Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-14 14:33:11    
Huduma ya mawasiliano ya habari ya televisheni ya kitarakimu

cri

Mtu akitaja televisheni ya mfumo wa teknolojia ya kitarakimu, watu hufikiria picha safi na vipindi murua vya televisheni. Lakini ukweli ni kwamba licha ya uwezo huo televisheni za aina hiyo zina uwezo wa mawasiliano ya habari na kutoa huduma nyingi kwa watu. Hivi sasa katika sehemu zilizoendelea katika mambo ya biashara na fedha, watu wanaotumia televisheni za kitarakimu wanaweza kununua magari, nyumba, kuweka miadi ya kuonana na madaktari, kununua vitu na hisa za kampuni au viwanda, hatua ambayo imerahisishia maisha ya watu.

Mzee Wang Jinpu mwenye umri wa miaka 77, anaishi katika mji wa Hongzhou, mkoani Zhejiang, kitu kinachotumika zaidi nyumbani kwake ni televisheni. Kabla ya mwaka mmoja uliopita, mzee huyu na mkewe walinunua televisheni ya kitarakimu. Jambo linalowafurahisha zaidi ni habari nyingi zinazotolewa kwa kupitia televisheni hiyo, ambayo sasa wanaweza kununua vitabu wanavyovipenda kwa kutumia televisheni yao.

"Katika televisheni kuna habari kuhusu vitabu vilivyouzwa sana katika wiki iliyopita, baada ya kuona vitabu ninavyovipenda, nikaenda kuvinunua, ni rahisi kwangu."

Televisheni za kitarakimu licha ya kutoa huduma kwa wazee kama Bw. Wang Jinpu, zinatoa huduma kamili kwa watu wanaokwenda kazini asubuhi na mapema, na kurejea nyumbani usiku. Mtoto wa Bw. Chen Hong, ambaye ni mkazi wa mji wa Hangzhou, bado ni mdogo, tena ana kazi nyingi, hivyo ananunua mchele, mafuta ya kupikia na vitu vingine kwa njia ya televisheni, sasa hana haja kutumia muda mwingi kufanya shughuli nyingi za nyumbani.

"Kwa mfano, baada ya kuchagua mchele ninaotaka, kazi ninayotakiwa kufanya ni kufanya uthibitishaji, kisha ninatakiwa kuchagua kiasi cha mchele ninachotaka kununua na kufanya uthibitishaji kwenye televisheni tu, nimemaliza utoaji oda."

Mchele alioutaka Bw. Chen Hong, ulipelekwa nyumbani kwake baada ya nusu saa. Mfanyabiashara katika sekta ya usafirishaji bidhaa Bw. Jin Qiang alimwambia mwandishi wetu wa habari, huduma ya kununua vitu televisheni imewaletea wateja wengi wa kudumu.

"Takwimu moja iliyofanywa hivi karibuni inaonesha kuwa, kiasi cha familia elfu 20 hadi 30 zimekuwa wateja wao wa kudumu katika huduma ya kununua vitu kupitia televisheni, ambao kila mmoja wao ananunua vitu kiasi cha Yuan 100 hadi 300 kwa mwezi."

Hivi sasa mjini Hangzhou kuna familia nyingi ambazo si kama tu zinaweza kuona vipindi mbalimbali vizuri zaidi katika televisheni kuliko zamani, tena wanaweza kupata habari nyingi zinazoambatana na maisha yao ya kila siku, na kuletewa urahisi katika shughuli za kununua vitu, kuomba kuwekewa nafasi za tikiti, kununua vyeti vya hisa, magari, nyumba, kuweka miadi ya kuonana na madaktari na kutafuta ajira.

Msaidizi wa meneja mkuu wa kampuni ya televisheni ya kitarakimu ya Hangzhou bibi Tang Yu alipozungumzia huduma ya mawasiliano ya habari ya televisheni ya kitarakimu alisema, "Tunaweza kuitumia kuangalia vipindi vya televisheni, tena tunaweza kuitumia kama chombo cha kutupatia habari nyingi za huduma za maisha yetu, ambazo tumefungua sehemu 6 za huduma za maisha, masomo ya televisheni, mambo ya fedha, burudani ya michezo, mambo ya kiutawala na makazi yetu. Sehemu 6 hizo za huduma zina manufaa sana kwetu, licha ya kutafuta habari tunazotaka, tunaweza kuzitumia habari hizo. Kila siku sehemu hizo 6 zinatembelewa na watu zaidi ya laki 8 na elfu 70."

Habari zinasema, hivi sasa utengenezaji wa vipindi, utangazaji wa vipindi na upelekaji wa vipindi vya televisheni unatumia utaratibu wa tarakimu. Lakini kutokana na kwamba wingi mkubwa wa televisheni zinazotumika hivi sasa ni za aina ya uingizaji (imitate; simulate; analog), hivyo suala muhimu katika ubadilishaji wa utaratibu wa televisheni ya kitarakimu ni kuhusu televisheni zinazotumika nyumbani kwa watu, kuweka Kisanduku kimoja juu ya televisheni zinazotumika hivi sasa, televisheni hizo zinaweza kupokea mawimbi ya kitarakimu.

Naibu meneja mkuu wa kampuni ya televisheni za kitarakimu Bw. Zheng Xiaolin alipoeleza ubora wa teknolojia ya televisheni za kitarakimu alisema, "Ikilinganishwa na televisheni za zamani, televisheni hizo zina njia pana ya upelekaji wa mawimbi ya tarakimu, tuliweza tu kupeleka mawimbi ya vipindi vya televisheni kwa njia kumi kadhaa, lakini kwa televisheni za kitarakimu tunaweza kupeleka mawimbi kwa njia mia kadhaa, tena kwa ubora wa kiwango cha juu. Kitu muhimu zaidi ni kuwa utaratibu huo unaweza kupeleka habari kwa wingi, ambapo watu wanaweza kutumia uwezo huo kuwasiliana na sehemu ya nje badala ya kuangalia vipindi vya televisheni tu, sasa televisheni ni kama kompyuta ya kawaida, tena namna ya kutumia uwezo wake wa mawasiliano ni rahisi zaidi kuliko kompyuta."

Sawa na mji wa Hangzhou, hivi sasa nchini China kuna sehemu na miji 50, ambayo inafanya majaribio ya kubadilisha utaratibu unaotumika sasa hivi kuwa utaratibu wa kitarakimu. Bw. Zheng Xiaolin anaona, kwa kuwa televisheni ni chombo kinachotumika zaidi katika mawasiliano ya habari, uenezaji wa matumizi ya televisheni za kitarakimu ni soko lenye uwezo mkubwa ambao haujatumika bado, na huduma za mawasiliano ya habari zinazotolewa katika televisheni zitawasaidia sana watu katika maisha yao ya kila siku.

Aliongeza, "ni kama televisheni za kitarakimu kufungua supamaketi ya habari, tunaanzisha baadhi ya uwezo unaohitajiwa, kwa mfano, uwezo wa kutoa habari, uwezo wa usimamizi wa wateja, uwezo wa uhamishaji fedha na uwezo wa shughuli za elektroniki za biashara, kazi zetu ni kujenga mashubaka ya kuwekea bidhaa na kuacha wafanyabiashara, idara za serikali au watu binafsi waweke bidhaa na habari kwenye mashubaka hayo na kuendeleza shughuli za biashara.

Uchumi na maendeleo

Idhaa ya kiswahili 2006-03-14