Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-05 16:47:41    
Mapishi ya vipande vya nyama ya ng'ombe, kuku na figili

cri

Mahitaji:

Nyama ya ng'ombe gramu 70, nyama ya kuku gramu 70, figili gramu 100, kiasi kidogo cha uyoga, chumvi, M.S.G, maji ya wanga, sukari, vitunguu maji, vitunguu saumu, wanga wa magadi nusu kijiko, na mvinyo wa kupikia nusu ya kijiko.

Njia:

1. Kata nyama ya ng'ombe na nyama ya kuku ziwe slesi, kata figili iwe vipande, weka uyoga kwenye maji mpaka uwe laini, na uukate uwe slesi.

2. Weka slesi za nyama ya ng'ombe na nyama ya kuku ndani ya bakuli moja, tia chumvi, M.S.G na wanga wa magadi, korogakoroga.

3. Tia mafuta kwenye sufuria pasha moto, mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia slesi za nyama ya ng'ombe na nyama ya kuku korogakoroga kwa haraka, kisha zipakue.

4. Washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu korogakoroga, tia vipande vya figili na uyoga, korogakoroga, halafu tia slesi za nyama ya ng'ombe na nyama ya kuku, tia chumvi, sukari, mvinyo wa kupikia, korogakoroga, mimina maji ya wanga, korogakoroga na kisha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.