Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-04 17:00:25    
Serikali ya China yatoa ramani za ujenzi wa nyumba kwa wakulima

cri

Ili kuwawezesha wakulima wa China waishi katika nyumba zenye hali nzuri na bei nafuu, wizara ya ujenzi ya China tarehe 21 ilitoa seti za ramani za nyumba zilizosanifiwa kwa ajili ya wilaya na tarafa 1887 nchini China, ili kuelekeza shughuli za ujenzi wa nyumba za wakulima kwenye miji midogo ya wilaya nchini China.

Katika sherehe ya kukabidhi seti hizo za ramani na kusaini makubaliano husika na vijiji vinavyofanya majaribio, naibu waziri wa ujenzi wa China Bwana Huang Wei alisema, kujenga nyumba ni lengo la wakulima wa China katika maisha yao yote, kazi hiyo ni matumizi makubwa kwa wakulima wa China katika maisha yao yote, hivyo kuimarisha uelekezaji na usimamizi wa ujenzi wa nyumba na kuinua sifa ya ujenzi wa nyumba ni muhimu sana kwa ujenzi wa vijiji nchini China.

Imefahamika kuwa seti hizo 22 za ramani za ujenzi wa nyumba zilizotolewa na wizara ya ujenzi ya China zimewekwa vielelezo vya usanifu wa nyumba za vijijini kwenye sehemu 16 nchini China, pamoja na ramani za miundo ya nyumba, ramani za njia ya kuingiza maji na kuondoa maji nyumbani, na kuonesha kanuni za kubana matumizi ya raslimali na kuhifadhi mazingira.

Bwana Huang Wei alisema, seti hizo za ramani za ujenzi wa nyumba za vijijini zenye vigezo mbalimbali zilikamilishwa kwa miaka miwili na wataalamu wa Taasisi ya usanifu wenye vigezo wa ujenzi wa nyumba ya China, hivyo zinaweza kutoa uelekezaji mzuri kwa ujenzi wa nyumba vijijini.

Bwana Huang ameainisha kuwa, hivi sasa katika ujenzi wa nyumba vijijini, watu wengi walitumia ovyo ardhi, bila kujali kubana matumizi ya nishati na matumizi ya fedha, ambapo nyumbani nyingi za vijijini huwa zinatumika kwa miaka 15 tu, huu kweli ni ubadhilifu mkubwa kwa wakulima binafsi na jamii nzima.

Wilaya ya Malan ya mji wa Gujiao mkoani Shanxi ni moja kati ya wilaya zilizopewa seti za ramani za ujenzi wa nyumba, Bwana Zhang Xiaozhong wa wilaya ya Malan alisema, kutokana na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya wakulima, wakulima wana matakwa mapya juu ya nyumba zao za kuishi. Wizara ya ujenzi ya China kupeleka seti za ramani za ujenzi wa nyumbani vijijini, kazi hiyo inaweza kuepusha ujenzi wa marudio nyumba zenye sifa ya chini vijijini, seti hizo za ramani za ujenzi wa nyumba vijijini zinahitajiwa sana katika juhudi za kujenga vijiji vya aina mpya nchini China kwa hivi sasa.

Mwaka huu China imeanzisha mpango wa kujenga vijiji vya aina mpya, mpango huo umeainisha kuwa, lazima kuboresha sura ya vijiji, kusisitiza kufanya vizuri mipango ya ujenzi wa vijiji, kuwaelekeza wakulima wajenge nyumba zao kwa hali mwafaka, na kuhifadhi mitindo ya ujenzi wa nyumba vijijini katika sehemu mbalimbali nchini China kutokana na kanuni za kubana matumizi ya ardhi, kujenga nyumba zenye seti kamili ya zana, kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira.

Wizara ya ujenzi ya China itatoa taarifa kuzihamasisha idara za usimamizi za sehemu mbalimbali nchini China zieneze ujuzi kuhusu ufundi wa ujenzi wa nyumba katika vijiji vya kote nchini, kuinua sifa ya ujenzi wa nyumba vijijini na kuboresha sura ya vijiji vya sehemu mbalimbali nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-04