongezi kwa kuwaletea wasikilizaji matangazo kutokana na ushirikiano na shirika la KBC. Kutokana na ushirikiano huo mzuri anapata matangazo vizuri sana. Anatoa shukrani kwa kuongezwa muda wa matangazo yetu.

Bw. Ngoko anaitakia idhaa ya Kiswahili mafanikio katika mwaka 2006, pia anawatakia watangazaji afya njema na baraka tele, anatumai tuzidi kukumbukana na kuwasiliana!

Tunamshukuru sana msikilizaji wetu huyo anayetuunga mkono kwa juhudi. Uungaji mkono wa wasikilizaji wetu wengi unatuhimiza kila mara tuchape kazi bila kulegea.

Msikilizaji wetu Justine N. Anari wa P.O.Box 1246 Kisii, Kenya ametuletea barua akisema, ametuandikia barua hjuku akiwana furaha tele. Anasema anatuunga mkono kwa kazi yetu nzuri, na amefurahishwa sana na kipindi cha chemsha bongo cha mwaka 2005.

Amesema anapendezwa na vipindi vyetu, kwani vinaleta raha, kuburudisha na kuelimisha jamii. Yeye ni mwanafunzi wa kidato cha nne, na amesema kuwa atajiunga na taasisi ya utangazaji, kwani sauti yetu inampa moyo wa kutangaza. Hata marafiki zake wanamuunga mkono awe mtangazaji. Tena anaishukuru KBC kwa kutuongezea muda wa matangazo kupitia idhaa yake ya Kiswahili.

Tunamshukuru sana kwa barua yake, ni matumaini yetu kuwa atafanya juhudi ili afanikiwe kuwa mtangazaji siku za mbele.

Msikilizaji wetu Benson Mbigura wa S.L.P 137, Kakamega, Kenya anaanza barua yake akiwashukuru watayarishaji hadi kwa wapeperushaji wa matangazo haya ya Radio China Kimataifa kwa kutoa huduma kwa wasikilizaji na mashabiki wa CRI kama yeye.

Anasema ameangalia na anafurahishwa sana na ile picha ambayo tulimtumia. Picha yenyewe inahusu wanyama jamii ya swala wakila majani. Lakini ameshtuka kusoma pembeni mwa hiyo picha kwamba hao wanyama ni baadhi ya wale ambao wako hatarini kutoweka. Anaona kuwa jambo muhimu ni kuwaomba wote ambao wanajua umuhimu wa wanyama asilia washirikiane kupitia Radio China Kimataifa kulaani wale ambao huenda wana nia mbaya kuwamaliza wanyama hao.

Anasema wanyama pori walioko nchini Kenya wanajulikana ulimwenguni, hivyo wageni wengi wanafanya utalii nchini Kenya, huku wakiwaletea pesa za kigeni na kusaidia kuimarisha uchumi wa Kenya. Lazima watu wote wahifadhi kwa wanyama hao kwa kuwapa maginzira bora na huru.

Msikilizaji wetu Jim Godfrey Mwanyama wa P.O.Box 1097, Wumanyi Taita, Kenya ametuandikia barua akitoa salamu kwa watangazaji na watayarishi vipindi wa idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa. Anatupongeza kwa kazi yetu ya kuwaletea wasikilizaji vipindi kemu kemu vinavyofundisha, kujulisha na kupanua bongo zao.

Tena anaishukuru Redio China Kimataifa kwa kumwandikia barua mfululizo ambazo zimemtia moyo. Mwishoni anapenda kutoa salamu zake kwa marafiki zake kote duniani kupitia Redio China Kimataifa.

Na sasa kwa wasikilizaji wetu wa 91.9 FM huko Nairobi Kenya tunatoa maswali mawili:

1. Katika matangazo yetu ya saa ya tatu kuanzia saa mbili hadi saa tatu usiku, kuna burudani za muziki na nyimbo, je, ni muziki na nyimbo za aina gani? Je, unavutiwa na nyimbo hizo au la?

2. Taja vipindi vitatu vya kila wiki katika matangazo ya Kiswahili kwenye wimbi la FM. Je unavipenda vipindi hivyo?

Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji mtajibu vizuri maswali haya na kututumia majibu haraka iwezekanavyo, ili waweze kupewa zawadi.

Idhaa ya kiswahili 2006-02-21