Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-08 16:16:00    
Hospitali zenye malipo nafuu kwa ajili ya watu wasio na maptato makubwa

cri

Kutokana na gharama kubwa za matibabu, wachina wengi wakiugua hawaendi hospitali kuwaona madakatari. Lakini katika siku za karibuni, mwandishi wetu wa habari aligundua kuwa, sehemu nyingi nchini China zimejenga hospitali na wadi maalum ambazo zinatoa huduma kwa watu wasio na mapato makubwa, hali hii imeondoa wasiwasi kwa watu wasio na mapato makubwa.

Hospitali ya Shangdi iko kwenye mtaa wa Haidian mjini Beijing. Hospitali hiyo sio kubwa, na hadi sasa imekuwepo kwa miezi miwili tu. Mwandishi wetu wa habari alifika kwenye hospitali hiyo adhuhuri, ambapo ni wakati wa kula chakula, lakini bado aliwaona watu kadhaa wakisubiri madaktari kuwatibu, hata baadhi yao walikuja kutoka mbali. Mzee Zhan Qingliang alisafiri umbali mrefu kutoka nyumbani kwake kusini mwa Beijing hadi kwenye hospitali hiyo iliyoko sehemu ya kaskazini ya Beijing. Alisema:

"Hospitali hiyo inajulikana kote mjini Beijing, nimekuja hapa kutokana na sifa ya hospitali hii. Nimeambiwa kuwa hospitali hii ni kwa ajili ya watu wasio na mapato makubwa kama mimi, malipo ya za matibabu na bei ya dawa hapa sio kubwa, hivyo leo nimekuja kujionea mwenyewe. Sasa nimegundua kuwa hospitali hii kweli ni nzuri, ni hospitali safi na yenye utaratibu mzuri, nadhani watu wanaweza kupata matibabu hapa bila wasiwasi."

Imefahamika kuwa hospitali ya Shangdi inawapokea wagonjwa karibu 200 kwa siku, wakati fulani idadi hiyo inafikia 300. Kwa hospitali hii iliyoanzishwa siku chache zilizopita, idadi kubwa namna hiyo ya wagonjwa wake imeonesha ufanisi wake. Kwa nini hospitali hiyo inaweza kuwavutia wagonjwa wengi?

Hospitali ya Shangdi ni hospitali ya kwanza iliyojengwa na serikali kwa ajili ya raia wenye mapato chini nchini China. Katika siku ambayo hospitali hiyo ilipozinduliwa, mgonjwa wake wa kwanza alilipa yuan za renminbi 5 tu, sawa na senti 63 za kimarekani, kama mgonjwa huyo akienda hospitali nyingine, atalipa mara 10 au zaidi ya kiasi hicho cha fedha.

Mkuu wa hospitali ya Shangdi Bi. Wangling alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kanuni za hospitali hiyo ni kuwawezesha wagonjwa wenye mapato madogo wapewe matibabu.

"Kwa mujibu wa kanuni yetu, wagonjwa wetu hasa ni wakazi wenye mapato madogo wa eneo la Haidian na watu wanaoishi huko kwa muda, ili kila mmoja aweze kupewa huduma za kimsingi za matibabu bila kulipa pesa nyingi."

Kwa kufuata kanuni hiyo, hospitali ya Shangdi inachukua hatua nyingi za kupunguza gharama za matibabu. Kama vile, kuondoa kabisa malipo ya upimaji, na kupunguza bei ya dawa zote kwa asilimia 5. Aidha, hospitali hiyo ina kituo cha kujifungua wanawake kwa wanawake wanaoishi Beijing kwa muda, malipo ya kujifungua kwa kila mja mzito haizidi yuan 1000, sawa na dola za kimarekani 125, lakini katika hospitali nyingine, malipo hayo huwa ni yuan elfu kadhaa.

