Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-11 19:47:18    
Rais Kibaki aongoza wakenya kuomboleza

cri

Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametangaza siku 3 za maombolezo kwa watu waliokufa katika ajali ya kuanguka kwa ndege ya jeshi tarehe 10, ambapo watu 14 kati ya 17 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walikufa.

Rais Kibaki akiwahutubia wananchi wa Kenya kupitia televisheni tarehe 10 jioni, alitoa salaam za rambi rambi na kuelezea kushtushwa na habari hizo.

Miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni pamoja na wabunge watatu, manaibu waziri wawili, marubani wawili wa jeshi la anga la Kenya na maofisa wa serikali. Na ofisa mwingine wa serikali na watumishi wawili wa ndege hiyo walijeruhiwa vibaya.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba wanasiasa hao ilianguka karibu na Marsabit, mji uliopo kilimota 450 kaskazini mashariki ya Nairobi baada ya kugonga mlima na kuwaka moto wakati ikiwa njiani kuwapeleka katika mkutano wa kusuluhisha mapambano ya kikabila.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana. Kuna maofisa waliosema kuwa, wakati ajali inatokea mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.

Shughuli za Bunge nchini Kenya zimeahirishwa ili kuomboleza vifo vya wabunge sita waliofariki dunia kutokana na ajali ya ndege iliyotokea tarehe 10.

Spika wa bunge la Kenya Bw. Fracis Ole Kaparo alisema kwamba, shughuli za bunge zimeahirishwa hadi hapo mazishi ya wabunge hao yatakapomalizika.

Bw. Kaparo Alidondokwa na machozi hadharani akisema, bunge haliwezi kuendelea na shughuli zake kutokana na msiba huo.

Alisema, kamati ya kuandaa mazishi ya wabuge waliofariki dunia imeundwa, na bunge litafanya kadiri liwezavyo kuwasaidia wafiwa.

Shughuli za kupiga vita ukimwi za ongezeka

Serikali nchini Kenya imeanzisha mapambanano makali dhidi ya ugonjwa wa ukimwi, ambayo lengo lake ni kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo hadi kufikia asilimia 5.5 ifikapo 2009.

Kike wa Rais Mama Lucy Kibaki alisema, serikali itatimiza lengo hilo kwa kuwapa wagonjwa dawa za bure ili kupunguza makali ya ugonjwa.

Alisema, asilimia ya wagonjwa wa ukimwi inaendelea kupungua kwa kiwango kikubwa, kutoka asilimia 14 hadi asilimia 6.1 mwaka huu.

Aliongeza kuwa sekta nyingi hasa za afya zimepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa kuna dawa za kutosha katika hospitali mbalimbali.