Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-14 19:56:26    
Teknolojia ya uchapishaji ya China kuwafaidisha waafrika

cri

Ifuatayo ni mahojiano kati ya mwandishi wetu wa habari Bwana Ali Hassan na mwandishi wa vitabu wa Kenya Bwana Abud Bashir Mchangano.

Ali: China ni taifa mojawapo ambalo limeanzisha ushirikiano na bara la Afrika ikiwemo Kenya, ndiyo maana ukipita mitaani utaona maduka ya kichina, hospitali za kichina na mikahawa mingi ya kichina, na sasa wamezindua kituo cha FM kwenye mitabendi 91.9 hapa Nairobi, Kenya. Hii ni ishara kwamba wanalenga sana soko na ushirikiano na nchi za Afrika. Una ushauri gani kwa serikali ya China katika kuwafaidisha waandishi wa vitabu nchini Kenya na sekta ya uchapishaji kwa ujumla?

Mchangano: Kwa hakika China imeendelea na inakua kwa haraka sana. Ina historia ndefu ya uandishi na uchapishaji. Japokuwa tunatofautiana katika lugha, lakini tunaweza kushirikiana katika teknolojia ya uchapishaji. Kwa kuwa lugha ya Kiswahili inapanuka hata Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa inasikika hapa Kenya. China imeendelea sana katika biashara, tunapenda kushirikiana na China katika teknolojia ya uandishi.

Serikali ya China inatupa misaada ya kifedha, lakini kama mvuvi kumpa samaki hafaidiki, mpe chombo cha kuvulia samaki atafaidika. Watupe sisi nchi changa katika kushirikiana nao teknolojia ambao sisi watatuwezesha hata kama ni ushirkiano wa kuunda bidhaa. Zile bidhaa ambazo wataka wachina kutul;etea sisi tunahitaji. Wakileta vifaa na teknolojia ya kuzalisha bidhaa zinazohitajika sana hapa nchini Kenya si kama tu itatusaidia sisi nchi changa, bali pia watafaidika weneywe.

Ali: Wewe ni mwandishi wa vitabu wa siku nyingi, utampa ushauri gani yule chipukizi ambaye angetamani kuwa mwandishi wa vitabu kama wewe?

Mchangano: Kuandika vitabu kuna sehemu mbili ambazo ni muhimu. Sehemu ya kwanza ufanye uchunguzi katika ile mada ambayo utaandika, kwa mfano lugha ya Kiswahili, au lugha yoyote. Unataka utafute mbinu za kufundishia lugha ile, na ujue maana yake katika kufundisha lugha ile kuna matatizo gani ambayo mwanafunzi anaweza kuyapata kutoka lugha yake ya mama na lugha ya Kiswahili, na uchunguzi unataka kusoma sana.

Pili ukishika kalamu ya kuandika, ukiyapelekea wachapishaji, itakuwa ni bahati kubwa sana ikiwa ni mchapishaji atakurudishia mswada au kukuambia rekebisha hapa rekebisha pale, ikiwa roho yako si ngumu, unavunjika moyo mara moja, na utaacha. Lakini hiyo ndiyo njia waandishi wengi wamepitia, hii inastahili uvumulivu, na ufanye uchunguzi zaidi. Hivyo ndivyo kidogo kidogo wameweza kufika katika hali ya kuitwa sasa ni mwandishi ambaye anatamaniwa na wachapishaji wengi. Ukishafika kiwango hicho, utajua kwamba umefika kwangu kizuri. Lakini pia usishangae maana kufanya uchunguzi na kutazama namna gani unaweza kuboresha ule uandishi wako.