Je, hospitali hiyo inaendeshwa vipi kwa kutegemea mapato madogo kutoka kwa wagonjwa? Njia muhimu inayochukua hospitali hiyo ni kutumia dawa na zana za tiba za bei nafuu. Kati ya dawa zenye kazi za aina moja, hopitali hiyo huchagua dawa za bei nafuu, lakini sharti la kwanza ni kwamba dawa hizo zifikie vigezo husika vilivyowekwa na serikali, hali kadhalika hospitali hiyo inavyochagua zana za tiba. Kuhusu hali hii, mkuu wa hospitali hiyo Bi. Wangling alitoa mfano mmoja akisema:

"Idara ya mionzi ya hospitali yetu inatumia zana zinazotengenezwa nchini, kwa kutumia zana hizo kuwapiga wagonjwa picha za X-ray, ??malipo hayazidi yuan 40, kama dola za kimarekani 5, lakini wakipigiwa picha hizo katika hospitali nyingine kubwa, watalipa yuan 180, ambayo ni mara 4 zaidi ya malipo ya hospitali yetu."

Sababu nyingine ya hospitali ya Shangdi kuweza kuendeshwa vizuri bila kutegemea malipo makubwa ni kwamba, fedha zinazohitajiwa na hospitali hiyo karibu zote zinatengwa na serikali ya mtaa wa Haidian. Fedha hizo ni msingi wa kuendesha hospitali hiyo, na pia ni uhakikisho wa huduma bora za hospitali hiyo kwa wagonjwa wenye mapato madogo.

Licha ya hospitali maalum kwa watu wenye mapato madogo, kama hospitali ya Shangdi, hospitali za sehemu mbalimbali zimeanzisha wadi maalum za bei nafuu, ili kuwapunguzia malipo ya matibabu watu wasio na mapato makubwa.

Msichana Xu Mengmeng wa mji wa Jinan, mkoani Shandong, alivunjika mfupa wa mguu, hivi sasa amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa siku zaidi ya 10. Kutokana na umri wake na hali ya kiuchumi ya familia yake, daktari anayemshughulikia msichana huyo, Daktari Gao Changhong alimtibu msichana huyo kwa njia moja bila kumfanyia operesheni, njia hiyo inahitaji teknolojia ya hali ya juu zaidi, na ustadi mzuri zaidi wa daktari, lakini bei ya kutibiwa kwa njia hiyo ni nafuu. Daktari Gao Changhong alisema:

"Kama tukimfanyia operesheni, hospitali yetu itapata faida kubwa zaidi, daktari anayefanya operesheni hiyo pia anaweza kupata pesa nyingi zaidi, lakini operesheni hiyo itamletea mtoto huyo uchungu mwingi, na huenda itachukua muda mrefu kwa mgonjwa kupona. Mwishoni, familia ya Xu Mengmeng walitumia yuan za renminbi 2300, kiasi ambacho ni kidogo kuliko walichodhani hapo zamani. Mama wa Xu Mengmeng alishukuru sana pendekezo la daktari Gao, akisema:

"Daktari huyo hakufikiria faida wake hata kidogo, aliyofikiria kwanza ni hisia za mgonjwa na jamaa zake, wadi anayolazwa mtoto wangu ni wadi maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kiuchumi, na tulipunguziwa baadhi ya malipo ya matibabu. Jambo tanalofurahia kabisa ni kwamba kutokana na juhudi za daktari, mtoto wangu hakukumbwa na matatizo mengi."

Mbali na hospitali ya Shangdi ya mjini Beijing na hospitali ya Jinan mkoani Shandong, hivi sasa hospitali za sehemu mbalimbali nchini China zimechukua hatua zinazofanana za kuwawezesha watu wa kawaida kupewa matibabu wakati wanapougua. Kutokana na mifano hiyo mizuri, wizara ya afya ya China imezitaka idara za afya za sehemu mbalimbali zijenge kwa juhudi hospitali za bei nafuu kama hiyo kwa ajili ya kuondoa shida za kiuchumi za watu wenye mapato madogo katika kujipatia matibabu.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-08