Mahitaji
Nusu nanasi, nyanya na kitunguu, kiasi kidogo cha maharage, kamba-mwakaje, yai moja, mchele bakuli mbili, sosi yenye ladha ya pilipili hoho na chumvi.
Njia
1. kata nanasi, nyanya ziwe vipande vidogovidogo, kata kitunguu kiwe vipande.
2. osha kamba-mwakaje halafu wakaushe. Koroga yai. Washa moto tia mafuta kwenye sufuria mimina yai lililokorogwa, korogakoroga halafu pakua.
3. Washa moto tena, tia vipande vya kitunguu, korogakoroga, tia kamba-mwakaje na maharage, korogakoroga halafu tia vipande vya nyanya, wali na yai korogakoroga, halafu tia vipande vya nanasi, na sosi yenye ladha ya pilipili hoho, chumvi korogakoroga kwa haraka, ipakue. Mpaka hapo mseto huo uko tayari kuliwa.
|